Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu kinaendelea kutoa sehemu ya nne ya mfululizo wa makala zinazohusu baadhi ya mifano angavu katika tarehe ya mafanikio ya bara la Afrika ya wanawake mashuhuri ambao wako hai au walioaga dunia, lakini kumbukumbu zao zimesalia katika kina cha historia. . Miongoni mwa mifano hii angavu:
Ameenah Gurib-Fakim
Mwanasayansi wa Mauritius wa Anuwai ya Kibiolojia (Bioanuwai) anayeaminika ndani na nje ya nchi, kwa sasa anafanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Tafiti za Tiba ya Mimea (CEPHYR), pamoja na kazi yake kama mhadhiri wa kemia hai, na Makamu wa Chuo Kikuu cha Mauritius. Aliwahi kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Mauritius kabla ya Bunge la nchi hiyo kumchagua kama Rais.
“Amina Fakim” alizaliwa mnamo Oktoba 17, 1959, katika kisiwa cha Mauritius, Alifanya kazi kama mkurugenzi mkuu katika Kituo cha Kimataifa cha Utafiti na Ubunifu (CIDP), vitabu vingi na utafiti juu ya sayansi ya kibiolojia, na ameshinda tuzo nyingi za heshima ni pamoja na tuzo ya “Nobel L'Oréal" ya UNESCO barani Afrika mnamo 2007, na pia alipokea Tuzo la Umoja wa Afrika kwa Wanawake katika Sayansi mwaka 2009.
Aliapishwa kuwa mwanamke wa kwanza Mwislamu kushika cheo cha Rais wa Jamhuri ya Mauritius tangu kisiwa hicho kipate uhuru kutoka kwa ukoloni wa Uingereza mwaka 1968. Uamuzi wa kumteua ulikuja baada ya Bunge kuamua kwa kauli moja kumteua baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake, “Rajkesvoor Buriag”, na kufuatia kuteuliwa kwake na Waziri Mkuu “Anirudh Jugnauth”.
“Fakim” ameshiriki katika mikutano kadhaa ya ushauri kuhusu masuala ya mazingira yaliyoandaliwa na Benki ya Dunia, na aliwahi kuwa mwanachama mwanzilishi wa Jumuiya cha Afrika yote cha Mimea ya Dawa ya Kiafrika. Ameandika vitabu 28 katika uwanja wa uhifadhi wa viumbe hai na maendeleo endelevu, na ametoa mihadhara mingi ya kisayansi katika nchi nyingi za ulimwengu.