Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu mkutano wa Imamu Mkuu na Mwenyekiti wa Mtandao wa Suluhisho la Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa

Imrfasiriwa na Bw., Said El-Sayed Moshtohry

  • | Sunday, 13 October, 2024
Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu mkutano wa Imamu Mkuu na Mwenyekiti wa Mtandao wa Suluhisho la Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa

     Imamu Mkuu alisema kuwa mojawapo ya changamoto kubwa za kisasa katika ulimwengu ni jinsi ya kupitisha sauti za wanazuoni wa dini, wanafalsafa, na wenye hekima kwa watungaji maamuzi ulimwenguni wanaoharibu ubinadamu, wakiongoza dunia kuelekea mauaji, vurugu, chuki, na machafuko zaidi, na wasijali uhai wa wasio na hatia -watoto, wanawake, na wanaume, akitangaza: "Nashangaa kuhusu kwamba hakuna nchi au nguvu inayoweza kusimama dhidi ya mipango ovu ya kizayuni inayolenga kuwaua Wapalestina, kupanua migogoro, na kugeuza eneo, bali ulimwengu mzima, kuwa kitovu cha vita na migogoro".
Sheikh wa Al-Azhar alikemea, wakati wa kumpokea Profesa Jifry Sax, profesa wa chuo kikuu cha Columbia na mwenyekiti wa mtandao wa suluhisho la maendeleo endelevu wa Umoja wa Mataifa, hitilafu kati ya vyama vya Democratic na Republican nchini Marekani katika kila kitu isipokuwa katika jambo moja, ambalo ni uungaji mkono usio na mpaka kwa mamlaka ya kizayuni, na hayo ni kwa sababu ya kuwepo maslahi ya siri ya Marekani na Israel, akiongeza, "Nasikia kuwa mamlaka ya kizayuni imetoa juhudi kubwa hasa wakati wa kuwepo rais wa Marekani anayetii Israel, ikiiruhusu kufanya inachotaka bila vikwazo vya kibinadamu au vizuizi vya kimaadili".
Kwa upande wake, Profesa Sax alisisitiza kuwa ni lazima sauti za haki na hekima za wanafalsafa, wanazuoni wa dini, taasisi za kiarabu, na mashirika ya Kiislamu zishirikiane na kusimama pamoja dhidi ya Marekani, na kuitakia kusimamisha usafirishaji wa silaha zake kwa Israel, na kuacha kutumia kura ya (veto) dhidi ya kusimamisha uadui dhidi ya Gaza, na kuweka kikomo kwa uungaji mkono usio na mpaka wa Marekani kwa Israel, akiashiria kuwa msimamo wa Marekani hauwakilishi waamareka, bali unapingana nao kwa ujumla, kwani waamerika wana maoni sahihi na wanataka kusimamisha uadui, lakini tatizo liko kwa viongozi wa kisiasa.
Profesa Sax alisisitiza kuwa fikra kali ya kidini imefikia kiwango cha juu zaidi huko Israel, kwa kuweka utukufu juu ya uadui na kutakia kwa ulazima wa kuendelea kwake kupitia aya za kidini zinazohimiza uvamizi, uharibifu, na kuwaua wasio na hatia, wanawake, watoto na wanaume, akisisitiza kuwa uongozi wa kisiasa wa kizayuni hatutaki amani, na haifikiri suluhisho yoyote ya amani, na haiheshimu maamuzi ya kimataifa yanayoashiria haki za Wapalestina za kuanzisha nchi yao huru, na walowezi wa Israel hawaamini chochote isipokuwa kile wanachopewa na vyombo vya habari vya kizayuni, ambavyo vinaonyesha kwamba viongozi wa kizayuni wanafanya haki na ukweli, akitangaza:  "Tatizo haliko kwa Israel, Israel haiwezi kuendeleza uvamizi hata siku moja bila msaada wa Marekani, na ikitaka Marekani kuisimamisha itaweza, lakini hatuna “rais wa Marekani ambaye anataka kusimamisha mamlaka hiyo, kama ilivyokuwa hapo zamani."
Profesa Sax alipendekeza kufanyika mkutano utakaojumuisha wanafalsafa na viongozi wa dini na wawakilishi wa Al-Azhar, ili kutafuta suluhisho ya amani inayoweza kutekelezwa kuhusu jinsi ya kusimamisha migogoro katika mashariki ya kati, na kutoa taarifa ya pamoja itakayofuatwa na mkutano wa kilele wa kimataifa kwa ajili ya kuunda maono ya kimataifa katika suala hilo, kwa upande wake sheikh wa Al-Azhar alikaribisha pendekezo hilo akisisitiza kuwa Al-Azhar iko tayari kutoa aina yote ya msaada ili kuhakikisha hilo kutoa katika sura bora zaidi. 
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.