Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu kinaendelea kutoa sehemu ya nne ya mfululizo wa makala zinazohusu baadhi ya mifano angavu katika tarehe ya mafanikio ya bara la Afrika ya wanawake mashuhuri ambao wako hai au walioaga dunia, lakini kumbukumbu zao zimesalia katika kina cha historia. . Miongoni mwa mifano hii angavu:
Wangari Maathai
Mwanaharakati wa Kenya ambaye miongoni mwa wanaohimiza kulinda mazingira. Alizaliwa "Nyeri" huko Kenya. Alipata digrii yake ya bachelor kutoka "Mount Saint Scholastica", na digrii ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha "Pittsburgh". Alikuwa mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki na Kati kupata shahada ya udaktari, ambayo alipata kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka wa 1971, na katika chuo kikuu hicho hicho alifundisha elimu ya maradhi ya wanyama. Mnamo 1977 alianzisha harakati ya eneo la mashamba, ambayo ilipanda miti zaidi ya milioni 30 barani Afrika, ambapo alikuwa mpiganaji maarufu katika uwanja wa mazingira, na alikuwa anawahimiza watu kupanda miti ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira, hata alijulikana kwa kutetea haki za binadam. Kati ya 1981 na 1987 aliongoza Baraza la Kitaifa la Wanawake nchini Kenya. Katika wakati wa 80 wa karne ya 20, aligombea urais katika uchaguzi wa urais dhidi ya Rais wa Kenya "Daniel Arap Moi". Alichaguliwa kushikilia nafasi ya serikali katika uchaguzi wa 2002, ambao ulisukuma chama tawala cha KANU chini cha uongozo wa Moi kuingia upinzani. Alishika nafasi ya Naibu Waziri wa Mazingira na Maliasili nchini mwake. Mnamo 2009 aliteuliwa kuwa Balozi wa Amani wa Umoja wa Mataifa.
“Mathai” alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2004 kwa sababu ya mchango wake katika kuimarisha demokrasia, amani na maendeleo, Hivyo, akawa mwanamke wa kwanza wa Kiafrika kupata Tuzo ya Amani ya Nobel. Katika mwaka huo huo wa 2004, alipata Tuzo ya “Sophie” iliyotolewa na mwandishi wa Norway “Jostein Gaarder” yenye thamani ifikiayo elfu100 za dolari ya Marekani.