Daesh litategemea nini katika siku zijazo?

Imeandaliwa na Kitengo cha Lugha ya Kituruki

  • | Tuesday, 22 October, 2024
Daesh litategemea nini katika siku zijazo?

Imefasiriwa na Bw., Farid Mohammed Farid

 

Kundi la kigaidi la Daesh limezoea kukubali hasara na mgawanyiko wa kishirika linalopata mara kwa mara kutokana na kampeni za usalama, kuwalenga viongozi wake, na hasara kubwa inayopatikana,  Kwa hivyo imekuwa muhimu kuelewa misingi ambayo Kundi hilo linaitegemea, na kulifanya likishikamana  pamoja wakati wa dhoruba yoyote ambayo inaweza kulikumba.

Ingawa mawazo makali ya itikadi yanashabihiana kati ya makundi yote ya kigaidi, lakini fomula ya wazo hilo na njia zake za kufanya kazi hutofautiana kutoka shirika moja hadi jingine, jambo hili lilionekana wazi katika Daesh haswa; Kundi hilo limejikita katika misingi kadhaa ya misimamo mikali, Ambayo nayo ilichangia kuchora sura ya madai ya ukhalifa, Ilibadilisha Daesh kutoka kundi lenye silaha hadi kundi linalofuata mikakati iliyoteuliwa kulingana na mipango ambayo inaendelea kulingana na hali inayopitia, Mbali na mazingira mazuri ya watu yanayotolewa kwake na vyombo vya habari na injini za propaganda ambazo zinatumia matukio moto kama vile vita vya Ghaza, pamoja na maeneo yenye migogoro ya kidini.

Hakika anayeangalia kwa makini historia ya Daesh atathibitika kwamba hasara zinazofuatana kwa viwango viwili vya kibinadamu na kimada zinazokumba hazimaanishi kwamba mwisho wake unakaribia; Kwa sababu nguvu za kundi hilo hazijikiti katika viongozi wake au uwezo wake wa nyenzo tu, bali nguvu ya Daesh inategemea vitendakazi vingine vya kimuundo kama vile kuwavuta wapiganaji wengine kujiunga na kundi hilo, mbinu bunulizi za kuchocheza na kupanga upya muundo wa kundi lenyewe .

Swali ambalo linaulizwa sasa: Je, kundi hilo litaendelea tena na azma yake ya kuunda ukhalifa wa hakika (kulingana na hotuba yake), au litaendelea na madai yake ya ukhalifa unaodaiwa? Je, kundi hilo litaendelea tena na azma yake ya kuzitawala pande zengine zisizikuwa linatawala, ama litaunda kitovu kinacholiwezesha kutekeleza opereshani za kigaid? Je, ni vigezo gani au vipengele gani muhimu zaidi vinavyoathiri kukua jukumu la kundi au kinyume chake?

Tunajibu maswali yaliyotangulia kupitia mfululizo wa makala ambao tumechagua kichwa chake:“ Jambo ambalo Daesh linalitegemea katika siku zijazo“ ; ambapo haiwezekani kutoa picha wazi ya hali ya sasa ya kundi hilo mbali na kuchambua vipengele vyote ambavyo Daesh linajikita, na kupitia kuunganisha vipengele hivyo na malengo ambayo kundi linatafuta basi  vitendakazi vingi vitakuwa wazi kwetu ambavyo vitawezesha kuelewa mikakati ya kundi na mipango yake ya baadaye. Kipindi cha kwanza cha mfululizo huo kimejitolea kwa Wilaya ya mbaliya kundi.

Asili ya kihistoria

Zaidi ya miaka kumi iliyopita, Daesh lilivunja mipaka kati ya Iraq na Syria, na lilidhibiti maeneo ya pande zote mbili, na kuchukua kama makao makuu ya ukhalifa  uliodaiwa. Ukhalifa huo ulijumuisha kile kilichodaiwa kuitwa : “wilaya“ Nje ya mipaka yake, zinazokiri uwalii  kwa kiongozi wa kundi. wilaya hizo zilizodaiwa zilijumuisha maeneo ya Afrika, Asia Mashariki, na Caucasus…ili viongozi  wa wilaya hizo wachukue majukumu ya "gavana wa wilaya" na wawe njia ya mawasiliano  kati ya uongozi wa Daesh na wanachama wake katika wilaya zao. chini ya amri yao kuna kundi la wasaidizi, ambao baadhi yao huitwa "Amiri wa vita" nao ni wahusika wa kijeshi, pamoja na utaalam mwingine kama vile Amiri wa kuajiri na Amiri wa fedha  n.k...

Nguvu na udhaifu wa mataifa hayo umetofautiana katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mazingatio yanayohusiana na maeneo ya matawi hayo na sera za serikali katika kupambana na ugaidi katika maeneo ya majimbo hayo.

Nguvu na udhaifu wa wilaya hizo zimetofautiana katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mazingatio yanayohusiana na maeneo ya matawi hayo na sera za serikali katika kupambana na ugaidi katika maeneo ya wilaya hizo, Pamoja na mikakati ya Daesh katika maeneo hayo. Kushindwa kwa Daesh kulichochea urekebishaji wa wilaya haizo na kuyapunguza kutoka wilaya 35 hadi 14, Baada ya Daesh kupoteza udhibiti wake wa mahali, lilirekebisha muundo wake ili kuendana na hali mpya, Hasa baada ya kupoteza viongozi wake wengi katika miaka ya hivi karibuni, kulingana na ripoti iliyochapishwa na "Kituo cha Sera ya Kimataifa," iliyonukuliwa na tovuti ya "Al Hurra" mnamo Julai 8, 2020. Daesh pia lilidumisha mbinu ya ugatuaji ambayo ilijulikana kwayo, ingawa wilaya ya mbali ilidumisha muundo wake wa kiutawala kwa mujibu wa sheria za shirika, ilibadilika kulingana na mkakati wake wa kazi na mawasiliano yake na uongozi mkuu kulingana na maendeleo ambayo. ilitokea kwake, kama ilivyo kwa lile linaloitwa jimbo la Khorasan, kwa mfano.

jiografia ya wilaya za Daesh

Daesh sasa inachangamka nchini Syria na vikundi vilivyoenea katika eneo la jangwa, na huko Iraq inachukua fomu ya vikosi vyenye idadi ndogo na vikali katika wakati huo huo, kama wataalam wanasema. Nje ya nchi hizo mbili, kundi hilo lina uwepo nchini Afghanistan na Pakistan chini ya jina la " Daesh -Khorasan". Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa mwaka 2021, basi wilaya hiyo inayodaiwa ina wapiganaji wapatao 2,200 waliowekwa katika miji ya Kunar na Nangarhar. Mnamo mwaka wa 2015, kundi hilo lilitangaza wilaya inayoitwa "Caucasus" , ambayo ilihusika na shambulio la hivi karibuni la "Dagestan" mnamo Juni 2024.

Daesh lina uwepo barani Afrika. wilaya za "Afrika Magharibi" na "Afrika ya Kati" ni kati ya matawi yanayofanya kazi zaidi ya kundi la Daesh katika miezi ya hivi karibuni; ambapo zilifanya oparesheni kubwa kiasi na kuteka baadhi ya ardhi na miji katika baadhi ya nchi, ingawa kwa muda maalumu, pamoja na kupata vyanzo zaidi vya ufadhili. Mnamo 2022, Daesh lilitangaza kile kinachoitwa "Msumbiji"; Hizi zote ni zana za kihabari ambazo Daesh hutumia kujitangaza.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.