Katika vita vilivyo hatari kama vile makabiliano ya silaha, nchi ya Somalia inaendesha vita vya kielektroniki dhidi ya propaganda za kundi la kigaidi la Al-Shabaab.
Wakati ambapo kundi hilo la fikra kali linaendeleza zana zake za vyombo vya habari ili kulenga akili na kutangaza mawazo yake mtandaoni, taasisi kama vile "Teknolojia Dhidi ya Ugaidi" iko mstari wa mbele kwa ajili ya kukabiliana na tishio hili la kidijitali.
Kupitia majukwaa ya siri na maudhui inayobeba jumbe zilizofichwa, kundi la Al-Shabaab linatawalia anga ya mtandao, katika jaribio la kuunda upya matukio ya wakati wa hivi sasa na kuimarisha nguvu yake nchini Somalia na Afrika Mashariki.
Somalia inapigana vita vikali dhidi ya kundi la kigaidi la Al-Shabaab, ambayo imezidisha juu ya vita vya silaha vita vya kielektroniki dhidi ya propaganda za fikra kali na habari potofu. Shirika la Kitaifa la Ujasusi na Usalama la Somalia limezidisha juhudi zake kwa kuunda timu maalumu za kufuatilia Mtandao zinazofanya kazi ya kutahadharisha makampuni ya teknolojia ili kuondoa maudhui yenye fikra kali.
Abdul Rahman Youssef Al-Adala, Naibu wa Waziri wa Habari, aliuambia mtandao wa Sauti ya Amerika, akisema: “Tulipoanza, kazi ilikuwa ngumu na ilihitaji maarifa na ujuzi mkubwa, tulitoa mafunzo kwa timu zetu, tukaanzisha ofisi maalumu na tumeandaa zana muhimu zinazohitajika, na kwa sheria iliyoidhinishwa na Bunge, tulikawa katika nafasi nzuri zaidi.”
Hivi majuzi, Waziri wa Habari Daoud Awais na naibu wake walitangaza kampeni mpya ya kupambana na habari potofu na uchochezi wa ghasia.
Katika hotuba yake wakati wa kongamano mjini Mogadishu, Aweys alisema: "Kwa pamoja tunaweza kukabiliana na uovu huu unaotishia umoja wetu, tuache kuunganisha safu zetu dhidi ya habari za uongo kwa ajili ya nchi yetu na watu wetu."
Mtafiti Mohamed Gilaid, mtaalamu wa usalama wa kidijitali ambaye hapo awali alifanya kazi pamoja na Meta aliashiria kwamba Al-Shabaab inategemea sana majukwaa kama vile Telegram na WhatsApp, ambayo ni vigumu kufuatilia kwa sababu ya usimbaji fiche.
Alifafanua pia: "Al-Shabaab wanatumia vibaya majukwaa haya na wanazieneza habari za uongo, wanatia chumvi nguvu na ushawishi wake, na wanazingatia masuala kama vile utaifa na kutokuwa na uwezo wa serikali kujionyesha kama mlinzi wa uhuru wa Somalia."
Bw. Adam Hadley, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Teknolojia dhidi ya Ugaidi, alieleza kwamba Al-Shabaab ni mmoja wa waigizaji wa hali ya juu zaidi ambao taasisi yake inawakabiliana nao kwenye Mtandao.
Wakati wa mazungumzo yake na Sauti ya Amerika, alisema: "Maudhui mengi yanayohusiana na Al-Shabaab yanaonekana kama ni yamefichwa na yenye changamano, na yanachukua muda mrefu ili kuthibitisha kwamba yana taarifa potofu au habari za uwongo, Katika kisa kimoja, tuligundua tovuti nzima ya habari iliyojaa habari za kutiliwa shaka inayounga mkono Al-Shabaab na Al-Qaeda, lakini haikuwa na maudhui yoyote ya vurugu au ya aibu, kama kwamba ilikuwa inatoa huduma ya habari ya kitamaduni."
Al-Shabaab inaendesha majukwaa kadhaa ya vyombo vya habari, yakiwemo redio na vyombo vya elektroniki yanyowalenga watu wa Somalia na Kenya.
Kwa mfano, Shirika la Habari la Shahada linalodai kwamba linaeneza habari za Somalia na Afrika Mashariki, na hueneza makala yake kupitia jukwaa la Chirp Wire, ambalo halina sera za udhibiti wa maudhui.
Pia hutumia akaunti kwenye majukwaa makubwa kama vile Facebook na Iks ili kufikia hadhira wengi.
Vile vile, jukwaa la vyombo vya habari la kundi la Al-Shabaab, Al-Kata'ib, hulenga kwa kiasi kikubwa Telegram, na huendesha idhaa kadhaa kwa lugha nyingi.
Katika uchunguzi uliochapishwa mwaka wa 2023, taasisi ya Kod For Afrika ilifichua kuwepo kwa uhusiano kati ya Al-Kata'ib na Shirika la Habari la Shahada.
Ripoti iliyotangazwa kwenye tovuti ya Al-Bawaba
Imefasiriwa na Bw., Eslam Ragab Mohammed