Wanadai .. Tunasahihisha

29

  • | Tuesday, 5 July, 2016

Hakika Omar hakuguguna katika uandishi wa Sunnah, lakini amevisifu vitabu vilivyo mikononi mwa watu,  akasema: " kilicho bora zaidi kuliko miongoni mwa vitabu hivyo kwa Mwenyezi Mungu ni vile vilivyonyooka na vyenye mafunzo mazuri zaidi.
Na Omar Ibn Al-Khattab alitaka katika habari hii kutilia mkazo zaidi Qur-ani Tukufu, basi akataka kuwaonya kutoshughulikia kitu cho chote isipokuwa Qur-fani Tukufu.
Kwa upande mwingine, habari iliyotajwa na watu hawa ni habari ambayo haifai kuwa hoja, bali waliileta bila ya kubainisha dosari yake, ilikuwa ni wajibu kusema kwamba: habari hiyo inatokana na riwaya ya Al-Qasim iliyosimuliwa na Omar, na kwamba Al-Qasim Bin Mohammed alizaliwa baada ya kifo cha Omar kwa miaka kumi na tatu, kwa hivyo Isnaad ya habari hiyo imekatika, na kukatika kwake ni dhahiri, jambo ambalo linasababisha kudhoofika kwa habari yenyewe, na kuiweka mbali na hadithi za hoja.
Hivyo ni wazi kwetu kwamba ile iliyodaiwa ya kwamba Omar (R.A.) alichoma moto yale yaliyomfikia miongoni mwa hadithi za Mtume (S.A.W.) kwa kuhofia misemo na hitilafu ni ukiukaji mkubwa wa ukweli; lakini habari ya kwamba Omar alichoma moto vitabu ni habari ambayo haifai kuwa hoja au dalili.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.