Wazayuni na mauaji ya kimbari yanayoendelea dhidi ya Wapalestina tangu 1948

Imefasiriwa na Bw. Eslam Ragab

  • | Thursday, 18 July, 2024
Wazayuni na mauaji ya kimbari yanayoendelea dhidi ya Wapalestina tangu 1948

     Mauaji ya Israel dhidi ya Wapalestina yalianza kabla ya tangazo la kuanzishwa kwa nchi ya Israel, na miongoni mwa mauaji ya kikatili zaidi ni mauaji ya Der Yassin yaliyofanywa magharibi mwa Al-Quds tarehe 9 Aprili 1948, na yaliyotekelezwa na makundi mawili ya kigaidi ya kizayuni: Irgun na Shtern.

Mauaji haya yametokea baada ya wiki mbili tu tangu kutiwa saini kwa mkataba wa amani kati ya wenyeji wa kijiji hicho na wakuu wa wazayuni, na kwa sababu ya tabia yao ya kuvunja ahadi, basi wamevunga mkataba huo na kundi la kigaidi la Irgun na Shtern walifanya mashambulizi hayo usiku wakati wa kulala, na ingawa utetezi wa Wapalestina, basi msaada wa kijeshi uliofika kwa wazayuni uliwawezesha kudhibiti kijiji hicho na kuzilipua nyumba zake zote, na kuwaua wengi wa wakazi wake, wakiwemo watoto, wanawake, na wazee, idadi ya wahanga ilifika kati ya 250 na 360, Wazayuni hawakutosha kwa mauaji, lakini walifanya mateso ya kikatili kama kukata miguu,  mikono, na kuwabaka wasichana mbele ya familia zao.

Mauaji ya Al-Lid 1948:

Wakazi wa mji wa Al-Lid, walio ni karibu na Ramallah, walikataa mauaji na kimbari ya kizayuni, jambo lililowasukuma vikosi vya kizayuni vya Palmach vinavyofuata taasisi ya Al-Haganah vilivamia mji huo mnamo 11 Julai 1948, na viliwachukua wanaume wote wenye umri zaidi ya miaka 16, vikawanyonga na risasi, na kufyatua risasi kila anayetembea,  jambo lililopelekea kutawanyika miili barbarani.

Magenge ya kizayuni hayakujali kwa jaribio la wakaazi waliokimbilia na kuingia msikiti, na waliuvamia chini ya uongozi wa Ishaq Rabin, na kuwauwa wakaazi hao hadi idadi ya vifo ilifikia takriban mashahidi 426.

Mauaji ya Khan Yunis 1956:

Jeshi la Israel lilitekeleza mauaji ya kikatili, kama mauaji ya kimbari ya Khan Yunis yaliyokuwa shahidi juu ya umwagaji damu wa jeshi hilo, basi 3 Novemba 1956 jeshi la Israeli lilivamia mkoa wa Khan Yunis katika Ukanda wa Gaza, na kuwauwa Wapalestina zaidi ya 500 (wengine wanasema kuwa idadi imefikia 1,600).

Mauaji haya yaliacha jeraha kubwa katika kumbukumbu ya Wapalestina kwa sababu yalipelekea kuwauwa wapiganaji wa makundi mbalimbali ya kipalestina, pamoja na wapiganaji Waarabu walioshirikiana katika vita vyao dhidi ya Wazayuni, mauaji hayo yaliendelea kwa muda wa siku tisa kamili.

Mauaji ya Msikiti wa Ibrahimi 1994:

Baada ya jinai za jeshi, basi raia wa kizayuni aitwaye Baruch Goldstein alipata mazoezi, risasi kutoka jeshi na kufanya mauaji kwa kuwaua Wapalestina 29 waliokuwa wakisali sala ya alfajiri katika mwezi wa Ramadhani mnamo Februari 1994, na pia jeshi lilimsaidia kwa kufunga milango ya Msikiti wa Ibrahimi, kisha mzayuni huyo aliulizwa na wapalestina baada ya kumaliza risasi yake.

Mauaji ya Jenin 2002:

Jeshi la Israel liliingia kambi ya Jenin mwezi wa Aprili 2002 ili kuwashinda muqawama wa kipalestina uliokuwa unasumbua mamlaka ya kizayuni, na mapigano yaliongeza ndani ya kambi hiyo dhidi ya wanajeshi wa kizayuni waliofanya mauaji ya kimbari na walizuia vyombo vya habari na madaktari kuingia kambini.

Hayo ni baadhi ya mauaji ya jeshi la kizayuni katika ukanda wa Ghaza na jirani zake, na kuna mauaji mengine mengi, ambayo ningetaka kuyataja yote, tusingekuwa na nafasi ya kutosha kuyataja

Mauaji ya Gaza 2023:

Mbali na mauaji hayo, baada ya 7 Oktoba mwaka 2023, yanakuja mauaji yaliyo makubwa zaidi ya wazayuni katik historia ya kizayuni, yaliyoendelea tangu miezi tisa hadi sasa hivi, mauaji yaliyoharibu miundombinu ya Gaza na sekta za kiafya, na yalisababisha vifo vya makumi ya maelfu ya Wapalestina wakiwemo watoto, wanawake na wazee waliouwawa bila ya huruma wala ubinadamu.

Kwa hakika, mamlaka ya kizayuni tangu mwanzo wa ukaliaji hapo mwaka 1984 mpaka sasa inatekeleza mauaji ya kimbari na jinai za kikatili dhidi ya Wapalestina kwa mbinu mbalimbali ikiwemo mabomo na silaha ambazo ni marufuku kutumika, maroketi na silaha za kikimekali na mbinu nyinginezo.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.