Je, idadi ya mashahidi huko Gaza inaweza kufikia 186,000? Kituo cha Al-Azhar kinafuatilia maelezo muhimu ya makala ya "Guardian" la kiingereza

Imefasiriwa na Bw. Said Moshtohry

  • | Tuesday, 23 July, 2024
Je, idadi ya mashahidi huko Gaza inaweza kufikia 186,000? Kituo cha Al-Azhar kinafuatilia maelezo muhimu ya makala ya "Guardian" la kiingereza

     Katika makala mpya iliyochapishwa na gazeti la "The Guardian" la kiingereza, swali liliibuliwa kuhusu uwezekano wa kufika idadi ya mashahidi wa Gaza kwa 186,000 hata ukisitishwa uadui wa kizayuni dhidi ya Gaza, ikieleza matatizo yanayokabili mchakato wa tathmini pamoja na kushindwa kwa wahusika ndani ya Gaza wa kuhesabu idadi ya mashahidi wa mashambulizi yanayoongezeka kwa haraka, na kuwepo kwa elfu 10,000 chini ya magofu.

Na chini ya anuani ya: “Kwa nini watafiti wanaogopa kufika idadi ya mashahidi katika Gaza kwa 186,000?”, basi gazeti la “The Guardian” liliripoti kwamba ikisitishwa vita vya Gaza, basi idadi ya mashahidi hayatasitishwa kwenye idadi iliyotangazwa hadi sasa; kwa sababu vita haviwaui watu kupitia mapigano ya moja kwa moja tu, basi kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wataalamu wa magonjwa katika miaka ya hivi karibuni kuhusu kuenea kwa magonjwa wakati wakati wa mizozo ya silaha kuhusu kile wanachoita “hasara za vita zisizo za moja kwa moja”,  basi vifo wakati wa vita na mizozo hutokana na mambo mengine kama: utapiamlo, ukosefu wa dawa, na hali mbaya ya maisha, ambayo yanakuja kwa sababu ya matokeo wazi ya athari za vita.

Na kulingana na wataalamu hao, basi idadi ya wahanga wa hali mbaya za kivita inaongezeka zaidi ya wahanga wa vita wa moja kwa moja, wakitoa mfano kwa kilichotokea huko “Timor Mashariki”, ambapo takriban watu 19,000 waliuawa au kutoweka kati ya 1974 na 1999, wengi wao wakati wa kuingilia kwa Indonesia, lakini namba hii haikaribii kutokana na kuhesabu gharama kamili ya mwanadamu; inakadiriwa kuwa watu zaidi ya 84,000 hatimaye walikufa kwa sababu ya kuhama kwa pamoja na njaa, jambo linaloashiria kuwepo vifo vinne visivyo vya moja kwa moja kwa kila kifo cha moja kwa moja.

Kwa mujibu wa yaliyopita, basi mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Afya ya Idadi ya Wakazi katika Chuo Kikuu cha McMaster nchini Canada alitarajia kutokea vifo vinne visivyo vya moja kwa moja kwa kila kifo cha moja kwa moja katika Ukanda wa Gaza, lakini hali mbaya zilimfanya yeye na wenzake kutarajia kurikodi viwango vya juu zaidi, ambapo waligundua kuwa uwiano wa watu wanne kwa mkabala wa mtu  mmoja unaweza kumaanisha jumla ya vifo vitakuwa elfu 186.000 huko Gaza.

Na kulingana na kilichoangaliwa na watafiti, basi kilichotangazwa kinazingatiwa kuwa matokeo ya "kushtua" kwani inawakilisha 8% ya wakazi wa Gaza ambayo idadi yao inafika milioni 2.4, lakini hayo ni  makadirio karibu sana ya ukweli hasa kwa pamoja na kuporomoshwa kwa sekta ya afya, na kabla yake iliporomoshwa mifumo ya maelezo, na athari zake katika kutegemea kwa idadi ya vifo vinavyotokana na vita sawa sawa ikiwa vya moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Kutokana na yaliyopita tunagundua kwamba vita vya moja kwa moja na sio pekee sababu kuu ya idadi ya vifo, lakini kuna sababu zisizo za moja kwa moja zinazotokana nazo na zinasababisha kuongezeka kwa idadi ya wahanga, na kuhusu Gaza, basi uharibifu wa kimakusudi kwa  miundombinu ya sekta ya afya wakati wa vita vya mwisho ulichangia kuongeza idadi ya mashahidi.

Lakini wakati huo huo, tunaashiria kwa kipindi cha kabla ya vita, kwani ripoti iliyotolewa na taasisi ya haki za binadamu ndani ya mamlaka ya kizayuni, "B'Tselem," Aprili 2023, maana kabla ya uadui wa kizayuni kwa miezi michache ilisisitiza kwamba mzingiro uliowekwa kwa zaidi ya miaka 15 dhidi ya Ukanda wa Gaza ulisababisha uhaba wa dawa na vifaa vya matibabu, kwa hivyo, miundombinu ya matibabu huko iko chini ya shinikizo ya kukidhi mahitaji ya wakaazi wa Ukanda wa Gaza hata kabla ya uadui.

Tukienda kwenye sababu ya pili isiyo ya moja kwa moja, basi katika kipindi cha kati ya 1999 na 2005, uhaba mkubwa wa chakula na maji safi nchini Sudan kusini kutokana na vita ulichangia kurekodi uwiano wa vifo visivyo vya moja kwa moja na vifo vya moja kwa moja vya takriban tisa kwa mkabala wa mmoja.

Na katika Gaza sasa hivi, vikosi vya kizayuni vimeharibu mashamba na kusimamisha malori yaliyojazwa na vifaa vya misaada ya kibinadamu kwenye mipaka, kama ilivyozuia pesa zinazokwenda kwa UNRWA, jambo lililoongeza viwango vya uhaba wa chakula hadi kiwango kisicho na kifani, na mfano wa hivyo basi Asilimia 90 ya wakazi wa Gaza walikabiliwa na kiwango cha njaa na uhaba wa maji safi mwezi uliopita.

Ama sababu ya tatu ni "kuhama," ambayo husababisha kiwewe na madhara makubwa ya kimwili, kipande chake kinarejea kwa hali ya kisaikolojia na kingine kinarejea kwa hali ya kambi zilizojaa kwa watu waliohamishwa huku kukiwa na kuzorota kwa hali ya afya na kibinadamu zilizoongezeka kwa sababu ya mashambulizi yanayoendelea, na mfano wa hayo ni nchi ya Sierra Leone, ambayo nusu ya wakazi wake walikimbia makazi yao wakati wa vita vilivyodumu kwa miaka 11, na uwiano wa vifo visivyo vya moja kwa moja ulikadiriwa kuwa 16 kwa mkabala wa mtu mmoja.

Na katika Gaza sasa hivi, takriban watu milioni 1.9, wanaowakilisha asilimia 80 ya wakazi wote, walikimbia makazi yao na kuzingirwa katika maeneo finyu katika Ukanda wa Gaza, jambo lililosababisha kuwepo magonjwa ya kuambukiza kujitokeza miongoni mwa wakimbizi makazi yao, hasa watoto.

Pamoja na kuendelea wa uadui wa kikatili wa kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, na baada ya maelezo yaliyotajwa na "The Guardian" kutoka maelezo na mifano ilivyotokea kabla ya miaka kadhaa, basi tunatahadharisha kutoka kuongezeka kwa idadi ya mashahidi kwa sababu ya mashine ya kikatili ya kijeshi au kwa sababu ya magonjwa, njaa, na uhaba wa maji safi, ili idadi ya vifo irekodi idadi "ya kutisha" labda ni ya juu zaidi katika historia ya kisasa.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.