Fikra Potofu ndio Chanzo cha Uovu na Maafa

Imeandaliwa na Bw., Eslam Ragab Mohammed

  • | Thursday, 12 December, 2024
Fikra Potofu ndio Chanzo cha Uovu na Maafa

 

    Msingi wa uovu unapatikana katika fikra kali, kwani ndio mzizi wa uovu wote, upotofu na ugaidi katika historia yote, na kutoka fikra kali hutoka mawazo haribifu na itikadi potofu zinazowapeleka watu kwenye kupigana.

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kitabu chake kitukufu Alijali sana fikra na utambuzi unaodhihirisha itikadi ya mwanadamu, kwa hiyo aya za Qur’ani na kisha hadithi za Mtume S.A.W zinalenga kurekebisha fikra kuhusu masuala makubwa, ili kudhibiti uhusiano huo, baina ya mtu na Mola wake Mlezi, na baina mtu na viumbe vingine vyote.

Kama ikiwa wazo na utambuzi ni sawa, basi mwelekeo utakuwa mzuri, na hatua husogea kuelekea lengo linalotarajiwa, na kama ikiwa mawazo na utambuzi umepatwa na ufisadi, basi itikadi huharibika, moyo huwa mgonjwa, roho inakuwa mbaya, na nafsi inaelekea kwenye uovu.

Kwa hiyo, ombi la Baraza la Ulaya la Fatwa na Utafiti kuhusu kufanya mkutano wa (jambo la ukatili na fikra kali katika historia ya Waislamu); lilikuwa anastahili, kwani balaa, vikwazo na kushindwa vyote vilitokana na upotovu wa kiakili na fikra kali, vile vile fikra nzuri ndiyo inayolisukuma taifa kuelekea kwenye malengo yanayotarajiwa na kupata ustaarabu na maendeleo.

Sababu za kuwepo fikra kali:

Mitazamo ya watafiti na wanasiasa ilitofautiana kuhusu sababu za kuwepo fikra kali, baadhi yao wanahusisha kwa sababu za kiuchumi kama vile umaskini na ukosefu wa ajira, lakini sababu hii ni dhaifu kwa sababu kuwepo fikra kali si tu miongoni mwa masikini na wasio na ajira, bali ipo katika nchi tajiri na, kwa hivyo fikra kali ya kwanza iliyoambatana na vurugu ilionekana wazi katika miongo ya hivi karibuni ilikuwa katika kundi la Juhayman walioikalia kwa mabavu Al-Kaaba Tukufu na wakamwaga damu mwaka wa 1400 H, walishambulia utakatifu wa mahali na wakati, na katika nchi inayoinua kauli mbiu ya tauhidi, na makusudio yao hayakuwa suala la kiuchumi, bali sababu ilikuwa ufahamu usio sahihi. Na baadhi ya watafiti na wanasiasa walihusisha kuwepo fikra kali kwa sababu za kielimu, kisaikolojia, kijamii, kiakili, au sawa na hayo. Tunaweza kugawanya sababu hizi katika zifuatazo:

Sababu ya kwanza: kulea ya dini isiyo sahihi iliyoenea katika jamii, kama vile nyumbani, shuleni, chuo kikuu na msikitini.

Sababu ya pili: ukandamizaji wa kisiasa, dhulma na udikteta uliozuia uhuru wa maoni na mawazo, kuwakandamiza wapinzani kwa nguvu na silaha, aina za mateso na aina za madhara, na jela ambazo ni nje ya wigo wa utu na haki za binadamu.

Sababu ya tatu: ni ujinga uliochanganyikana na kukosa ufahamu wa dini na sheria za Mwenyezi Mungu Mtukufu: yaani baadhi ya watu hawana elimu wala ujuzi, lakini pia hawajui kwamba wao hawana elimu, au kwa maneno mengine: wanadhani kwamba wamefikia kiwango cha ijtihad, na wanaanza kutoa maoni yao katika masula ya kidini, lakini kweli ni kwamba wao hawajafikia kiwango hicho.

Sababu ya nne: umaskini, ukosefu wa ajira, na matatizo ya kiuchumi na kijamii, kwani mambo haya yana umuhimu wake, na hutumiwa na wale wenye fikra kali ili kuweka chuki baina ya watu, na kuwavuta vijana wenye uhitaji.

Masuluhisho:

Tiba madhubuti ya fikra kali - kama ugonjwa wowote - iko katika kutibu sababu zake kwa njia ifuatayo:

Kwanza: Kuemarisha elimu ya dini kwa elimu sahihi ya kidini, na Kuemarisha mazingira yanayokumbatia fikra kali kwa mazingira yanayokumbatia fikra sahihi, na kuweka mfumo wa kati katika imani, ibada, maadili na tabia, kupitia kueneza kwamba dini yetu ya Uislamu ni dini ya rehema kwa watu wote, dini ya usalama kwa mwanadamu, na dini ya amani kwa ulimwengu wote.

Pili: kuzingatia upande wa kuadhibu kupitia adhabu kama vile adhabu zinazohusiana na matokeo ya fikra kali na ugaidi, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka adhabu mbili kali kwa wale wanaosukumwa na fikra kali kwenye ugaidi na ukatili dhidi ya jamii na nchi nazo ni: adhabu ya vita na ufisadi duniani, na adhabu ya kushambulia nchi na usalama wake.

Kulingana na hayo hapo juu, fikra kali kinasababisha ugaidi, mauaji, na shambulio, na Uislamu umeweka kundi la adhabu ili kuwazuia magaidi kutekeleza matendo yao ya kikatili dhidi ya jamii, na pamoja ya hayo ni lazima na wajibu ya watafiti kuwafunza watu maadili na mafundisho sahihi ya Uislamu ili kukomesha fikra kali.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.