Wanadai .. Tunasahihisha

24

  • | Wednesday, 29 June, 2016

Kwa hakika yale madai yanayotangazwa na makundi hayo inafungamana na kuwepo utambulisho unaofaa ambao unajumuisha wafuasi wake wote, na kuwafanya wapendane na washikamane, utambulisho huo wa kundi la Daesh na makundi mengine yanayofanana nalo ule utambulisho hutegemea uongo na udanganyifu, ambapo wawadanganya watu wote duniani kwamba wao ndio wanaoteseka wakiuawa na kupatwa na adhabu kali na kunyimwa na uhuru wao wa kufanya ibada za dini ambayo pia ni uongo na udanganyifu, wanadai pia kwamba wanayoyafanya miongoni mwa jinai za kikatili ni kwa ajili ya kujibisha uadui mkali unaofanywa dhidi yao na dini yao, basi vitendo wanavyovifanya ni vya kutetea na kulinda mawazo yao jambo linalosababisha  mauaji, na kuwachinja watu ili kulipiza kisasi kwa mateso waliyopatwa nayo, kisha wakaeneza wazo hilo lisilo sawa duniani, kwa hiyo waislamu wapya duniani huwaunga mkono madaesh hasa wanapowaona kama ni watu waliopatwa na dhuluma nyingi mno ambapo huuawa, basi waislamu wapya hawa hukubali na kukiri kuwa wanapaswa kuwatetea kwani wao ni waislamu sawa sawa nao, kwa hivyo Madaesh  wameweza kutumia utambulisho wa kidini ili kudhibiti maoni ya waislamu wapya kwa ajili ya kuwatumia vibaya ili kutekeleza maslahi zao wenyewe na matumai yao, wakifaidika na uchache wa ujuzi na utamaduni wao wa kidini na uhamasa wao mwingi wa kuwanusuru waislamu ndugu zao, isipokuwa hivyo tukiangalia kwa makini tutagundua kwamba aghalabu ya waislamu na ujumla wao hawayaamini mawazo ya Daesh, wala hawakubali vitendo vyao, zaidi ya hayo hawana shaka yo yote kwamba vitendo hivyo havihusiani kabisa na Uislamu, bali wengi wa wanaoamini mawazo ya makundi haya ni vijana wanaojaa uhasama na haraka ya kufanya kitu hasa waliojiunga na Uislamu tangu wakati chache au wale vijana wadogo ambao hawajatambua ukweli wa dini yao au pengine wale kikundi cha vijana wa kimagharibi wanaosikia dhiki kwa sababu ya taratibu za maisha bila ya kuwa na uchochezi wa kufanya kitu kipya, basi kwa hiyo vijana hao huvutwa kwa maisha ya wafanyaji jihad kwa mujibu wa mtazamo wao, ile maisha inayojaa ushindi na nishati kubwa inayofanana na maisha ya mhusika mkuu katika kazi za kisanaa zinazotekelezwa kule    Hollyood, ambapo yule mhusika mkuu hupata kutiliwa mkazo zaidi kuliko wahusika wengine.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.