Kuzuia chakula kuingia Gaza…. Siasa ya kizayuni inayoendelea kwa muda mrefu

Imefasiriwa na Bw. Farid Mohammed

  • | Friday, 24 May, 2024
Kuzuia chakula kuingia Gaza…. Siasa ya kizayuni inayoendelea kwa muda mrefu

 

     Mamlaka ya Kizayuni hufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina tangu tarehe 7 Oktoba 2023 katika Ukanda wa Gaza, kupitia njia na nyenzo kadhaa kama vile: Milipuko ya anga, operesheni za ardhini, kuboromosha hospitali, na njia nyingine zinazotumiwa na mamlaka ya kizayuni kama silaha zinazolenga mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza unaozingirwa.

Na labda silaha ya "Kuzuia chakula"‎ ni moja ya silaha maarufu zaidi zinazotumiwa na mamlaka hiyo katika uhalifu huu, na unahisabiwa miongoni mwa halifu za kivita zinazojulikana zaidi zilizofanywa nayo katika uvamizi wake unaoendelea dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya nusu mwaka. Ingawa sio sera mpya kwa uvamizi huo dhidi ya Ukanda wa Gaza, ilhali inazingatiwa kuwa mbaya na kali zaidi kwa wakazi wa Ukanda huo tangu 1967 BK, yaani tangu kuanzia ukaliaji ‎wa kizayuni katika Ukanda wa Gaza, tangu tarehe hiyo mamlaka ya kizayuni inatawala mfuko wa chakula ‎wa kipalestina katika Ukanda wa Gaza‎, na hudhibiti mahitaji ya chakula kwa wakazi wake ili kutumia chakula kama silaha ya kuwatawala. Kwa muda wa miongo kadhaa, ukaliaji umeharibu uwezo wa ukanda wa kuzalisha chakula chake, Pia ilipunguza nafasi ya wakazi wake kupata maji safi ya kunywa na vyakula vyenye manufaa, hivyo, kujua siasa hii iliyopanuliwa ni muhimu kuelewa njaa inayoenea kwa sasa huko Gaza.

ukaliaji huo ulifuata sera ya "Kuzuia chakula" katika Ukanda wa Gaza, ambapo uliharibu mashamba na kuiba zaidi ya 10% ya ardhi ya kilimo huko Gaza, na kungoa miti zaidi ya 226000, ukaliaji huo pia uliimarisha mzingiro wa anga na baharini kwenye Gaza, ulilipua uwanja wa ndege ambao ulijengwa mnamo 1998 kama sehemu ya Makubaliano ya Oslo, Mnamo 2002, ukaliaji huo uliharibu bandari ambayo ilijengwa kwa ushirikiano wa Uholanzi na Ufaransa, Kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa katika Mkataba wa Sharm El-Sheikh mwaka 1999, ukaliaji pia ulipanga maeneo ambayo Wapalestina wanaweza kuvua samaki, ambapo uliwekea mipaka katika eneo dogo sana la pwani, ukielekeza pigo kali kwa moja ya nguzo za mfumo wa chakula huko Gaza. Taratibu hizi, pamoja na vikwazo vikali vinavyozidi kuongezeka kwa usafirishaji wa watu na bidhaa, zimesababisha uhaba mkubwa wa chakula ndani ya ukanda, Hili lilithibitishwa na ripoti iliyochapishwa katika jarida la kiingereza la kitiba mwaka 2002, ambalo lilisema kwamba idadi ya watoto wanaokabiliwa na utapiamlo huko Gaza imeongezeka maradufu katika miaka miwili.

Katika kipindi hiki, Waziri Mkuu wa mamlaka wa kizayuni -wakati huo- Ariel Sharon alianza kutambua kwamba haiwezekani tena kueneza mamia ya wanajeshi wa jeshi la ukaliji ndani ya Ukanda wa Gaza ili kulinda mkaliaji elfu nane katika Ukanda huo, Pia aliamini kwamba kwa kutekeleza “mpango wa kuchanua fungamano” wa upande mmoja, na utawala wa Kizayuni utaweza kujionyesha kuwa umemaliza kukalia Gaza kwa mabavu, jambo ambalo lingesaidia kuunda utengano kamili kati ya Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa ujumla, Pia litaliruhusu utawala wa Kizayuni kupanua ujenzi wa makazi ya wakaliaji katika Ukingo wa Magharibi kuviimarisha pia.

Hakika, mwaka 2005, serikali ya ukaliji ilisambaratisha makazi haramu ya Gaza, Ilieneza wanajeshi wa jeshi la ukaliji kwenye mipaka ya Ukanda wa Gaza, ikaanzisha kambi za kijeshi moja kwa moja nje ya Ukanda wa Gaza, na kuongeza matumizi ya ndege zisizo na rubani, Iliunda eneo la kujitenga ambalo upana wake kuanzia mita 150 hadi 500, hukata ardhi ya kilimo, pia Iliwalazimu wakulima walime mazao  yenye majani madogo kama vile mchicha, figili na letusi (Kabichi ya saladi); ili kutozuia mwonekano wa askari wa ukaliaji walioko kwenye mipaka ya Ukanda wa Gaza.

Tangu wakati huo, ukaliaji umeanza kuandaa orodha ya bidhaa ambazo haziwezi kuingizwa ndani ya Gaza, Iliweka vikwazo vikali kwa idadi ya bidhaa za kibiashara na za kibinadamu, jambo ambalo lilithibitishwa na Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Palestina na mashirika mengine kadhaa mwaka 2006, ambapo zilitaja kwamba  vikwazo vya ukaliaji vimesababisha uhaba wa unga, mibadala ya maziwa na dawa, Haya yalitangazwa kwa uwazi na Dov Weisglass, mshauri wa waziri mkuu wa ukaliaji na pia mkuu wa Bodi ya katibu wakuu wa Chuo Kikuu cha Haifa akisema: sera ya serikali” Ni kama kukutana na mtaalamu wa malisho. Wapalestina watapunguza uzito wao kwa haki, lakini hawatakufa”. Kuwekwa kwa vikwazo hivi kulisababisha kuongezeka kwa umaskini, na kujenga hali ya uhaba wa chakula, na wakati huo serikali ya ukaliaji iliacha wajibu wake kuhusua hali hii. Ambapo Ilidai kuwa kwa mujibu wa matini  ya " mpango wa kuchanua fungamano” wa upande mmoja, ambayo inasema kwamba baada ya kuondoka kwa vikosi vya uvamizi kutoka Gaza "hakutakuwa na msingi wa madai kwamba Ukanda wa Gaza ni eneo linalokaliwa kwa mabavu", Mwendesha mashitaka wa mamlaka ya kizayuni alitangaza kwamba utawala wa Kizayuni haujabeba wajibu wowote kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza kama jeshi linaloukalia kwa mabavu.

Katika mwaka 2007, mamlaka ya kizayuni iliweka rasmi mzingiro dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza, ambao idadi yao ilifikia milioni 1.5 wakati huo, katika eneo ambalo ni miongoni mwa maeneo yenye watu wengi zaidi duniani, Kama sehemu ya maelekezo ya Baraza la Usalama la Kizayuni "Alkabinet" la kulazimisha kufungwa juu ya ukanda huo, Baraza lilipendekeza kupunguza usambazaji wa mafuta na umeme, na kuruhusu tu kuingiza bidhaa muhimu za maisha.

Utapiamlo na kuzihesabu kalori

Mamlaka ya kizayuni  iliendelea sera zake zinazolenga utapiamlo kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza, Hii inafanywa kwa kuingiza bidhaa za msingi za chakula kwenye ukanda huo kwa idadi maalum, jambo ambalo lilifichuliwa na jarida la “New York Review” katika makala iliyochapishwa Desemba mwaka jana.   Mtafiti Sarah Roy alinukuu kutoka taarifa kwa tarehe 3 Novemba 2008 iliyotumwa na Ubalozi wa Marekani mjini Tel Aviv kwa Waziri wa Mambo ya Nje:” Kama sehemu ya mpango wa kina wa kuizingira Gaza, maafisa wakuu wa Kizayuni walisema [kwa maafisa wa ubalozi] katika minasaba kadhaa kwamba walikuwa na nia ya kuweka uchumi wa Gaza kwenye hatihati ya kuporomoka bila kuusukuma ukingoni”.

Vyakula vilivyopigwa marufuku kuingizwa Gaza na mamlaka ya kizayuni ni pamoja na (chokoleti, mafuta ya zeituni, asali na baadhi ya matunda), ambavyo vilisanifishwa kama "bidhaa za ghali". Na hisa ya nyama mbivu kwa watu wote kiliwekwa kuwa ndama 300 kwa kila wiki.

jambo lililosukuma kampuni ya chakula huko Gaza kuwasilisha ombi kwa Mahakama Kuu ya Israeli dhidi ya vizuizi vya mwisho mnamo 2008. Majibu ya mwendesha mashitaka ya uvamizi huo yalikuwa kwamba serikali ilihesabu kwamba wakazi wa Gaaza walihitaji ndama 300 tu kwa kila wiki ili kutosheleza mahitaji yao ya kibinadamu. Kwa kuzingatia utamaduni wa zamani kuhusu masuala ya haki za msingi za binadamu kwa Wapalestina, mahakama ya mamlaka ya kizayuni ilikataa kuingilia kati.

Baadaye, shirika la haki za binadamu ndani ya taasisi ya Kizayuni litwalo: “geshah” lilianza kufanya kazi kwa ajili ya kufichua Vita vya kisheria vilivyodumu kwa miaka mitatu na nusu kwa kufichua rekodi zinazoonyesha kuwa Israel ilifikia kundi la aina mbalimbali za kanuni za hisabati ili kubainisha kiasi na aina ya chakula iliyoruhusu kuingia Gaza. Mnamo mwaka wa 2012, shirika hilo lilifanikiwa kurusha waraka uliotolewa na Wizara ya Vita ya Kizayuni, Kulingana na kifani kilichoandaliwa na maafisa wa Wizara ya Afya, chini ya anuani: "Matumizi ya Chakula katika Ukanda wa Gaza - Mistari mekundu". kinajumuisha majedwali na mipango yanayoelezea kwa kina ulaji wa chakula wa kila siku kulingana na jinsia umri, na kuhesabu kiwango cha chini cha kalori ambacho kitaruhusu "mlo wa kutosha kwa kuishi bila maendeleo ya utapiamlo".

Hati hiyo ilidhani kuwa Wapalestina huko Gaza hawataweza kuagiza "bidhaa za kimsingi za chakula" ila kwa idadi ndogo ya unga, mchele, mafuta, matunda, mboga, nyama, samaki, maziwa ya unga na mbadala wa maziwa ya mama kwa watoto wachanga, Ambazo mamlaka ya kizayuni ilikadiria zinaweza kuingizwa katika lori 77 kwa kila siku. Pamoja na kuongezwa kwa madawa, vifaa vya matibabu, vifaa vya usafishaji, na vifaa vya kilimo, idadi ya lori zinazoruhusiwa kuingia kila siku (siku 5 kwa wiki) ilifikia lori 106. pamoja na malori 60 mengine yanayopakizwa ngano kila wiki, yataingia kupitia mikanda ya kusafirisha mizigo kwenye kivuko cha Karni. mwishoni jumla ya lori zinazoruhusiwa kuingia kila siku ni malori 118.

Hesabu hizi zilidhania kwamba vyakula ambavyo vingeingia Gaza vingegawanywa kwa usawa baina ya wakazi, nayo ni dhana ambayo haijawahi kutokea katika muktadha wowote wa kihistoria au kijiografia. mamlaka ya kizayuni pia ilidhania kuwa ni asilimia 10  tu ya mahitaji ya chakula ya wakazi yatapatikana kutokana na matunda na mboga zinazozalishwa huko Gaza – nayo ni kukiri kwa wazi kiwango cha uvamizi huo unaoendelea kudhibiti maisha ya Wapalestina.

Ni wazi kutokana na kile tulichokitaja, na kwa mujibu wa data iliyotajwa katika ripoti iliyorushshwa na mtandao wa "Siha Maqomit", kwamba kabla ya uvamizi unaoendelea sasa dhidi ya Ukanda wa Gaza, ambao unaweza kuitwa: “vita vya mauaji ya kimbari” kwa muda mrefu,  mamlaka ya kizayuni imefanya wengi wa wakazi wa Ukanda wa Gaza hukumbwa na utapiamlo, ambapo Watoto (watoto wachanga) walikuwa hukumbwa na kifo mara saba zaidi kuliko wale waliozaliwa katika maeneo ya karibu sana na Ukanda wa Gaza, kama vile Beersheba au Tel Aviv.

Taarifa hizi tulizozionyesha ni za nyakati za kawaida, sio nyakati za uadui wa kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, Ambavyo vimetokea mara tano katika miaka 15 iliyopita, Katika kipindi ambacho mzozo unazidi, mamlaka ya kizayuni inapunguza kiwango cha chini cha ulaji wa chakula kwa wakaazi wa Ukanda wa Gaza, ambayo tutaelezea katika makala inayofuata:

Kuzuia chakula kuingia Gaza…. Siasa ya kizayuni inayoendelea muda mrefu(2)

Kitengo cha Lugha ya Kiebrania

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.