Wanadai .. Tunasahihisha

25

  • | Friday, 1 July, 2016

Kwa hakika watu hawa wamechukua baadhi ya matini za kisheria wakapuuza kwa kusudi baadhi nyingine kama vile zile hadithi zinazokanusha ulazimisho wa Hijra, kama vile kauli yake Mtume (S.A.W.) iliyonukuliwa katika Sahihul Bukhari kutoka kwa Ibnu Abbas (R.A.): “hakuna Hijra baada ya kufungua Makkah, lakini ni Jihadi na nia, mtakapotakiwa kwenda jihadi basi nendeni". Na aidha kauli yake Mtume (S.A.W.) kwa mtu aliyekuja kuapa mbele yake kwamba atafanya Hijra ili kumnsuru kama ilivyonukuliwa katika Sahihul Bukhari: “kwa kweli hakuna Hijra baada ya kufungua Makkah, lakini nitampa ahadi juu ya kuliazimika kwa Uislamu" , na kwamba Maulamaa wameziambatanisha hdithi hizo kwa kusema: kwa kweli Hijra iliyoisha ni ile  Hijra inayofanyika kutoka Makkah kwenda Madinah ya Mtume Muhammad (S.A.W.)

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.