Ndani ya mfumo wa kazi ya Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra potofu wa kufuata mawazo ya makundi yenye fikra kali, na makala na habari wanazozitoa; Kituo kilifuatilia makala iliyochapishwa na gazeti la ISIS la Al-Naba, katika moja ya matoleo yake yaliyotolewa mnamo Novemba 2024 BK, yailigunduliwa ndani yake mawazo kadhaa ya sumu na ya uwongo, na shambulio kali dhidi ya Waislamu, makala hii inadai kwamba sababu ya kuchelewa umma na kushindwa kwake kupata ushindi ni kupotoka kwa maulama hawa, ambao makala iliwaita “maulama wa kutopiga vita”, wakati indapo makala hiyo inaonyesha suala la jihadi, tunaikuta kwamba inatazam juu ya msingi wa fikra kali, kupitia kuwatangaza wengine kuwa ni makafiri, bila ya dalili ya kisheria, hapa tutajaribu kukanusha baadhi ya tuhuma zilizomo, kulingana na dalili ya kisheria na ya kiakili kutoka maisha yetu ya kila siku:
Kwanza - Kuifahamu Jihadi katika Sheria:
Jihadi katika Uislamu ni ibada kubwa, nayo ni kilele cha dini, kama Mtume S.A.W alisema, lakini kama ilivyopo katika hukumu za kisharia zingine, jihadi ina udhibiti na masharti, yaliyobainishwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui" [Al-Baqarah: 190]; Kwa hivyo, inabainishwa kwamba sheria ya Kiislamu ilikuwa na nia ya kudhibiti jihadi kwa njia ambayo inafikia malengo ya jumla ya Uislamu, kama vile kujihifadhi nafsi, dini, akili, fedha na heshima.
Hapa ni lazima tutofautishe baina ya mapigano halali, ambayo ni kwa ajili ya kujilinda na kuondoa uadui, kulingana na wanavyoona wataalamu wa jambo hili, na mapigano ya machafuko, ambayo yanafanywa na vikundi ambao ni nje ya sheria, na yanaanza bila ya kupanga, huleta balaa juu ya umma, na yanakwaishwa kwa umwagaji damu usio na haki.
Makala hiyo inaacha udhibiti huu wa kisheria, na inawatukana wasomi na wanafikra wanaofichua uwongo wao na wanaofichua udanganyifu wao, na huwaeleza kwa “waenezao fitna” au “wasaliti”. Uelewa huu uliopotoka unaakisi ujinga wa makusudio ya Sheria, na umbali kutoka kwa uadilifu na wastani, na wakati tunaposoma makala na kuchunguza mambo yake ya ndani, hatuoni kwamba inatoa maono wazi ambayo yanaonyesha kina cha mawazo au kufikiri vizuri, badala yake, tunasoma maneno ya kiburi, matupu na yasiyo na maana yoyote sahihi.
Pili - Jihadi sio lengo, bali ni njia:
Moja ya makosa yenye hatari zaidi ambayo kundi la kigaidi lilifanya ni kwamba liliijaalia jihadi kuwa ni lengo peke yake, ingawa kwamba Jihadi katika Uislamu ni njia ya kufikia haki na kusimamisha dini, maulama walisema: kuacha jihadi katika baadhi ya hali huenda inakuwa wajibu; iwapo itadhaniwa kuwa itapelekea madhara makubwa zaidi, mfano wa hili ni: Mtume S.A.W aliweka mkataba wa amani pamoja na washirikina katika mkataba wa Hudaybiyyah; Mtume S.A.W aliacha baadhi ya haki za Waislamu (kama vile Umra); Kwa kuzingatia maslahi ambayo ni kubwa zaidi, wasifu wa Makhalifa Waongofu pia una hali nyingi zinazoonyesha kwamba kupigana sio lengo peke yake, bali ni njia inayotumika kulingana na haja, kiwango chake, na udhibiti wake uliowekwa na Sheria.
Tatu - Athari za fikra kali juu ya jihadi:
fikra kali haijaleta chochote ila ole kwa umma. Ushahidi wa hili ni: kuangamizwa kwa nchi za Kiislamu; kwani makundi mengi yenye silaha yaliyoanzishwa kwa jina la Jihadi yaliisha kwa kuchosha umma, na yalisabibisha kuwepo nchi zilizoharibiwa na raia waliokimbia makazi yao. Fikra kali pia linaharibu sura ya Uislamu; hayo kwa sababu kwamba matendo ya baadhi ya makundi yenye silaha ndio yameharibu sura ya kimataifa ya Uislamu; Jambo ambalo lilijaalia iwe vigumu kwa walinganiaji wa kweli wenye ujumbe wa kuwasilisha ujumbe wake wenye kuvumilia na unyoofu.
Nne - Kutia chumvi katika kukafirisha na uhaini:
Wazo la kuwatuhumu wengine kwa uhaini linadhihiri katika Makala, kwa kuzingatia matukio ya kibinafsi bila dalili ya kutosha, inapaswa kusisitizwa hapa kwamba uhaini na kuwatuhumu watu kwa ukafiri bila dalili ni haramu, kama alivyosema Mtume S.A.W: “Mtu akimwambia ndugu yake: Ewe mkafiri, basi mmoja wao amekufuru”. Basi vipi kuhusu mtu anayewatuhumu umma mzima au idadi kubwa ya Waislamu?! Ukweli ni kwamba makundi haya na mengineyo kama hayo yanafanya juhudi kubwa ili kuwatangaza umma kuwa ni makafiri na wasaliti, na yanawavutia wachafu na wajinga kwake; Kisha yanaunda mstari mpya kutoka watu ambao wanajitupa nafsi zao kwenye uharibifu.
Pia, kutoa hukumu bila ya utambuzi na mashauriano, na kuwashutumu wanachuoni na walinganiaji wote waliotofautiana nao kuwa ni “walinganiaji wa motoni” au “wasaliti” kunaakisi kiwango cha ujinga wao na tabia yao mbaya katika kutendana na wanaohitilifiana nao, Mwenyezi Mungu S.W Amesema: {Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amaniau la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangelilipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa sifadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yakemngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu} [An-Nisa: 83] Mwenyezi Mungu S.W Akasema kwamba wanavyuoni wanaiamini wanatoa hukumu kutoka Qur-aan na Sunna, na wala hawashikamani kwa maana awali za matini, na wala hawatie chumvi.
Kwa upande wake, Kituo cha Al-Azhar kinathibitisha kwamba makala hii iliyomo katika jarida la ISIS la Al-Naba inaakisi mwelekeo hatari wa kiakili unaotokana na fikra kali, na inaishia kwa kuwatangaza Waislamu kuwa ni makafiri na inagawanya safu zao. Ni wajibu juu ya Waislamu leo kuwaunganisha na kuwafuata wanazuoni wa kweli na taasisi za kidini zilizoidhinishwa ambazo zinasawazisha baina ya matini ya kisheria na Maisha ya kila siku, pia tunathibitisha kwamba hakuna shaka kwamba jihadi ni faradhi kubwa, na kwamba haijazuiliwa katika zama za sasa.
Wanachama wa kundi la kigaidi la ISIS wanaishi katika udanganyifu hatari: wanaamini kwamba wana " usafi wa kiakili na usafi wa kimtazamo" ambapo wanaamini kwamba wao pekee ndio wanaobeba bendera ya ukweli safi na njia iliyonyooka. Imani hii ambayo ipo ndani ya nafsi zao sio tu iliwajaalia kuwaainisha mujahidina wengine -waliotofautiana nao katika mtazamo wao- kuwa ni wapotovu, au wazushi, kama kwamba wao ni walinzi wa makusudio ya waumbwa na hukumu za dini.
Hotuba yao yanategemea ukiritimba wa ukweli na madai ya usahihi kabisa, sio tu wanahalalisha damu za wapinzani wao wasiokuwa Waislamu, bali pia wanatumia ndimi zao kutangaza kuwa Waislamu wenyewe ni makafiri, ISIS imekuwa mfano wa wazi wa kupotoka katika mawazo na mbinu, hawakubali wingi wa maoni au jitahada ya wanazuoni, bali wanajiweka kama kiwango kimoja cha ukweli, wanajiona kuwa ni kundi lililookoka na kila mtu mwingine anazama katika upotofu, na dai hili linawagawanya umma na linawapa maadui wa Uislamu nafasi ya kuiharibu sura yake na kuuzingira kifikra na kisiasa. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Atakase umma wetu kutokana na wazo hili potovu, kuunganisha neno lao, na kuwaepusha fitna iliyoonekana na iliyofichika.
Imefasiriwa na Bw., Eslam Ragab Mohammed
Kutoka kwa makala ya Kiarabu iliyoandaliwa na Kitengo cha Lugha ya Kihispania