Al-Azhar Al-Shareif inalaani vikali uadui wa kigaidi wa kizayuni dhidi ya maeneo ya kusini na mashariki mwa Lebanon, jambo lililosababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa mamia ya Walebanon wakiwemo wanawake na watoto na kuwahamisha maelfu wengine kutoka makazi yao, hayo yanatokea wakati ulimwengu unakaa kimya.
Al-Azhar inasisitiza kuwa, mashambulizi ya kizayuni dhidi ya Lebanon si ila dalili ya nia yake ya kijinai, na juhudi zake zinazoendelea za kugeuza eneo la Mashariki ya kati kuwa uwanja wa vita, na kupanua eneo la migogoro, ili kujumuisha nchi na maeneo mengine, baada ya kuigeuza Gaza kuwa vilima vya magofu, na chemchem ya damu, na maelfu ya wahanga wasio na hatia, jambo linalotishia hatima ya wananchi wote.
Al-Azhar inajiuliza ikishutumu: Uko wapi ulimwengu wa kimataifa kuhusu kuzuia wazayuni magaidi wenye jeuri?! kwa nini wote wananyamaza kimya mbele ya ugaidi mbaya uliohalalisha kuwaua wanaume, wanawake na watoto bila dhamiri?! kwa nini ulimwengu haukujibu vilio vya wanawake na watoto huko Palestina na Lebanon.. Je, kuna maslahi pamoja na mamlaka ya kigaidi ya kizayuni?! Au dhamiri ya ulimwengu imekufa?!
Al-Azhar inaitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ya haraka ili kukomesha uadui huo wa kizayuni, na kukomesha umwagaji damu wa raia wasio na hatia huko Gaza na Lebanon, ikielezea mshikamano wake kamili na wananchi wa Lebanon, na rambirambi zake kwa familia za wahanga, na kukataa kwake kabisa kwa ukiukaji kwa utawala wa Lebanon.
Imefasiriwa na Bw. Said El-Sayed Moshtohry