Baada tu kumpokea mialiko rasmi kutoka kwa raisi wa nchi tatu barani Asia, Mheshimiwa Imamu Mkuu Profesa/ Ahmed Al-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharief, aitikia mialiko hiyo na kufanya ziara rasmi kwa nchi tatu za (Malaysia, Thailand, na Indonesia) Kusini Mashariki mwa Asia.
Mwanzoni mwa ziara yake kwenda Malaysia, Mheshimiwa Imamu Mkuu alikutana na viongozi wakuu wa kidini, kitamaduni na kisiasa, ili kuunga mkono uhusiano wa Al-Azhar na Malaysia, na kuimarisha msimamo wa Kiislamu kuhusu kukabiliana na mashambulizi ya mamlaka ya kizayuni dhidi ukanda wa Gaza.
Baada ya hayo, Mheshimiwa Imamu Mkuu alielekea mji mkuu wa Malaysia “Kualalumpur”, na huko amekutana na Waziri Mkuu wa Malaysia, “Datu Seri Anwar Ibrahim”, na kufanya mashauriano na viongozi wa kidini, kitamaduni, na taasisi za kiraia nchini kwa ajili ya kujadili njia za kuimarisha jukumu la Al-Azhar, kufaidika na uzoefu wake mkubwa, na kupanua katika kuanzisha vituo vya Al-Azhar vya kufundisha lugha ya Kiarabu nchini Malaysia.
Waziri Mkuu wa Malaysia alisisitiza uungaji mkono wa nchi yake kwa msimamo wa Sheikh wa Al-Azhar wa kukataa uadui dhidi ya Gaza na kuomba kwa kumaliza haraka kwa uadui huu wa kikatili, na ameongeza kwamba Malaysia inachukua misimamo yake kutoka hotuba za Sheikh wa Al-Azhar zinazoelezea majanga ambayo ndugu zetu wa Gaza wanazikabili.
Kwa upande wake Mheshimiwa Imamu Mkuu alielezea furaha yake kwa ziara yake kwa Malaysia, na akishukuru mapokezi mazuri aliyoyapata, na kubainisha undani wa uhusiano unaoiunganisha Al-Azhar na Malaysia, hasa wanafunzi wa Malaysia wanaosoma Al-Azhar ambayo inajumuisha takriban wanafunzi 7,000, akieleza kwamba wanafunzi wa Malaysia wanafurahi kwa ufadhili maalum wa Al-Azhar, na wao ndio wanastahili huduma hii kwa sababu ya maadili na adabu yao .
Kisha Mheshimiwa Imamu Mkuu alikwenda kwa mji mkuu wa Thailand “Bangkok”, na akaelekea kwa Kituo cha Kiislamu ili kutekeleza Sala ya Ijumaa na mkusanyiko wa waumini, akibadilishana nao mazungumzo ya kirafiki na picha za ukumbusho.
Pia mheshimiwa Mfalme “Vajiralongkorn”, wa Thailand, katika jumba la Kifalme mjini mkuu “Bangkok” alipokea mheshimiwa Imamu Mkuu profesa/ Ahmed Al-Tayyeb kwa kuwepo kwa Malkia Suthida, Malkia wa Thailand; ambapo mheshimiwa Mfalme alimkaribisha mheshimiwa Imamu Mkuu, akielezea furaha yake kwa ziara hii ya ukarimu, na akasifu juhudi za Al-Azhar za kueneza na kukuza maadili ya mazungumzo, amani, uvumilivu na kuishi pamoja.
Mheshimiwa Imamu Mkuu alithibitisha kwamba Al-Azhar iko tayari kupokea Waislamu wa Thailand, akionyesha kwamba Al-Azhar inatoa ufadhili wa masomo 160 kila mwaka kwa Waislamu wa Thailand ili wajiandikishe katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na kwamba Al-Azhar iko tayari kuongeza ufadhili wa masomo unaotolewa kwa watu wa Thailand, kwa njia inayokidhi mahitaji ya umma wa Kiislamu nchini Thailand, akionyesha kwamba Al-Azhar inafafanua na inafasiri Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake na kuwafundisha Waislamu duniani kote, na hata kwa wasiokuwa Waislamu, na kwamba ujumbe wa Al-Azhar ni kueneza ujumbe wa Uislamu, ambao msingi wake ni amani baina ya watu wote.
Na katika kituo chake cha tatu barani Asia, Mheshimiwa Imamu Mkuu alielekea "Indonesia" na kukutana na raisi wa nchi "Joko Widodo" kwenye ikulu ya Merdeka katika mji mkuu "Jakarta", ili kujadili njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja katika nyanja tofauti, zikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, kutoa mafunzo kwa maimamu na walinganiaji katika Chuo cha Kimataifa cha Al-Azhar, kuimarisha ushirikiano kati ya Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali na vituo vya Indonesia vinavyofanya kazi katika uwanja huo huo, na kuanzisha vituo kadhaa vya Al-Azhar vya kufundisha Kiarabu katika majimbo mbalimbali ya Indonesia.
Kwa upande wake, Rais "Joko Widodo" amesisitiza kwamba Indonesia inafuata misimamo yote ya Imamu Mkuu kuhusu kuunga mkono masuala ya ulimwengu wa Kiislamu, hasa misimamo yake ya heshima katika kuunga mkono Ghaza na kukataa hujuma dhidi ya raia wasio na hatia, akisifu msimamo wa Misri katika kurahisisha kuingia misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza tangu mwanzo wa uadui, akithibitisha kwamba msimamo wa Sheikh wa Al-Azhar unaafikiana na msimamo wa Indonesia.
Kwa upande wake, Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali kinasisitiza kwamba ziara ya Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa/ Ahmed Al-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar kwa Kusini mashariki mwa Asia ni ziara inayoonyesha jukumu la kistaarabu na kihistoria kwa serikali ya Misri na pia jukumu la kisayansi na kitamaduni kwa Al-Azhar Al-Sharif, kikieleza kwamba ziara hii ilishuhudia mapokezi mazuri, na shukrani kubwa kwa taasisi ya Al-Azhar na Sheikh wa Al-Azhar. Na miongoni mwa malengo makuu ya ziara hii ni yafuatayo:
- Kueneza maadili sahihi ya Uislamu yanayosimamia usawa na wastani.
- Kujadili njia za ushirikiano, kukuza jukumu la Al-Azhar Al-Sharif, na kufaidika na uzoefu wake mkubwa, na kueneza huduma zake za kida'wa na kielimu katika nchi hizo tatu.
- Kujadili masuala maarufu ya hivi sasa kidini na kijamii, na kukutana na Maimamu, Walinganiaji, Mufti, na wale wanaosimamia Taasisi za Da'wa na Fatwa.