Bila shaka familiya ndiyo msingi wa kwanza wa jamii yoyote, ambapo mafanikio ya jamii yanatokana na kufanikiwa kwa familiya katika kujenga kizazi cha waislamu walio na maadili mema, tabia njema na fikra sahihi. Pia, ukati na kati katika Uislamu huzingatiwa msingi muhimu na nguzo imara ya dini hiyo, jambo lililotajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume aweni shahidi juu yenu} [2/143].
Familia ina majukumu makubwa kuwalea watoto na kurekebisha mwenendo wao na kuwaelekeza kwenye tabia njema na kuitakasa nafsi na roho zao. Majukumu hayo ya kuwalea watoto ni ya pamoja baina ya wazazi wawili, ambapo kila mmoja wao anawajibika mambo maalumu ya kutekelezwa minajili ya kuwalea watoto wao malezi mema, kwani wazazi ndio mfano wa kuigwa kwa watoto wao na ruwaza wao, kwa hiyo, wakiwa waumini wa kweli wanaofanya mema basi watoto wao huwa hivyo hivyo, ama wakiwa waovu basi watoto wanahofiwa kuathiriwa uovu huo. Kwa hakika baba mzazi akiwa hajali kuwapa wanawe malezi yaliyo bora wakati ambapo mama pia anashughulikia mambo mengine, basi watoto huwa katika hatari kubwa na huenda watapata matatizo mengi maishani mwao, hivyo jamii nzima huathirika vibaya, kwani jukumu la msingi la wazazi ni kuwalea watoto wao, ambapo malezi mema ni jukumu la familia kisha ni jukumu la taasisi za kielimu kama vile; msikiti, skuli, chuo kikuu na kadhalika, basi taasisi hizo zikiwa na upungufu kutimiza jukumu lake, familia watakiwa kwajaza mapengo na kurekebisha dosari zilizopo.
Inafahamika kuwa jamii ya kisasa inateseka kuenea fikra za kigaidi na misimamo mikali, zaidi ya kuongezeka wito na harakati za kuwavuta vijana kwenye upotofu na uharibifu wa kiakili, kwa bahati mbaya baadhi ya vijana hujibu wito hizo na kujiunga na makundi haya ya kigaidi wakidhani kuwa wapo sawa, na kuwa wote wasio fanana nao kifikra na kimaoni basi wahalifu ambao wanastahiki kuadhibiwa, hapa umuhimu wa famili na roli yake kuwakinga watoto wao kutokana na fikra na woto hizo inajitokeza, kwani malezi siyo kivitendo tu bali kuna malezi ya kifikra ambayo umuhimu wake haupungui malezi ya kivitendo, malezi ya kifikra hayo yanatokana na familia inayoshikamana vizuri na kupendana sana, kwa kuwa familia ni mhusika wa kwanza kuhusiana na malezi; kimwili, kiakili, kifikra, kitabia na kimwenendo, ikizingatiwa kwamba malezi ya kifikra yana umuhimu sawa sawa na makezi ya kimwili na kimwenendo na kimaumbile.
Nazo Taasisi za kielimu zina roli na majukumu makubwa sana katika malezi baada ya wazazi kuhakikisha upendo, usalama na amani ya ndani ya familia, kupitia kupanga mitalaa sahihi ya kitaaluma inayoambatana na wanavyuoni husika na inayotokana na uelewa sahihi wa matini za Qurani Takatifu na Sunnah za Mtume (S.A.W.), na kupitisha mitalaa hiyo katika viwango mbalimbali vya elimu kuanzia maandalizi na elimu ya msingi kwenda elimu ya katikati mpaka kufika Chuo Kikuu.
La kusikitisha kuwa baadhi wanafanya uhalifu na jinai za kuwahofisha, vurugu, ukatili na mauaji na kuwatishia watu kwa madai ya kuitetea dini na kuwa sheria inaagiza hivyo na kuwa watakaofuata njia hiyo watapata thawabu mwishoni, lakini hali hii haiwi ila kwa yule aliye hajui chochote kuhusu ukweli wa Uislamu au yule ambaye anachukia mafundisho ya dini hiyo takatifu. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwamba uelewa wa familia kwa ukweli wa Uislamu na mafundisho yake na mshikamano wa wanandoa ndiyo kigezo cha amani cha familia na jamii kwa jumla, kinachopambana na hali yoyote ya kuwasha fitina na kupoteza amani na utulivu.
Kwa hakika Mtume wetu (S.A.W.) ndiye mfano bora na ruwaza njema, ambapo kama alivyozingatia kuwalea maswahaba wake na kuzitakasa nafsi na roho zao, hivyo hivyo wazazi wanawajibika kuwalea watoto wao na kuzitakasa nafsi zao, kwa kuwa Mtume (S.A.W.) amevumilia jukumu zito mno lisilowezekana kutekelezwa na mtu yeyote mwingine isipokuwa yeye, jukumu hilo ni kuwaita watu kumwamini Mwenyezi Mungu na kumpwekesha pamoja na jukumu la kuwalea watu wanaoamini, maana alikuwa na jukumu la {kufikisha ujumbe kwa makafiri na malezi kwa walioshaamini}, ikizingatiwa kwamba jukumu la pili halipungui katika umuhimu wala ugumu wake kuliko la kwanza. Hivyo, Mtume (S.A.W.) amewalea maswahaba watukufu kwa mujibu wa tabia njema, maadili mema na sifa nzuri, akaondoa mabaki ya ujahili na movu yake kutoka nyoyo zao, ambayo ni kama vile; mauaji yasiyo na haki, kuwatishia na kuwahofisha wasio na hatia. Kwa hivyo, Uislamu ndiyo dini iliyotakasika alikuja nayo Mtume (S.A.W.) akifikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu (S.W.) kwa waja wake, dini hiyo inahusiana na nyanja zote za maisha, ambapo ni dini ianyokusanya imani na sheria kwa sehemu zake mbili kuu ambazo ni; ibada na vitendo (matendeano) au tabia.
Hapana shaka kuwa tabia njema katika Uislamu zinatokana na imani na sheria, maana yeyote ambaye imani, ibada na matendeano yake ni sahihi basi tabia zake huwa njema, ilhali yule ambaye imani, ibada na matendeano yake ni mabaya basi tabia zake huwa mbaya. Kwani tabia ni kundi la maadili mema na sifa nzuri zinazolenga kufuzu duniani na akhera, na kuchangia kuleta amani na kuenea usalama, kwa kuwa amnai inategemea sana kuimarika kwa tabia njema, hakuna mtu atasikia amani na usalama wakati ambapo jamii inakosa tabia njema na maadili mema. Kwa hivyo, Qurani Takatifu imetia maanani maadili mema na pia Sunna ya Mtume (S.A.W.) imezingatia sana tabia, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amewabinishia waumini kanuni za kujumla za tabia Aliposema Akimhotubia Mtume wake (S.A.W.): "Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, najitenge na majaahili" [Al-A'araaf: 199]. Kwa sababu hiyo, familia wanawajibika hususan na jamii kwa jumla kupambana na lolote linaloweza kuathiria vibaya utulivu wa familia, kwa njia ya kuimarisha tabia njema na kuwashawishi wanachama wa familia washikamane na misingi ya tabia njema na sifa nzuri za familia katika Uislamu. Vile vile, tabia njema ina umuhimu mkubwa kwa mtu, familia, jamii, nchi na ulimwengu kwa ujumla, kwani zinachangia kupambana na maradhi hatari za kjamii zinazoweza kuharibu familia na jamii, kwa hiyo tunaweza kusema kuwa tabia njema kwa mtu ni sawa sawa na kichwa kwa mwili, roho kwa mwanadamu, ambapo mwili bila ya kichwa au mwanadamu asiye na roho huwa maiti isiyoathiri wa kuathiriwa, hivyo Mwenyezi Mungu (S.W.) Amemsifu Mtume wake (S.A.W.) kwa kuelezea kuwa tabia zake ni adhimu: "Na hakika wewe una tabia tukufu" [Al-Qalam: 4].
Kwa kumalizia tunasisitiza kuwa haki iliyo muhimu zaidi ya watoto juu ya wazazi ni kuwalea kwa msingi wa tabia njema, na sifa nzuri, kwa kuwa umma haupati ustawi wala maendeleo ukiwa unatilia mkazo malezi mema yanayozingatia kuwalea kizazi kwa tabia njema na sifa nzuri, hivyo basi tabia na sifa hizo zinakuwa msingi wa maendeleo ya jamii nzima. Pia, sababu ya kuleta manufaa kwa wote katika jamii kunalingana na kiwango cha tabia katika jamii hiyo, maana jamii ikikosa tabia njema haitapata mafanikio yoyote wala maendeleo ya kistaarabu au usatwi, kwa sababu ya mafanikio hayo yanatokana na tabia na maadili yaliyopo katika jamii. Kwa kweli, ushirikiano baina ya mwanaume na mwanamke ni jambo la lazima hasa kwa zama hizi kwa ajili ya kuandaa na kuunda familia yenye furaha, huruma, upendo na utulivu, tena jamii istawe na kuimarika na umma mzima kuendelea.