Wanadai .. Tunasahihisha

28

  • | Tuesday, 5 July, 2016

Miongoni mwa mambo thabiti kihistoria kwamba zoezi la kuandika hadithi za Mtume (S.A.W.) lilianza alipokuwa Mtume hai ambapo hadithi kadhaa zilizo sahihi zilibainisha kuwa Mtume (S.A.W.) aliwaruhusia maswahaba wake kuandika hadithi zake, jambo ambalo haliwezekani kukanwa.
Pia hadithi ya kwanza inabainisha kwamba ukatazo wa kuandika ulikuwa unahusiana na ile karatasi ambayo ilitumiwa kuandika Qur-ani juu yake basi Mtume (S.A.W.) alihofia kuchanganyika maneno yake na Qur-ani Tukufu; akawakataza maswahaba wake wasiandike hadithi na Qur-ani katika karatasi moja.
Ilhali riwaya nyingine ya hadithi ni dalili ya kwamba hadithi zilikuwa zinaandikwa wakati huo, lakini jambo lililokuwa linahitaji ruhusa ni lile jambo la ghafula waliotaka kuliandika, lakini Mtume (S.A.W.) hakuwapa ruhusa ya kuliandika na kulinukuu kwa kusudio lake hasa, na katika tamko la "tumeomba ruhusa" alama ya kwamba waliokuwa wanaandika hadithi za Mtume walikuwa wengi sio mmoja au wawili.
Vile vile Mtume (S.A.W.) aliruhusia kuandika Sunnah kwa dalili nyingi, kati ya dalili hizo: 
Iliyopokelewa na Bukhariy na Muslim na wengineo kwamba Mtume (S.A.W.) aliporudia Makkah akatoa hotuba kisha mtu mmoja wa Yemen akaja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niandikie - yaani hadithi -, akasema Mtume (S.A.W.) mmwandikie akizungumzia maswahaba wake" Ibn Hajar alisema kwamba Abu Shaah, Al-Awzaaiy aliulizwa: nini maana ya niandikie? Mtu huyu alikuwa anakusudia nini hasa? Akajibu: alikuwa anataka sehemu ya hotuba ya Mtume (S.A.W.) iandikwe kwake, na kwamba uagizo la Mtume la kuandika ni uagizo wazi na la moja kwa moja.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.