Wanadai .. Tunasahihisha

26

  • | Friday, 1 July, 2016

Uhamiaji uliobaki ni kuhamia (kuacha) ukafiri, maovu na madhambi bila ya kujali mahali po pote pa kukaa panapofaa kwa  kumwabudu Mwenyezi Mungu pasipo na ulazimisho au unyanyasaji kwa mujibu wa kauli yake  Mtume (S.A.W.) kwa mswahaba wake aitwaye Fadeek katika hadithi iliyoopokelewa na Bin Hibaan katika kitabu chake cha sahihi yake aliposema: Ewe Mtume, kuna watu wanaodai kuwa asiyekuhama basi, ameangamizwa, Mtume (S.A.W.) alisema: "Ewe Fadeek, usimamishe Swala, utoe Zaka, uache maovu japokuwa mahali po pote utakapokaa katika ardhi ya jamaa zako kama unavyopenda".
Hadithi hizi na nyinginezo ni nyingi ambazo hazitiliwi mkazo na mwanachama wa Daesh zinathibitisha kwamba uhamiaji ulikuwa ukifungamana na kipinda cha kufanyiwa maudhi Mtume (S.A.W.) na maswahaba wake na washirikina wa Makkah, na kwamba mwislamu akiweza kujikinga nafsi yake na dini yake, akaweza kuishi kwa amani mahali po pote duniani, basi si wajibu juu yake kuhama, bali kwa mujibu wa kauli yao kwamba ardhi zote ni nchi za ukafiri, lakini siyo nchi zote za ukafiri ni lazima kuzihamia na kwenda nchi nyingine, bali uhamiaji huwa wajibu juu ya mtu wakati ambapo kukosa uwezo wa kufanya ibada katika nchi anapokaa.
Muhatasari wa maneno katika suala la uhamiaji ni kwamba uhamiaji sio wajibu ila katika hali ambayo mwislamu hawezi kumpwekesha Mola wake wala hawezi kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa amani na uhuru,  na pia uhamiaji haupaswi kuwa kwenda nchi fulani au kwa taifa maalum la watu, bali uhamiaji wa kweli huwa kwa mahali po pote anapoweza mwislamu kupata amani kuhusu nafsi yake na dini yake, kwa hiyo basi uhamiaji hauhusiani kabisa na ardhi zinazodhibitiwa na kundi la Daesh.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.