Uadui wa Kizayuni dhidi ya Gaza na Kuporomoka kwa Maadili ya Kibinadamu

Imeandaliwa na Bw., Eslam Ragab Mohammed

  • | Thursday, 10 October, 2024
Uadui wa Kizayuni dhidi ya Gaza na  Kuporomoka kwa Maadili ya Kibinadamu

 

Ingawa uharibifu na mauaji yanayoendelea katika ukandas wa Gaza, bado wapo wanaoona kile kinachofanywa na mamlaka ya kizayuni ni kujilinda tu, na tangu kuanza kwa uadui unaoendelea huko Gaza, pengo kati ya mabara na maeneo ya kijiografia limeongezeka, na mvutano na migawanyiko iliyotukia ndani ya nchi nyingi imeongezeka kwa njia isiyo ya kawaida, jambo linalomaanisha kwamba, kwa bahati mbaya, tunaishi katika ulimwengu unaoshuhudia kurudi nyuma kwa maadili ya ulimwengu na kanuni za kisheria zinazoshirikiwa pamoja na ubinadamu.

Kwa utangulizi huu, tovuti ya Sehemu ya Vyombo vya Habari ilifungua makala kutoka kwa blogu ya mwanasiasa wa Vita hivyo vya Gaza vinazingatiwa vita vikali zaidi ambavyo vilirekodiwa na kutangazwa moja kwa moja, ikijumuisha zaidi ya Wapalestina 30,000 waliouawa kwa mikono ya jeshi la Israeli, 60% miongoni ma  waliouawa walikuwa watoto na wanawake, pamoja na kuwepo kuhamishwa, mateso, njaa, uharibifu, kukatwa maji, mafuta na umeme, hali ya kiafya isiyo ya kibinadamu, na hali mbaya ya wagonjwa, waliojeruhiwa na waliokatwa viungo vya mwili ambao wanatibiwa kwa njia za awali na kufanyiwa upasuaji bila ganzi.

Ingawa nambari, hadithi, video na ushuhuda huu huchapishwa mara kwa mara na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, taasisi za kibinadamu na taasisi za haki za binadamu, waandishi wa habari na wapiga picha wajasiri wa Palestina, serikali nyingi na vituo vya televisheni katika nchi za Magharibi zimetoa uamuzi kwamba janga hili limetokea kwa sababu ya uharibifu wa vita na mashambulizi mabaya yaliyoanzishwa na kundi la kupigania uhuru la Kiislamu (Hamas), na Israel injilinda tu.

Ukimya wa vyuo vikuu na taasisi za kikazi

Inawezekana katika mazingira haya kuwa makundi ya maoni ya watu wa Magharibi wanaelewa mazungumzo haya ambayo yanalaani uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na ukatili uliofanywa na Israel huko Gaza.

Haishangazi kwamba kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu tuhuma za mauaji ya kimpari bado haieleweki kwa watu wengi wa nchi za Magharibi, Kwa sababu ya uwongo wa vyombo vya habari vya Magharibi na upotoshaji wa ukweli.

Lakini kinachoshangaza ni kuona vikundi vyenye uwezo wa kupambanua kutoka wale wanaohusika na vyuo vikuu, taasisi za utafiti, hospitali na vyama vya waandishi wa habari wakizama katika aina fulani ya usingizi na kukataa uwajibikaji wao wa kimaadili na kiraia dhidi ya janga hilo huko Gaza na wanakaa kimya au wanajadili kwa kiasi kidogo kwa njia yasiyo rasmi mauaji yanayowalenga Wapalestina.

Tunawezaje kuufundisha ubinadamu sheria za kimataifa, maadili na tabia bila ya tuwe na msimamo wa kisheria au wa kimaadili kuhusu mauaji ya kila siku dhidi ya wenzetu?

Kinachoshangaza zaidi pia ni ukimya wa vyuo vikuu vingi na taasisi kuu za kitamaduni katika kukabiliana na uhalifu unaowalenga wanachuoni, watafiti, matabibu na waandishi, pamoja na uharibifu ambao katika wakati wingi huonyeshwa na husherehekewa kupitia askari wenyewe.

 Kwa njia gani tunaweza kuelewa msimamo hasi na kimya kwa hoja ya kutokuwamo wa kisayansi kwa baadhi ya vituo vya utafiti vya Ulaya na Amerika vinavyohusika katika Mashariki ya Kati au uhusiano wa kimataifa katika wakati ambapo taasisi za utafiti za Palestina zinaangamizwa.

Hakika kinachotokea wakati hivi sasa sio tu ukimya na ukosefu wa kutoridhika, bali kwamba vyuo vikuu, shule na vilabu vya michezo katika visa kadhaa vimetoa shinikizo na vimetishia kwa kuchukua hatua kali dhidi ya mpango wowote wa kuunga mkono Wapalestina. Pia maonyesho ya vitabu na matukio ya kisanii na michezo yameshuhudia kupigwa marufuku kwa programu na wageni kwa sababu ya misimamo yao mikali dhidi ya uhalifu wa Israel.

Gaza na mustakabali wa demokrasia

Yote haya yanaonyesha kwamba tunaishi katika ulimwengu ambao unashuhudia kurudi nyuma wazi kwa maadili ya ulimwengu na kanuni za kisheria zinazoshirikiana baina ya ubinadamu, na kwamba demokrasia ya Magharibi ambayo inapitia machafuko leo na ambayo baadhi ya jamii zake zinaathiriwa kwa siasa za kibaguzi imeanza kupoteza uaminifu na ukweli wake.

Mwishoni, msimamo wa aibu ya watu wengi wa serikali za demokrasia hizi za Magharibi kuhusu uharibifu wa Gaza na watu wake utabaki kama ni jeraha wazi ambalo litakuwa gumu kupona kwa mamia ya mamilioni ya raia wa ulimwengu huu, na kwa hivyo harakati mpya, mitandao na ushirikiano wa kisiasa lazima yanakuwa pamoja ili kuwasilisha hotuba mpya wa kimataifa na kupambana na jambo la kutowaadhibu wenye nguvu na kufanya ubaguzi dhidi ya wahanga wa vita na mauaji kulingana na uhusiano wao na maeneo ambayo wanaishi ndani yake.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.