Jukumu la Vyombo vya Habari kupambana na Fikra Potofu

Imeandaliwa na Bw. Farid Mohammed

  • | Thursday, 15 August, 2024
Jukumu la Vyombo vya Habari kupambana na Fikra Potofu

      Haijakuwa siri kwa mtu yeyote umuhimu wa vyombo vya habari na hatari yake katika nyanja mbalimbali za maisha ya kisasa, iwe katika nyanja za kimalezi, kiutamaduni, kiuchumi au kiusalama.  Ambapo Tafiti nyingi zimeafikiana kwamba vyombo vya habari vimekuwa mojawapo ya vipengele maarufu vya enzi ya kisasa na njia imara ya kuunda dhamiri za watu na jamii.

usalama ulipokuwa ni hitaji la lazima kwa ajili ya kuendelea maisha ya binadamu na kipengele cha msingi kwa ukuaji na maendeleo yake, Wale wanaosimamia huduma za usalama wametambua umuhimu wa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari na kufaidika navyo ili kueneza ufahamu wa usalama na kuhudumia jamii na masuala yake mbalimbali. Sambamba na sera hiyo, vimeibuka vyombo vya habari vya usalama ambavyo ndani yake vimebeba malengo ya kueneza ujumbe wa kuelimisha kwa usalama kwa masuala mbalimbali yanayoitia wasiwasi jamii, inakuja katika mstari wa mbele  hali ya fikra kali ya kikatili kwenye vijana wa Kiarabu kwa kuisifu chuki dhidi ya jamii na usalama wake na amani yake.

Hakika ujumbe wa vyombo vya usalama unawakilika kuhakikisha usalama na amani kwa raia kupitia kuhifadhi nidhamu na maadili ya kiujumla kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuheshimu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia maisha ya umma, pia kukabiliana na wanaokiuka sheria na kanuni hizi, na kuchukua kila taratibu na kila hatua za usalama ili kuzuia uhalifu kutokea au kuugundua baada ya kutokea kwake na kuwafungulia mashtaka wahusika wake.

Vyombo vya habari vya usalama ni moja wapo ya dhana za kisasa ambazo zilionekana kwenye eneo la media kama matokeo ya maendeleo ya maisha ya kijamii katika muongo wa mwisho wa karne ya ishirini haswa, na pia kama matokeo ya maendeleo ya kushangaza ya Vyombo vya habari na hitaji la kufaidika na mawezekano wake mbalimbali kama njia bora ya kuwashawishi wanajamii, hasa vijana, chini ya kivuli cha vyombo vya habari vipya na njia za mawasiliano ya kijamii, na habari za digital na teknolojia zilizoendelea.

Vyombo vya habari vya usalama, kama )Donald Reimer( anavyofafanua, ni vyombo vya habari vinavyozingatia maslahi ya kitaifa ya kila nchi bila ya kupingana na ujumbe wa vyombo vya habari vya umma na umuhimu wake. (William Bailey) anaafikiana naye, kwani anaamini kwamba vyombo vya habari vya usalama vinahifadhi nguvu ya jukumu la serikali katika kuhakikisha usalama na utulivu dhidi ya vyombo vya habari vilivyo wazi.

Tunaona kwamba fasili hizi zinafafanua vipengele muhimu zaidi vya vyombo vya habari vya usalama, ambavyo ni kwamba ni aina ya vyombo vya habari maalum vinavyozingatia uaminifu na umaudhui katika kuwafahamisha raia habari, kweli na sheria zinazoathiri usalama na utulivu wa jamii,  Pia ni vyombo vya habari vinavyoenda sambamba na sera ya serikali na havipingani nayo, bali vinafanya kazi ili kusaidia maslahi ya taifa, Kuhifadhi usalama na utulivu wa jamii na kusimama mbele ya vyombo vya habari vilivyo wazi, ambavyo wakati mwingine vinajaribu kukomesha jukumu la serikali na kutishia jamii kupitia yale ambayo vinatangazwa  na vyombo vya habari ambayo yanahimiza upotovu, uhalifu na fikra kali.

Kuhusu suala hili, tunakuta baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa vyombo vya habari kwa njia zake mbalimbali hasa vya kisasa vinazingatia moja ya vyanzo muhimu zaidi vya kujua(ujuzi wa) mifumo ya tabia na muamko(ufahami) wa kijamii, na zaidi ya 90% ya watazamaji(wafuatiliaji) wa vyombo vya habari hasa vijana wanaiweka katika cheo cha kwanza kama chanzo cha utamaduni wa vurugu na misimamo mikali na tabia ya kiuhalifu inayopambana na jamii.

Utafiti wa kisayansi unaohusiana na jukumu la vyombo vya habari katika kuunda muamko(ufahami) wa kijamii baina ya vijana ulionyesha kuwa 59.82% daima wanatazama vyombo vya habari na 50.2% wanatazama vyombo vya habari kutoka saa moja hadi masaa matatu, pia Masuala ya kuvuta dawa za kulevya, matatizo ya ujana, vurugu, na misimamo mikali ya kidini yanakuja katika mstari wa mbele wa masuala ambayo vijana hupokea kutoka vyombo vya habari. Kuanzia hapa, linadhihirikia jukumu la vyombo vya habari, kupitia njia zake mbalimbali, katika kushawishi maoni ya umma na mitazamo na tabia za watu binafsi, hasa wadogo na vijana. Hakika Baadhi ya yale yanayotazamwa, kuchapishwa au kutangazwa yana athari mbaya kwa malezi ya vijana na kwa usalama na amani wa jamii, hivyo inafaa kujulisha vyombo vinavyohusika na uangalizi kuhusu hatari za mienendo hii, na kushirikiana nao ili kuwasilisha taswira inayochangia kuijenga jamii katika hali nzuri.

Kutokana na hayo linakuja jukumu la vyombo vya habari vya kiusalama ili kutekeleza jukumu muhimu katika maisha ya jamii na kuelimisha maoni ya umma kuhusu hatari zinazoizunguka zinazohusiana na usalama na maisha yake. Ili kuweza kutekeleza jukumu hili, lazima ijikite kwenye mkakati wenye malengo wazi ambayo yanachangia kikamilifu katika kuhakikisha baadhi ya nyadhifa yanayohusiana na mtu binafsi na jamii kupitia kukabiliana na ukengeufu na itikadi kali, na kujikinga nayo, au kutibu  athari zao zilizotokea nazo.

Malengo haya ni:

  1. Kufatilia matukio ya kiuhalifu na harakati za kigaidi katika ngazi za kitaifa na kimataifa, na kuchambua athari zao, na kufuatilia shughuli zake za vyombo vya habari, na kufichua mbinu zake za kufanya kazi, na kuwachochea wanajamii kuripoti habari zinazoweza kusaidia vyombo vya usalama katika kugundua seli za kigaidi na makundi yenye msimamo mkali yanayolala.
  2. Uendelejia mkakati madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na mawazo yenye msimamo mkali kwa kuamsha majukumu ya taasisi za kiraia kama vile shule, familia, vyombo vya habari, vyama vya manufaa ya umma na vilabu vya michezo.
  3. Kutekeleza kampeni endelevu za kiuelimishaji na za kujikinga kwa familia, watoto na vijana ili wasiwe mwathirika wa makundi yenye itikadi kali ambayo yanafanya kazi ya kuvutia na kuwaingiza vijana katika seli zao za kigaidi.
  4. Kuzifahamisha sheria zinazohusiana na halifu za kigaidi na itikadi kali ya kidini, kisiasa na kijamii ili watu wote wafahamu sheria hizi ambazo hutumika kama vikwazo kwa wale wanaoingizwa kwenye makundi yenye misimamo mikali, kwani Sheria haiwalindi wapumbavu, na aliyekuwa mbali na adhabu hatakuwa na adabu.

Kutoka upande huo, tunasifu jukumu la kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na itikadi kali katika kukabiliana na ugaidi na itikadi kali kupitia mkakati wa vyombo vya habari kinachoutekeleza kama sehemu ya juhudi za serikali zinazolenga kupambana na itikadi kali ambao unategemea unyonyaji bora(utumikiaji bora) wa vyombo vya habari, hotuba ya kidini, na vyombo vya habari vya kielektroniki ili kuelimisha maoni ya umma na jamii ya kiarabu kuhusu hatari za ugaidi na itikadi kali, na Kutayarisha mada za vyombo vya habari za kisauti, za kuchapisha na za kuonekana kwa ajili ya kuelimisha vizazi na vijana na kuwalinda dhidi ya kuanguka katika mtego wa ugaidi na itikadi kali, Mbali na kuelekeza hotuba ya vyombo vya habari vya kidini sambamba na sera na mielekeo ya serikali kuelekea kupambana na ugaidi, ghasia na misimamo mikali na kujitolea kueneza utamaduni wa uvumilivu na uwastani.

Misimamo mikali: Ugonjwa ambao umeenea katika jamii kwa sababu ya kutokubali utamaduni wa mwingine au dini yake, kutofahamu dini kwa njia sahihi, ushupavu, na msimamo mkali. Yote hayo yanageuka kuwa mawazo na mazoezi ya kiadui kuelekea wengine.

Misimamo mikali ina aina, zenye umuhimu zaidi ni: ya kidini, kisiasa na kijamii. Katika aina hizi zote, watu wenye msimamo mkali hukimbilia aina zote za vurugu ili kufaradhisha imani yao wenyewe, Kuna dalili za uzushi wa msimamo mkali, zenye muhimu zaidi ni:

Kuwatuhumu wengine kwa ukafiri na upotofu, na kuzikafirisha serikali na walinda usalama, na kuchochea dhidi ya makundi na vikundi yanayotofautiana nanyi katika dini na madhehebu. Hakika Sababu zinazowasukuma wanajamii, hasa vijana, kuwa na msimamo mkali, vurugu na kulipiza kisasi dhidi ya jamii zinarudi kwa kundi la vitendakazi na sababu, muhimu zaidi kati ya hizo ni: Kutojua dini ya Kiislamu, utupu wa kifikra, kutokuwepo na mamlaka za kidini zinazotegemewa, udhaifu wa utambulisho wa kitaifa na upendo wa nchi, na ukosefu wa kanuni na sheria kali za kupambana na misimamo mikali. Yenye umuhimu zaidi ya yote hayo ni jukumu hasi la vyombo vya habari katika kukabiliana na tabia hizi zisizo za kijamii zinazoathiri muundo wake.

Suluhisho zilizopendekezwa za kukabiliana na misimamo mikali ni kama zifuatazo:

  1. Serikali ipitishe mkakati wa vyombo vya habari unaozingatia kuandaa kampeni za vyombo vya habari na za uelemishaji ili kueneza utamaduni wa kuvumiliana na kuishi pamoja na wengine, pamoja na kuangaliza hotuba ya kidini katika vyombo vya habari, kuangaliza tovuti za mitandao ya kijamii, na kurejelea vitabu vya kimasomo na marejeleo yanayopatikana katika maktaba.
  2. Dharura ya wazazi kuwatahadharisha na kuwaelimisha watoto wao na kuangaliza mienendo na mahusiano yao na watu wengine, hasa marafiki kwa kuhofia wachanganyike, wajulikane na wasiliane na wale wenye itikadi kali kupitia vyombo vya habari mbalimbali na mitandao ya kijamii ambayo imekuwa jukwaa la kufahamiana na kuwasiliana kati ya kizazi cha kisasa cha vijana.
  3. Kuunda kamati za ushauri kutoka wasomi wenye msimamo wa wastani, wanasaikolojia na wanasosholojia ili kujadiliana na kuwashauri wafuasi wa fikira zenye msimamo mkali na kuwahoji na kuwaelimisha kuhusu hatari ya kuangukia kwenye mitego ya misimamo mikali na kupotoka kiakili kutoka kwa uwastani.
  4. Kutoa kanuni na sheria zinazoharamisha matamshi ya chuki na misimamo mikali yenye vurugu, kama vile Sheria ya Kukataa Matamshi ya Chuki katika nchi ya UAE, ambayo inajumuisha kikundi cha vifungu vinavyoharamisha matusi kwa dini, vitabu vya kimbinguni na mahali pa ibada, na kuchochea mizozo ya kimadhehebu na kikabila. Na kuadhibu mtu yeyote anayeunga mkono na kufadhili mawazo ya itikadi kali na ya kigaidi.
  5. Kuimarisha upande wa kiusalama kwa kuangaliza vipengele vinavyotia shaka ili kujua mienendo na shughuli za watuhumiwa na kufuatilia fedha zinazotoka ndani au kutoka nje ya nchi zinazofadhili makundi yenye itikadi kali.

Mwishoni: Hakika Kupambana na itikadi kali hakuhusiani nachombo maalum, bali ni jukumu la jamii nzima, haswa familia, ambayo ndio msingi wa kwanza wa kuilinda jamii dhidi ya aina zote za mponyoko, uhalifu na tabia mbaya dhidi ya kijamii. Halafu linakuja jukumu la taasisi zingine, haswa vyombo vya kiusalama, vyombo vya habari, na mashirika ya kiraia.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.