*Al-Azhar: Gaza inakabiliwa na mauaji ya kimbari kwa msaada wa baadhi ya taasisi na serikali*
*Al-Azhar: Mauaji ya Wazayuni yanawakilisha fedheha kwa wanadamu*
*Al-Azhar inalaani mauaji ya "Nuseirat" ... na inatoa wito kwa watu huru wa ulimwengu kukusanyika kwa ajili ya Gaza*
Al-Azhar inalaani vikali mauaji ya kikatili yaliyofanywa na magaidi wa uvamizi wa Kizayuni leo Jumamosi dhidi ya raia katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza, ambayo ilisabibisha vifo vya mashahidi zaidi ya mia mbili, na mia nne waliojeruhiwa katika jinai mpya iliyoongezwa kwenye historia ya Wazayuni weusi dhidi ya Wapalestina wanaomiliki ardhi hiyo.
Al-Azhar inalaani kuendelea uungaji mkono na baraka za baadhi ya tawala na serikali kwa jinai ya chombo hiki cha kikatili na kutekeleza mauaji ya umwagaji damu dhidi ya raia wasio na ulinzi, na kuuthibitishia ulimwengu mzima kwamba ni vita vya mauaji ya kimbari vinavyofanyika katika ardhi ya Palestina.
Al-Azhar inalaani na kukemea mauaji hayo ya kikatili, na bado inaendelea kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na watu wenye dhamiri huru ili kuzuia umwagaji damu huko Gaza na kulinda na kutoa misaada kwa raia, watoto, wanawake na wazee, ikitaka kutoa hesabu kwa mamlaka ya Kizayuni kwa sababu ya kukiuka sheria na kanuni zote za kimataifa, na ikitaka pia kutonyamaza juu ya mauaji hayo ya magaidi wa Kizayuni ambao walifanya uharibifu mkubwa duniani, jambo linalozingatiwa ni fedheha kwa binadamu.