Mchango wa Vyombo vya Habari kukuza Uzalendo

Imeandaliwa na Dkt., Alaa Salah Abdulwahed

  • | Monday, 22 July, 2024
Mchango wa Vyombo vya Habari kukuza Uzalendo

     Vyombo vya habari ni zana mojawapo zana muhimu za kueneza fikra na utamaduni mbalimbali, zilizo sawa na zisizo sawa, kwani vinawaathiria hadhira kwa mawazo ambayo yanatangazwa na kurushwa kupitia kwake. Kwa hiyo jamii zote zilitakiwa kuvitumia vyombo hivyo kwa njia inayoisaidia kueneza maadili na fikra sahihi.

Uzalendo ni miongoni mwa fikra muhimu na utamaduni wa maana ambao unatakiwa kufundishwa kwa wananchi wote kupitia njia na vyombo tofauti kwa sababu hali hii inachangia sana maendeleo ya jamii na nchi husika, jamabo linalotweelezea hoja za uzingatifu na uangalifu wa nchi kuu duniani kwa vyombo vya habari katika kupitisha mamlaka yake na kueneza utamaduni wake.

Inafahamika kwamba kuipenda nchi ni sifa mojawapo sifa za kimaumbile wanayo wanadamu wote, kwa hiyo Mtume wetu alishtuka aliposikia kutoka Waraqa bin Noufal kwamba watu wake watamalazimisha ahamie nchi yake kwa kuwa anaipenda sana na amekuwa hataki kuihamia kabisa, na alipokuwa akitoka alisema kauli yake: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba Makka ndiko nchi bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu na kwangu pia na angalau watu wake wamenilazimisha nihamie nisingetoka hata kidogo"

Na kuipenda nchi si sifa ya wanadamu tu, bali wanyama pia, kwa hiyo si jambo la kushangaza kuwa sheria imekuja kuwahimiza wananchi kuipenda na kuitetea na kupigana kwa ajili yake hata mmoja akipotezwa na maisha yake huwa na fadhila kubwa nayo ni kuwa shahidi aliyekufa kwa ajili ya nchi yake, ambapo shahidi huyu amepewa cheo cha juu kabisa na kutunukiwa na Mwenyezi Mungu na watu pia, Mwenyezi Mungu Amesema: {Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia yaMwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakininyinyi hamtambui} [2/154].

Zaidi ya hayo Mwenyezi Mungu Amewaruhusia wananchi kutangaza upendo wao kwa nchi na kuwa wako tayari kufanya lolot kwa ajili ya nchi hiyo, hata ikiwa ni kupigana na wale wanaotaka kaiharibu nchi na kuwatokeza watu wake kutoka makwao: {Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu,na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu} [60/9].

Wakati huo huo Mwenyezi Mungu Amewaelekeza waumini kuwapenda na kuamiliana na wale wasiofanya uadui wowote dhidi ya nchi kwa wema na uadilifu hata wakiwa si waislamu: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema nauadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [60/8].

Kwa hiyo tunaona kuwa uzalendo na kuipenda nchi katika sheria ndiyo sababu ya kupenda ama kutopenda na chanzo cha kujitolea na kujitahidi kuzuia madhara yoyote dhidi yake nchi tunakotoka. Inafahamika kuwa matini nyingi katika Qurani na Sunna za Mtume zimesisitiza ukweli wa kwamba uzalendo na kuipenda nchi ni sehemu ya imani inayotokana na maumbile ya kibinadamu, na kwamba hisia za upendo kwa nchi ni sifa inayopatikana kwa kila mwenye mwenendo ulio sawa na akili timamu, hata akiwa anaishi nje ya nchi yake hiyo.

Maumbile haya ya kuipenda nchi na kuwa na hamu kuinusuru na kuitukuza ni yale yale kwa wanadamu wote kwa dini mbalimbali, uraia tofauti, makabila mbalimbali n.k. Kwa hiyo Uislamu ulitambua haki ya kuipenda na kuitetea nchi kwa waislamu na wasio waisalamu, ambapo wote wanawajibika kuinusuru nchi na kusaidiana pamoja kulinda nchi yao bega kwa bega. Pia, heshima ya nchi ni sehemu ya heshima ya mtu kwa hiyo Mtume (S.A.W.) alisisitiza kuwa: "Ye yote anayeuliwa akiwa anatetea heshima yake au mali zake au jamaa zake au ardhi yake basi huyu ndiye shahidi" Inafahamika kuwa ardhi ndiyo nchi.

Kwa hiyo tunatakiwa kuachana na hitilafu na migongano ya mitazamo na maoni na badala ya hayo tushirikiane na tufanye pamoja kuinua nchi katika nyanja mbalimbali na kushikamana kwa lenga la kuendeza nchi na kuyatatua matatizo yake. Wala hatusahau mchango wa mwanamke na nafasi yake kufanikisha juhudi za maendeleo na ustawi wa nchi, ambapo mwanamke ndiye nusu ya jamii ambaye anawalea nusu wengine na kuwafundisha kuanzia uchanga mpaka uzima. Kwa hivyo mwanamke ana mchango ambao hausahauliki kujenga ustaarabu na kuimarisha hali ya jamii na nchi.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.