Sheikh wa Al_Azhar akutana na Rais wa Azerbaijan alipowasili kwa mji mkuu Baku ili kushiriki katika COP29

  • | Tuesday, 12 November, 2024
Sheikh wa Al_Azhar akutana na Rais wa Azerbaijan alipowasili kwa mji mkuu Baku ili kushiriki katika COP29

     Sheikh wa Al-Azhar, Profesa Ahmed Al-Tayyeb, alikutana na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev mwanzoni mwa ziara yake katika mji mkuu, Baku ili kushiriki katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi (COP29).

Sheikh wa Al-Azhar alielezea shukrani zake kwa Azerbaijan na kwa uongozi wa mkutano huo kwa maandalizi bora kuhusu mkataba wa umoja wa mataifa, na mkutano wa kilele wa viongozi wa dini kwa ajili ya tabianchi.

Sheikh Al-Tayyeb alionyesha kwamba ziara yake imekuja sambamba na tangazo la mji wa Shusha kuwa Mji Mkuu wa Utamaduni wa kiislamu kwa mwaka 2024, akisisitiza umuhimu wa kutoa juhudi ya kurudisha nafasi kwa ulimwengu wetu wa kiislamu katika mfumo mpya wa kimataifa, na kutumia urithi wa kiislamu kwa ajili ya kufikia maendeleo makubwa katika nyanja zote, na mwanzoni mwake ni kutoa juhudi ya kujumuisha umma wa kiislamu.

Akiashiria kuwa Al-Azhar inatoa juhudi kubwa ili kuhakikisha umoja wa kiislamu unaotarajiwa kupitia kuandaa mkutano nchini Bahrain, ili kuimarisha mazungumzo kati ya madhehebu tofauti ya kiislamu, hasa Sunna na Shia, kwa lengo la kutoka na sauti moja ya kiislamu inayoweza kuelezea msimamo wa wanazuoni wa kiislamu kuhusu changamoto mbalimbali za kisasa zinazoikabili umma.

Kwa upande wake, Rais wa Azerbaijan alieleza shukrani zake kwa Sheikh wa Al-Azhar kwa kukubali mwaliko wake, na kuthamini juhudi zake katika kueneza maadili ya amani  ulimwenguni, undugu, na uvumilivu, alisema kwamba bado anakumbuka ziara yake katika Al-Azhar mwaka huu, akisisitiza kuwa ziara ya Sheikh wa Al-Azhar nchini Azerbaijan inachangia kuimarisha uhusiano kati ya pande zote mbili, hasa katika nyanja ya mazungumzo kati ya dini, na kuthamini juhudi za Al-Azhar katika kuhakikisha umoja wa kiislamu, aliongeza kuwa Azerbaijan inatoa juhudi za kuinua kiwango cha ukaribu kati ya nchi za kiislamu, kwani ulimwengu wa kiislamu hautaweza kusonga mbele na kustawi ila kupitia mshikamano na uratibu kamili kati ya sehemu zake mbalimbali.

Rais wa Azerbaijan na Sheikh wa Al-Azhar walikubaliana juu ya umuhimu wa kuendelea kuhamasisha juhudi za kimataifa ili kusimamisha uadui dhidi ya Gaza na Lebanon, na kuwezesha kuingiza misaada ya kibinadamu kwa ukanda uliozingirwa, wakitangaza kuataa vikali uvamizi wa mali za UNRWA na kuzuia kazi yake kwa Wapalestina wasio na hatia, jambo lililozidisha janga la kibinadamu katika kambi, na kuwauwa shahidi zaidi ya wapalestina 40,000, wengi wao ni wanawake na watoto, na kuwahamisha wapalestina milioni mbili.

 

Imefasiriwa na Bw. Said Moshtohry

 

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.