Wanawake Mashuhuri wa Kiafrika .. Mifano angavu na Majukumu nyeti (3)

“Ellen Johnson-Sirleaf ”

  • | Wednesday, 11 September, 2024
Wanawake Mashuhuri wa Kiafrika .. Mifano angavu na Majukumu nyeti (3)

Imeandaliwa na Dkt., Hossam Mostafa

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu kinaendelea kutoa sehemu ya tatu ya mfululizo wa makala zinazohusu baadhi ya mifano angavu katika tarehe ya mafanikio ya bara la Afrika ya wanawake mashuhuri ambao wako hai au walioaga dunia, lakini kumbukumbu zao zimesalia katika kina cha historia. . Miongoni mwa mifano hii angavu:

Ellen Johnson-Sirleaf

Image

Alizaliwa “Monrovia” mji mkuu wa “Liberia”, katika 29 Oktoba 1938. Ni mwanasiasa mkongwe anayejulikana kwa uadilifu na ukakamavu wake, kiasi kwamba alipewa jina la utani la “Mwanamke Chuma” au “Iron Lady”. Alifanya kama Rais wa ishirini na nne wa Liberia kutoka 2006 hadi 2018, na kuwa mwanamke wa kwanza kushika uraisi wa nchi katika bara la Afrika. Alisomea elimu za uchumi kutoka 1948 hadi 1955 katika Chuo cha Afrika Magharibi huko “Monrovia”. Mnamo 1961, alisafiri Marekani kukamilisha masomo yake ya uchumi na elimu za siasa. Kisha akapata shahada ya uzamili katika ukurugenzi mkuu kutoka Chuo Kikuu cha “Harvard” mwaka 1971. Katika mwaka huo huo, alirudi nchi yake kufanya kazi katika serikali ya “William Tolbert”, ambapo alianza kazi yake katika serikali ya Liberia kama Waziri Msaidizi wa Fedha, hadi kufikia wadhifa wa Waziri wa Fedha wakati wa utawala wa “Tolbert”, lakini hivi karibuni alikosoa uongozi wa nchi na kuuacha na kuondoka kuelekea Marekani, ambako alifanya kazi katika Benki ya Dunia kama mtaalam wa uchumi hadi alipogombea uchaguzi mwaka 2005.

"Ellen" anazingatiwa kuwa mmoja wa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, kwani aliunda hatua mashuhuri zaidi katika historia ya nchi yake “Liberia”, aliposhinda uchaguzi wa 2005 uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 14, na baada ya kumshinda, uchaguzi huo, "Ellen" alipata sifa nyingi za kimataifa kwa kazi yake ya kujenga upya “Liberia”.

Alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka wa 2011 kutokana na jitihada zake za kufikia amani nchini mwake “Liberia”, na nafasi kubwa aliyoicheza katika mapambano ya usalama wa wanawake na kukuza haki zao. Mnamo 2016, aliorodheshwa kama mwanamke themanini na tatu mwenye ushawishi mkubwa zaidi ulimwenguni na jarida la “Forbes”.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.