Wanadai .. Tunasahihisha

27

  • | Saturday, 2 July, 2016

Aya hiyo imeteremshwa katika washirikina wa Makkah kwa maana ya kwamba: “Na piganeni nao kwa kumzuia mwislamu asipatwe na fitina katika dini yake na ili kumlinda mwislamu asidhulumiwa, au kwa ajili ya kumkinga mwislamu kugeuzwa na itikadi yake akawa mkafiri baada ya kuwa mwamini., na kwamba amri ya kupigana na makafiri hapa ilikuwa katika hali  ya kujitetea na kujihifadhi na kupambana na uadui walioufanya washirikina dhidi ya Mtume Muhammad (S.A.W.) na mwaswahaba wake (R.A.), isitoshe bali anayefuatilia na kusoma vyema vita vya Mtume wa Mwenyezi Mungu huona  kwamba vita hivyo vyote vilikuwa kwa sababu ya kimantiki inayokubalika kiakili, ambapo vilikuwa kwa ajili ya kutetea uadui na kulinda Daawa na waislamu katika nchi zao, hayo yote hayatajwa katika matini hata moja miongoni mwa matini za Daesh, na hata wanachama wa Daesh hawakutaja kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): "Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua". (Al-Anfal: 61), na pia wamesahau kwa makusudi kauli ya Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu". (Al-Mumtahina: 8), na kwamba aya hizo mbili ni aya zinazohusiana na mapigano yo yote yanayotokea baina ya waislamu na wasio waislamu, wakati wo wote na mahali po pote.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.