Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu mkutano wa Imamu Mkuu na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya

  • | Tuesday, 10 September, 2024
Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu mkutano wa Imamu Mkuu na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya

 

Imamu Mkuu wa Al-Azhar anamuuliza Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya:

Je, kuna suluhisho la uzushi huo mkubwa wa kihistoria tunaouona huko Ghaza?

Nani anaweza kusitisha uvamizi wa kikatili dhidi ya watu wa Palestina!

Je, kuna mwanga wa matumaini kwa wale wanaouza silaha nje ya nchi wasitishe msaada wao na kuamka dhamiri zao na ubinadamu wao!

Je, kuna matumaini ya kugeuka wale wanaowafariji kwa maneno miongoni mwa  wahusika wa uamuzi wa kisiasa na kuwa na jukumu la kweli na la makini katika kukomesha uvamizi dhidi ya Ghaza!

 

Mheshimiwa Imamu Mkuu prof. Ahmed Al-Tayeb, Sheikhi wa Al-Azhar Al-Sharif, Amempokea leo Jumanne katika makao mkuu wa usheikhi wa Al-Azhar, Bwana Josep Borrell Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya kwa Mambo ya kigeni na siasa ya kiusalama akifuatana na ujumbe wa ngazi ya juu uliojumuisha Bwana. Sven Koopmans Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya kwa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati na bwana Balozi Christian Berger Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya mjini Cairo.

Sheikh wa Al-Azhar amesema kuwa, maneno na misemo havina uwezo wa kueleza kile wanachoteseka wananchi wa Palestina kutokana na uvamizi, mauaji ya kinyama na mauaji (uchinja wa) ya kila siku yanayowakabili, ambayo historia ya vita na migogoro haijawahi kutokea na kifani. Akieleza kuwa kile ambacho hufanyika kwa watu wa Ghaza ni "unyama usiojulikana kwa lugha za wanadamu" na kwamba si ujasiri au tabia njema kwa mtu mwenye silaha kushambulia watu waliokimbia makazi yao na kuwaua, akisema mheshimiwa kwamba “hatujaona ukatili wa namna hiyo katika ulimwengu wa wanyama na wanyama pori, utawala huo wa kizayuni ulipita vipimo vyote vya kibinadamu na ulifanya uhalifu mbaya sana na kugeuka kuwa mnyama mkubwa wa kidamu na kuwaua watu wasio na hatia.

Sheikhi wa Al-Azhar akauliza: Je, kuna suluhisho la uzushi huo mkubwa wa kihistoria tunaouona huko Ghaza! Nani anaweza kusitisha uvamizi wa kikatili! ulimwengu wa leo umegawanyika kati ya makundi mawili; Ama mshiriki na msaidizi kwa silaha na anayehusika katika mauaji ya watu wasio na silaha, na ulimwengu mwingine unaoshiriki katika msiba huo kwa kukaa kimya au kuzungumza juu yake kwa kulaani na kukemea Je, kuna mwanga wa matumaini kwa wale wanaouza silaha nje ya nchi wasitishe msaada wao na kuamka dhamiri zao na ubinadamu wao! Je, kuna matumaini ya kugeuka wale wanaowafariji kwa maneno miongoni mwa  wahusika wa uamuzi wa kisiasa na kuwa na jukumu la kweli na la makini katika kukomesha uvamizi dhidi ya Ghaza!, na wanaweza kufanya hivyo kama wanataka!

Sheikhi wa Al-Azhar ameashiria kuwa, hali ya mambo katika eneo la Mashariki ya Kati imekuwa ngumu sana huku akionya kwamba iwapo hali hiyo mbaya haitapatiwa ufumbuzi, dunia nzima itatelezeka kuelekea kwenye hatari kubwa ambayo haiwezikani kutabiri ukubwa wa maafa yake na kusisitiza kwamba utawala  wa Kizayuni "ilitiwa katika eneo hilo ili kulifanya kuwa ukumbi wa kudumu wa vita na migogoro na kulidhoofisha kiaskari, kisiasa, na kiuchumi na kuliiba maliasili  na utajiri wake.

Kwa upande wake, bwana Josep Borrell alielezea shukrani zake kwa Sheikhi wa Al-Azhar na jukumu lake kuu katika kueneza utamaduni wa amani na kutetea haki za wanyonge, na mchango wake muhimu katika kukuza mazungumzo kati ya dini, akibainisha kuwa anashirikiana na Mtazamo wake unaohusiana na changamoto za Mashariki ya Kati na eneo hilo, na kwamba hakuna suluhisho kwa migogoro hii isipokuwa kwa kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina na kupata Wapalestina haki zao kamili, na kufanya kazi ya kubadilisha usawa wa madaraka, na taifa la Palestina kukua kihatua, akisisitiza kwamba Umoja huo unafanya juhudi kubwa kufikia usitishaji vita huko Ghaza, na tunatumai kuwa Umoja huo utaweza kuweka misingi ya amani na kufikia mapatano ya kibinadamu ambayo hupelekea kukomesha kabisa uvamizi.

Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya kwa Masuala ya Kigeni aliashiria kuwa hajawahi kuona katika maisha yake suala tata na lililosababisha kugawanyika ndani ya Umoja wa Ulaya kuliko suala la Palestina na uvamizi dhidi ya Ghaza. Ilhali tunaona misimamo ya baadhi ya dola za umoja wa ulaya kusimamisha usafirishaji wa silaha kwa jeshi linalokalia kwa mabavu, bado kuna baadhi ya nchi ndani ya umoja zinazoendelea kuiunga mkono israil kwa silaha na katika nyanja za siasa za kimataifa, akibainisha kuwa Umoja huo uliwasilisha pendekezo la kuwawekea vikwazo baadhi ya maofisa wa utawala huo kujibu siasa zao za uhasama na kauli zinazochochea chuki, na pia kupendekeza kuweka vikwazo kwa kila mtu ambaye alishiriki katika uhalifu wa mauaji ya kimbari na mauaji yanayotokea Ghaza, lakini mamlaka yetu yanafikia pendekezo tu, na lazima liwepo msimamo wa umoja wa nchi wanachama kuidhinisha adhabu hiyo, jambo ambalo halikufanikiwa, na hivyo kuthibitisha kuwa Umoja huo utaendelea kutoa shinikizo zaidi ili kukomesha uchokozi dhidi ya Ghaza.

 

Imefasiriwa na Bw. Farid Mohammed

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.