Kwa hakika, maelezo na ripoti kadhaa za hivi karbuni, zilithibitisha kuwa biashara na magendo ya mihadarati katika eneo la katikati mwa Afrika, kwani ripoti maalumu kutoka kwa Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa serekali za nchi za katikati kwa Afrika zilidhibiti takriban kilo 15 za mihadarati ya cocaine katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, na Umoja wa Mataifa unasema kuwa hiyo inafanywa tangu mwaka wa 2016 hadi mwaka huu wa 2024.
Jambo hilo linatia wasiwasi pande za kiusalama hasa nchi za Magharibi, kwa sababu baada ya uchunguzi mwingi ilibainika kuwa kuna uhusiano unaofungamana kati ya ongezeko la kiasi cha mihadarati na makundi ya magendo ya kigaidi hasa ISIS katika eneo hilo.
Biashara hiyo ndiyo chanzo kubwa zaidi cha pesa za ugaidi wa ISIS katika bara la Afrika, hata imekuwa njia badala ya biashara ya kuwateka nyara mateka wa Magharibi na kuomba fidia ili kuwaacha huru.
Shirika la Habari la “France-Press” ilieleza kuwa makundi ya kigaidi na mwanzoni mwake ni kundi la ISIS yana uhusiano wa kutiliwa shaka na pande zinazofanywa biashara na magendo ya mihadarati, na kuna ushirikiano mkubwa kati yao unaozingatiwa na maslahi, na ripoti zinaonyesha kuwa pande za biashara ya mihadarati zinatumia mapengo katika mipaka kavu, baharini na anga katika nchi za kati ya Afrikaili kunukuu mihadarati, na kwa upande mwingine, makundi ya kigaidi yanalinda operesheni za kuingiza mihadarati kupitia sahara.
Ripoti ya “France-Press” imeongeza kuwa makundi ya kigaidi, sawasawa yenye mafungamano na Al-Qaeda, au yale ya ISIS, na yote yanahusika katika kunukulu shehena za mihadarati kama kokeni na bangi.
Hapa, "François Patuel", Mkurugenzi wa tafiti za Afrika Magharibi na Kati katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mihadarati na halifu, anasema kuwa makundi ya kigaidi ndiyo wanapata faida kubwa kutoka shughuli za magendo ya mihadarati kwani biashara hiyo inayawezesha kununua silaha na kulipa pesa kwa wanamgambo wao.
Al-Kush ni mojawapo ya aina hatari zaidi za mihadarati ambazo makundi ya kigaidi kunukuu na kufanya biashara, kulingana na gazeti la “The Times”.
Al-Kush hiyo hutengenezwa na ina nitazines, na ina nguvu hadi mara 100 kuliko heroini na wale wanaoitumia inawezekana kufa wakiichukua kwa kiasi kikubwa “Julius Maada Bio”, Rais wa Sierra Leone, alisema katika hotuba yake ya televisheni mwezi Aprili mwaka jana kwamba nchi yake sasa inakabiliwa na tishio kubwa kutokana na mihadarati ya Al-Kush inayotengenezwa.
Al-Kush imeenea nchini Sierra Leone na majirani zake Guinea, Guinea-Bissau na Liberia.
Na nyingine huitwa "monkey tail" ambao ni mchanganyiko wa kinywaji kinachoitwa “homemade alcoholic gin” na mbegu za bangi, majani, mashina, na mizizi, na unaenea nchini Nigeria.
Na mihadarati nyingine iitwayo "Nyaobi", ambayo ni mchanganyiko wa heroin isiyo na ubora pamoja na bangi, kemikali za kusafisha, sumu ya panya na vitu vingine hatari na imeenea katika miji mingi nchini Afrika Kusini.
Kwa jumla, Kituo cha Alazhar cha kupambana na fikra potofu, kinasisitiza kuwa makundi ya kigaidi kama vile; Daesh (ISIS), Boko Haram, Al-Shabab na wengineo, hayana maadili wala msingi wowote kutoka katika dini wala ubinadamu, kwa hiyo makundi haya hayachungi usihi wala uhalali wa vyanzo vya kupata mali za kuendesha shughuli zake, ni jambo la kawaida kwa kuwa anayefanya halifu kama vile mauaji, uporaji, utekaji nyara na jinai nyinginezo hataangalii mali alizozipata zilitokana na chanzo gani.