Sheikh_Al-Azhar ampokea Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kolombia na waomba kwa msimamo mkali wa kuzuia kuzitengeneza silaha

  • | Sunday, 24 November, 2024
Sheikh_Al-Azhar ampokea Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kolombia na waomba kwa msimamo mkali wa kuzuia kuzitengeneza silaha

 

Sheikh wa Al-Azhar anatoa shukrani zake kwa msimamo wa Rais wa Kolombia katika tamko lake la kutekeleza agizo la kukamatwa lililotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuhusu wahalifu wa kivita wa mamlaka ya Kizayuni.

Mke wa Rais wa Kolombia atoa shukrani zake kwa juhudi za Sheikh wa Al-Azhar katika kueneza amani duniani.

Mheshimiwa Imamu Mkuu Professa. Ahmed Al-Tayeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif alimpokea leo Jumapili katika mkao mkuu wa Sheikh wa Al-Azhar Bibi Veronica Alcocer Garcia, mke wa Rais wa Jamhuri ya Kolombia.

Mheshimiwa Imamu Mkuu alimkaribisha Bibi Veronica katika Al-Azhar, akisisitiza shukrani zake kwa Jamhuri ya Kolombia, pia alimwomba afikishe salamu zake kwa Rais wa Kolombia Gustavo Petro, na shukrani zake kwa msimamo wake katika kuthibitisha umuhimu wa kuheshimu uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa kutekeleza amri ya kukamatwa iliyotolewa na mahakama hiyo kuhusu wahalifu wa kivita wa mamlaka ya Kizayuni, na maombi yake ya kuendelea ya kukomesha mauaji ya kimbari na mauaji yanayofanywa huko Gaza.

Mheshimiwa Imamu Mkuu aliashiria kwamba Al-Azhar inafanya kazi ya kueneza ujumbe wa Uislamu ambao ni kueneza amani baina ya wote, Uislamu ulifanya kujuana, kujumuika, na huruma kuwa ni msingi wa mahusiano ya kibinadamu kati ya watu bila kujali itikadi, na rangi zao, ukionyesha kwamba ikiwa Mwenyezi Mungu Akitaka Atawajaalia watu wote wafanane, lakini Alitaka kufanya tofauti kuwa ni sheria ya ulimwengu wote, na kufanya mafungamano ya udugu wa kibinadamu kuwa ndio jambo la msingi katika mahusiano baina ya waumini na baina ya waumini na makafiri, na Akaupa kwa udugu huu wajibu wake na faradhi zinazoinua thamani ya mwanadamu hata katika wakati wa vita, Akieleza kwamba vita katika Uislamu havikuanzishwa isipokuwa kuzuia uadui, na kwamba kile tunachokiona kuhusu kinachotukia katika vita vilivyojulikana kihistoria kama vita vya kidini havikuwa na msukumo wa kidini, kwani vilichochewa na itikadi za kisiasa zilizojaribu kuitumia vibaya dini, kama inavyotokea sasa huko Gaza katika suala la mauaji, maangamizi, na vitendo vya uhalifu wa kutisha chini ya kifuniko cha matini ya kidini ya kibiblia ambayo yanafasiriwa kwa njia potofu na isiyo sahihi ili kuhalalisha malengo ya kisiasa ya unyakuzi wa ardhi na unyakuzi wa haki za Wapalestina.

Mheshimiwa Imamu Mkuu alibainisha kwamba Al-Azhar imechukua hatua kubwa ili kueneza utamaduni wa amani na udugu ndani na nje ya Misri, Al-Azhar ilianzisha Nyumba ya Familia ya Misri pamoja na makanisa ya Misri ili kuimarisha uhusiano wa udugu na kuishi pamoja kati ya Wamisri., Waislamu na Wakristo, kuanzia mpango huu ilikwenda kwa taasisi za kidini na kitamaduni kote ulimwenguni, na tulifanya juhudi kubwa katika kujenga madaraja ya mawasiliano na taasisi za Magharibi, juhudi hizi zilifaulu katika kutiwa saini kwa Hati ya kihistoria ya Udugu wa Kibinadamu huko Abu Dhabi pamoja na kaka yangu mpendwa Papa Francis, ambayo ulichukua mwaka mzima kuufanyia kazi kabla ya kusainiwa kwake, Umoja wa Mataifa pia ulipitisha kumbukumbu ya kusainiwa kwake katika 4 Februari kama Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu.

Sheikh wa Al-Azhar alisisitiza kwamba sababu kuu ya mateso ya watu hivi leo ni siasa za mwili ambao umeutengwa kabisa na roho na dhamiri, na mwelekeo huu wa kimataifa unaojaribu kuitenga dini, na kuingiza siasa katika dini ili kufikia tamaa, hasa kuruhusu utengenezaji wa silaha na milipuko, ingawa ni sababu ya migogoro na vita.

Kwa upande wake Bibi Veronica alitoa shukurani zake kwa kukutana na Sheikh wa Al-Azhar, na ufuatiliaji wake wa juhudi za kuleta amani duniani, akisisitiza imani yake katika uwezo wa viongozi wa dini kuleta amani na kuieneza kwa njia ya mazungumzo, pia alionyesha kukubaliana kwake na maono ya Sheikh wa Al-Azhar kuhusu hatari ya kuzitengeneza silaha, na kwamba ndiyo ni sababu kuu katika mkasa huo unaotokea duniani, akionyesha hamu yake ya kukomesha tasnia hii ili kuondoa umaskini, migogoro, chuki na vita, pia alisisitiza kwamba ni lazima kuitazama dunia kwa maono tofauti na wanasiasa ili kubadilisha upendo badala ya chuki na kubadilisha amani badala ya vita na kuwa na wa dini, alionyesha umuhimu wa hati ya kihistoria ya udugu wa kibinadamu na hitaji la ulimwengu la mfano huu wa ushirikiano kati ya watu wa kidini.

 

 

Imefasiriwa na Bw., Eslam Ragab Mohammed

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.