Suala la ugaidi na kuenea kwa misimamo mikali likawa tatizo kubwa zaidi katika jamii yetu ya kisasa, linaloathiria vibaya maendeleo na utulivu wa mataifa na jamii mbalimbali duniani. Kwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili inabidi kutambua kuwa taasisi za kijamii kwa aina zake tofauti zinatakiwa kuchangia kulitatua tatizo hilo, taasisi za kimafundisho na za kutoa malezi zina nafasi kubwa mno zikilinganishwa na taasisi nyinginezo, ambapo taasisi hizo zina uwezekano wa kubadilisha mwelekeo wa jamii na kurekebisha makosa ya kifikra yanayojitokeza na kupelekea hali hii. Umuhimu wa malezi uko wazi kuzuia sababu za kuenea kwa fikra kali baina ya vijana.
Na malezi mema huchangia kwa kiasi kikubwa kupambana na ugaidi na fikra potofu kwa njia ya kuudhibiti mwenendo wa jamii husika na kuwapa vijana na watu kwa jumla mafunzo yanayowasaidia kujikinga na fikra hizo mbaya, ambapo mafunzo wanayoyapata wanafunzi katika vipindi tofauti vya mafunzo yanaunda akili na kuchora njia watakaofuata baadaye, kwa hiyo tukisema kuwa malezi utotoni yana jukumu la kuunda binadamu na kumpa mwangaza wa kuanza kutembea katika maisha, basi mafunzo huwa dira yake katika njia ile ya kumwelekeza kwenye vichochoro vya maisha.
Pia, kwa kufikia ufumbuzi wa kudumu kwa tatizo hili, taasisi za kimafunzo na kimalezi zinatakiwa ziambatane na kushirikiana kwa ajili ya kupambana na tabia hii na kuainisha kuzichambua sababu zake kwa kutambua mambo yabayowashawishi vijana na kuwavutia kwa njia za ukatili na fikra potovu. Tukiangalia mchango wa taasisi za kimalezi na kimasomo tutagundua kuwa ziko aina na idadi kubwa za taasisi hizo, ambapo kila aina ina kiwango na malengo yake maalumu. Hata hivyo zote zinaambatana katika lengo lake kuu ambalo ni pamoja na kuwaelekeza na kuwasaidia watu kwa viwango vyao vyote.
Kuanzia shule za kimaandalizi, msingi, sekondary, vyuo na vyuo vikuu na hata vyuo vya kuwafundisha watu misingi ya kusoma na kuandika tu, pia taasisi za kwatunza watu wazima ambao hawana mwenye kuwatunza na kuwahudumia, taasisi hizo zote na zaidi zinachangia sana kuathiria mwanadamu kiakili, kiitikadi na kifikra.
Tunweza kusema kuwa mchango wa taasisi za kidini, kiutamaduni, kijamii uko wazi na haiwezekani kuukana, pamoja na mafunzo mengine kuhusiana na kuimarisha uelewa wa kupitia jumuiya na mashirika ya huduma za kijamii. Kwa kweli juhudi za taasisi hizo zinaweza kupunguza hatari na kuisaidia jamii iepukana na mabaya ya kuenea ugaidi na fikra kali.
Ama kuhusu mitalaa inatakiwa kuwa na mada na maelezo yanayokwenda sambamba na hali ilivyo katika jamii na iwe na uwezo wa kuzungumza na vijana kwa lugha yao ya kisasa na kutambua mahitaji ya vijana na namna ya kuwasaidia kifikra wawe mbali na ushawishi na ulaghai wa maadui wanaojaribu kuwavuta vijana hawa kwa kuwavuta kwenye fikra zilizo sawa na kuwatahadharisha kutoka mitego na mikakati mibaya inayotegwa na maadui wa umma na maadui wa amani na usalama wa mataifa kuwatumia vibaya.
Kwa jumla tunaweza kusema kuwa majukumu ya taasisi ya kimalezi na kimafundisho yako mengi lakini lililo muhimu zaidi kuidhibiti na kurekebisha fikra na mwenendo na fikra. Vile vile, tabia nzuri ina umuhimu wake kurekebisha fikra na kuudhibiti mwenendo na hali ya jamii kwa upana, ambapo jamii inayowajibikia tabia njema haiwezi kuwa na matatizo wala maangamizi kwani wanachama wake huwa na tabia zinazowahimiza kufanya mema na kuepukana na maovu, kwa hiyo haikubaliki kuamini kuwa jamii ya kiislamu ambayo ni jamii ya tabia njema ni jamii ya vurugu na ukatili, bali vitendo vya wachache wanaojidai kuwa ni waislamu vinasababisha kuchafuka kwa jamii nzima.
Kifupi, taasisi zote za jamii na watu wote wanaoishi katika jamii fulani wana majukumu ya kurekebisha hali na kusisitiza mazuri na kupambana na maovu kwa kutumia njia na mbinu mwafaka kwa mujibu wa shida na sababu zake kwa kuwa kulitatua tatizo lolote inawajibisha kutambua mizizi yake na namna ya kulitatua kabisa na kupambana nalo kwa njia iliyo sahihi.
Kwa hakika malezi ambayo mtoto anapewa utotoni na mafunzo ambayo mwanadamu anapata kupitia maisha yake huathiri sana katika mwelekeo wake wa kifikra na kuainisha mambo ambayo anayapenda na yale ambayo anayachukia kwa hiyo tuzingatie malezi na mafunzo tunayowapa watoto wetu kwa ajili ya kuwaelekeza kwenye njia sahihi na kuwaepukusha na mabaya duniani na Akhera.