Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar chasifu maelezo mazuri ya Pop Francis kuhusu kutofungamanisha Uislamu na vurugu

  • | Wednesday, 3 August, 2016
Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar chasifu maelezo mazuri ya Pop Francis kuhusu kutofungamanisha Uislamu na vurugu

Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kwa lugha za kigeni kimeyasifu maelezo ya Pop Francis, Baba wa Vatican, aliyoyatoa kwa waandishi wa habari kuhusu Uislamu na tuhuma zinazochochewa juu yake, ambapo alitoa maelezo haya alipokuwa ndani ya ndege akirudi kutoka Polanda, ambapo alisisitiza kuwa kufungamanisha Uislamu na tuhuma ya kuchocheza vurugu ni jambo lisilokubalika kabisa, ambapo sio la uadilifu kuunga Uislamu na vurugu kwani ni ujumlisho unaokataliwa, na kwamba wapo watu wenye misimamo mikali katika dini zote hata katika Ukristo yenyewe.
Pia, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kwa lugha za kigeni kinazingatia maelezo hayo yanadhihirisha ufahamu wa yule Pop kwa ukweli wa Uislamu na mafunzo yake mema, na kwamba ametambua vyema kwa ukweli wa mambo na matukio yanayojiri duniani, vile vile Kituo kinazingatia kutolewa kwa maelezo hayo mazuri mara moja baada ya mkutano uliofanyika baina ya Imamu Mkuu wa Al-Azhar na Pop Francis hapo mwezi wa mei uliopita ni jambo linalothibitisha umuhimu wa mazungumzo wa kudumu baina ya pande mbili ambazo ndizo jumuiya kubwa zaidi za kidini duniani kwa ajili ya kutekeleza maslahi za wanadamu wote.
Pop Francis alikuwa ametoa maelezo yake hayo akiashiria ule mkutano uliofanyika baina yake na Mheshimiwa Imamu Mkuu, akisema kuwa alikutana na Imamu Mkuu wakafanya mazungumzo marefu ambapo hujua vyema waislamu wa kweli kama vile Imamu Mkuu wanajua njia ya kuliwaza, akiongeza kuwa waislamu hawa wanatafuta tafuta amani na mazungumzo.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.