Ufanisi ni Sababu ya Maendeleo ya Umma

Imeandaliwa na Dkt., Alaa Salah Abdulwahed

  • | Thursday, 16 January, 2025
Ufanisi ni Sababu ya Maendeleo ya Umma

 

     Bila shaka kufanya kazi yoyote kwa ufanisi na kwa namna iliyo bora ni jambo linalotakiwa, kwani linasaidia kufikia mafanikio yanayotarajiwa kutoka kazi hiyo. Umma wowote wa kiustaarabu huwa wanajali sana kazi na ufanisi wa shughli zinazofanywa nao.

Mwenyezi Mungu (S.W.) Ametupigia mifano bora zaidi katika ufanisi wa kazi, ambapo Ameviumba viumbe vyote kwa namna iliyo bora zaidi na kuvipanga katika hali isiyo na mfano, Mwenyezi Mungu Amesema: {Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasi na ruwaza; na anapo taka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa} Al-Baqara: 117. Pia, Mwenyezi Mungu Amesifu ufanisi wa uumbaji wake kwa viumbe na kuvipanga kwa namna iliyo bora zaidi kwa kusema: {Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo} An-Naml: 88.

Ifahamike kwamba ubora wa kazi na vitendo unaotakiwa ni ule ambao unaambatana na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu (S.W.) Peke yake, sio kwa ajili ya chochote kingine. Na ikiwa haki ya kazi na sharti yake kuu kwa mujibu wa mafunzo ya kiislamu ifanywe barabara, kama alivyosema Mtume (S.A.W.) katika hadithi iliyosimuliwa kutoka kwake na Bibi Asha (R.A.) aliposema Mtume: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu hupenda mmoja wenu akiwa anafanya kazi fulani, basi aitimize barabara". Pia, haki ya mwajiriwa apate ujira wake kamili kutokana na juhudi zake alizozifanya kwa ajili ya kuitimiza kazi hiyo, bila ya kumpunguzia haki yake wala kuchelewesha, kwa hiyo Mtume (S.A.W.) alisema: "Mpeni mwajiriwa ujira wake moja kwa moja baada ya amalize kazi yake".

Vile vile, mwajiriwa ana haki ya kupata maisha mazuri yenye kufaa na juhudi na taabu zake, na kupewa heshima ya jamii kulingana na mchango wake kujenga na kuendeleza jamii, pia apate hifadhi asidhulumiwa wala asinyonywa wala kutumiwa vibaya, ambapo mwajiriwa kwani ni mmoja wa wanadamu huwa na haki ya kupata cha kutosha kwa kuendesha maisha yake miongoni mwa chakula, vinywaji, mavazi, makazi n.k. Na huduma za lazima kama vile, huduma za afya na huduma ya mwili na roho, kwani roho pia inabidi kutukuzwa na kuhudumiwa kwa elimu na maarifa.

Ikumbukwe kwamba mwili huishi kwa kutegemea chakula, vinywaji, mavazi n.k. Wakati huo huo, roho inatakiwa kuhudumiwa kwa maarifa, elimu, mawazo yaliyo sawa, imani na itikadi. Umma unapaswa kukamilishana kukidhi mahitaji hayo ya kimwili na kiroho wenyewe kwa wenyewe, maana mtu akikosa uwezo wa kupata yanayomsaidia aitunza nafsi yake kimwili au kiroho, basi wengine wanatakiwa kumsaidia awe na mahitaji hayo. Kwa kubainisha maana hii Mwenyezi Mungu (S.W.) Amethibitisha kuwa wanaofanya hisani kwa wengine walio maskini, Akaeleza kuwa thawabu ya wanaofanya hisani na kuchangia kuboresha maisha ya wenzao haitapoteswa bure, bali watapata badala ya waliyoyatumia mengi tena mema zaidi: {Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya mema} [Al-Tawbah: 120], Pia Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na subiri, kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wawanao fanya wema} [Hud: 115].

Hivyo, tunaelewa kuwa Mwenyezi Mungu Hapotezi ujira wa wanaofanya kazi zao ipasavyo, sawa kazi hizo ni za dunia au dini, maana hukumu ni kwa jumla. Isitoshe, bali Mwenyezi Mungu Amethibitisha kwamba Atamlipia mtu kwa kazi yoyote wala kitendo chochote kikubwa au kidogo: {Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! * Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!} [Az-Zalzalah: 7-8].

Uislamu ndio dini iliyomtukuza kazi na wafanya kazi ikisisitiza umuhimu wa kazi kama ni kigezo kilicho muhimu sana kuwahukumia watu wala sio maneno tu. Dalili dhahiri ya umuhimu wa kazi kwa mtazamo wa Uislamu ni kwamba kazi imepewa nafasi ya kwanza hata kabla ya Jihad (Kupigania Vita kwa ajili ya Mwenyezi Mungu), ambapo Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu} [Al-Muzzammil: 20].

Naye Swahaba Mtukufu Omar bin Al-Khattab (R.A.) alikuwa anassema: "Hakika ni bora kwangu nife nikiwa kazini (sokoni) kuuza na kununua kuliko nife wakati wa kupigana vita katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu Ameweka kazi mbele na kuitaja kabla ya Jihad".

Kwa sababu ya umuhimu wa kazi na nafasi yake kuendeleza nchi na kuleta ustawi, Mtume (S.A.W.) amewapa wafanya kazi shime kubwa, ambapo Imamu Al-Twabaraniy amesimulia kutoka kwa Ka'ab bin Ajurah alisema: Mtume (S.A.W.) siku moja mtu mmoja alipita mbele ya Mtume na maswahaba wake wakamsifu uhodari na uvumilivu wake wakasema: Ewe Mtume! angekuwa mtu huyu mmoja wa majeshi wa waislamu (wakimshauri mtu amwite yule mtu awe mpiganaji katika jeshi kwa sifa zake nzuri), Mtume (S.A.W.) alijibu: huyu mtu akiwa ametoka kutafuta riziki ya watoto wake, basi yeye yu sawa na mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka arudi, hali hiyo hiyo akiwa ametoka kuwatunza wazazi wazee au kujitosheleka badala ya kuombaomba au kufanya uhalifu, basi yeye yuko sawa sawa na anaepigana katika njia ya Mwenyezi Mungu"

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.