“Dark Web” ni Tishio la Usalama wa jamii

Imefasiriwa na Dkt. Hossam Mostafa

  • | Wednesday, 22 May, 2024
“Dark Web” ni Tishio la Usalama wa jamii

     Mtandao wa Giza, au kile kinachoitwa “Dark Web”, unazingatiwa kuwa ni nafasi isiyoonekana kwenye Mtandao wa intaneti ambayo haiwezi kuifikiwa kupitia zana za utafutaji za kawaida, na ufikiaji wa nafasi hii inayozunguka na hatari unahitaji matumizi ya programu maalum na teknolojia, kama vile kivinjari cha “Thor” ambayo huficha utambulisho wa mtumiaji na mahala pake.

Mtandao wa Giza hutumika kwa malengo ambayo mengi yake ni kinyume cha sheria, ambapo Mtandao wa Giza ni mazingira yawezeshayo kuenea kwa halifu, kwani usiri na ufichaji wa mtumiaji unaobainisha nafasi hii unaruhusu kwa watumiaji kufanya halifu zao, ikiwa ni pamoja na biashara haramu, ulaghai, na ukiukaji wa siri za wengine, bila hofu ya mashtaka.

Yafuatayo ni maelezo mafupi kuhusu aina maarufu zaidi za halifu zinazotendwa kupitia mtandao wa giza:

Biashara ya Mihadarati  na Silaha: Biashara ya mihadarati na silaha ni mojawapo ya halifu zinazoenea sana kwenye mtandao wa giza, na watumiaji wanaweza kununua aina yoyote ya mihadarati au silaha kwa kutumia sarafu za kidijitali kama vile Bitkoin bila kufichua utambulisho wao.

Udhalilishaji wa kijinsia: Inazingatiwa kuwa moja ya halifu za kutisha zaidi kwenye mtandao wa giza; Watumiaji wanaweza kupata picha na video za mashambulio ya kingono, haswa dhidi ya watoto, kwa lengo la kufurahisha na labda ulaghai.

Biashara ya viungo vya binadamu: Ni uwanja wa biashara hii haramu ambapo wafanyabiashara na wale wanaotaka kuuza au kununua viungo vya binadamu hukusanyika, na kupitia kwake mipango ya halifu za mauaji inaandaliwa kwa lengo la kutoa viungo vya binadamu kwa biashara na kuvionyesha.

Kuuza nyenzo za ponografia: Watu pia hujirekodi filamu za ponografia na kuzichapisha kwenye jukwaa hili kwa kubadilishana na pesa nyingi. Kuajiri watu kwa ajili ya kutekeleza halifu na operesheni za kigaidi.

Kufanya vitendo vya unyama na unyanyasaji: kama vile kutangaza mubashara kwa magenge ambayo yameteka nyara watu, na kuanzisha mnada kwa kulipa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kinafikia maelfu ya dola, kwa yule alipaye zaidi kuchagua mbinu ambazo mwathiriwa aliyetekwa nyara atauawa, au kurekodi kanda za video zinazothibitisha operesheni za mauaji ya kutisha kwa moja ya watu na kuuza kanda hizo kwa gharama kubwa mno.

Ulaghai, utapeli na udanganyifu: Walaghai na wadanganyifu hufanya kazi yao kwenye mtandao wa giza, wakitumia usiri wa mazingira kuiba taarifa za kibinafsi na data za kifedha kutoka kwa waathiriwa.

Utakataji wa Pesa: Mtandao wa giza unatumiwa kutakatisha pesa zinazotokana na shughuli haramu kama vile biashara ya mihadarati na biashara haramu ya binadamu.

Jinsi Mtandao wa giza unavyohudumia Fikra potofu na ugaidi?

Makundi yenye fikra potofu hutumia mtandao wa giza katika kuendesha shughuli zake zenye shaka, miongoni mwake ni, kwa mfano:

Kueneza mada zenye fikra kali: Mtandao wa giza hutumiwa kueneza madhumuni yenye fikra kali, ikiwa ni pamoja na hotuba ya chuki, vurugu, na propaganda za kigaidi, na usiri huwaruhusu watumiaji kueneza madhumuni haya bila vikwazo au uangalizi.

Uvutaji na kunadi fikra zao: Watu wenye fikra kali hutumia Mtandao wa Giza kuvutia wanachama wapya kwa kundi ambalo wanalifuatia na kuunda vikundi vya kigaidi ili kuvutia wanachama wapya, na kuunda mtandao mkubwa zaidi wa kundi kwa kiwango kikubwa.

Kuuza silaha na vilipuzi: Mtandao wa giza hutumika kuuza silaha na vilipuzi, ambavyo watu wenye fikra kali hutumia katika kutekeleza halifu zao za kigaidi.

Hatari na changamoto za Mtandao wa giza kwa usalama wa jamii

Mtandao wa giza una idadi ya hatari zinazoufanyia kuwa changamoto inayohitaji kazi ili kukabiliana nayo na kuipambana kwa uthabiti ili kuhifadhi usalama wa jamii, miongoni mwa hatari hizi ni:

Tishio la usalama wa kitaifa: Halifu za mtandao wa giza ni tishio kubwa kwa usalama wa kitaifa; ambapo zinaweza kutumika kueneza propaganda za fikra kali na kupanga mashambulizi ya kigaidi ambayo yanapigia usalama wa nchi na kusababisha kutishia utulivu wa jamii.

Kusababisha madhara kwa watu na jamii: Halifu za mtandao wa giza husababisha madhara makubwa kwa watu na jamii inayoweza kupelekea uraibu wa mihadarati, kusambaa unyanyasaji na unyonyaji wa kingono, kuenea kwa matatizo ya akili, na kupoteza imani katika jamii.

Ugumu wa uchunguzi na mashtaka: Usiri wa Mtandao wa Giza hufanya kazi ya kuchunguza halifu na kuwashtaki wahalifu kuwa ngumu sana; ambapo mtandao huu hautoi data yoyote kuhusu wanaotuhumiwa kwa kuutumia au kufanya halifu kupitia mtandao huo, jambo ambalo hufanya kazi ya kuainisha tambulisho zao na kuwafungulia mashtaka kuwa ni jambo gumu.

Mwishoni, mapinduzi ya kiteknolojia tunayoyashuhudia katika zama yetu ya hivi sasa yanatuletea changamoto nyingi kama vile yalivyotupatia fursa nyingi, na kila mtu; watu binafsi na taasisi, anapaswa kunufaika na fursa ambazo teknolojia inatupatia, kwa kuzingatia changamoto zinazotukabili kutokana na maendeleo haya makubwa, na kwa hivyo ni muhimu Kushughulikia hatari za mtandao wa giza, kupitia:

  • Kuongeza ufahamu wa hatari za halifu za mtandao wa giza, hasa kwa vijana.
  • Kuunga mkono na kuimarisha utafiti na maendeleo katika uwanja wa teknolojia za kupambana na halifu za mtandao wa giza.
  • Ushirikiano wa kimataifa, kushiriki data, na kuendeleza mikakati ya pamoja ya kupambana na halifu za mtandao wa giza.
  • Kukuza elimu na funzo; Kwa lengo la kuimarisha maadili ya demokrasia, usamehe, heshima, na kuhimiza kufaidika na teknolojia.
  • Kuhakikisha kuwa gunduzi za kisasa zinachukuliwa kuwa ni nyenzo za ujenzi sio ubomoaji, maendeleo sio uharibifu, na sababu za maendeleo na ustawi sio ufisadi na kupotoka.

 

Kitengo cha Uchunguzi na Tafiti

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.3

Please login or register to post comments.