Akili bandia na athari zake katika kushawishi utambulisho wa kidini... kupotosha matini za Qurani na Sunna kama mfano

Imeandaliwa na Kitengo cha Utafiti - Imefasiriwa na Bw., Farid Mohammed Farid

  • | Monday, 20 January, 2025
Akili bandia na athari zake katika kushawishi utambulisho wa kidini... kupotosha matini za Qurani na Sunna kama mfano

 

     Siku za sasa zinashuhudia maendeleo ya haraka katika teknolojia ya akili bandia, na uingiliaji wake katika maeneo mbalimbali ya maisha umekuwa hali halisi, Kutoka kwa uwanja wa fasihi na matumizi yake katika uandishi, tafsiri na uchambuzi, hadi uwanja wa kiufundi na kuunda nambari za programu, hadi nyanja zingine, Kufikia uwanja wa kidini na matumizi yake katika utoaji wa fatwa na kuandika utafiti wa kidini, na surah za Qur’ani Tukufu na hadithi za Mtume(S.A.W).

Shida haiko katika kutegemea akili bandia na kuwa sehemu ya zana zetu za kutimiza kazi na majukumu, au hata kufikiria juu ya suluhisho la shida au kitu kingine chochote, lakini hatari ni kwamba zana hii ya bandia iliyopangwa kuangukia mikononi mwa wasiohusika, Hasa katika nyanja ya kidini na ulinganiaji. Kama vile akili bandia hutoa fursa nzuri za maendeleo na ustawi na huchangia kuimaliza miradi mingi kwa urahisi na harakaharaka, inasababisha tishio kubwa ikiwa itatumiwa na wasiohusika. Kwa mfano, mtu asiye mtaalamu wa masuala ya kidini hawezi kuona makosa yaliyomo katika matini za kidini ambazo akili bandia inazitaja ili kuthibitisha hukumu au kuthibitisha kesi kama ilivyo katika Qur'ani Tukufu, hadith za Mtume, maneno yaliyosimuliwa kutoka kwa Maswahaba na Wafuasi, au fatwa muhimu za kisheria, n.k. Huenda wengine wakaitumia kwa ajili ya malengo ya kiutafiti basi husababishia kufanya makosa yasiyohesabika, ikiwa ni pamoja na kupotosha matini za Qur’ani Tukufu, kutunga Hadith ambazo hazipo na wala haisihi kuzinasibisha kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), au kutaja maneno ya Wafuasi ambayo hayakutajwa katika vitabu vya turathi, ikidai kuwa yametajwa katika baadhi ya vitabu, na kutaja marejeo yasiyosahihi baada yake.

Zana hizi mahiri zimeenea sana kati ya watumiaji kwa njia ya kutatanisha, na nyanja ya matumizi yake yametofautiana, pia wengi wa wahusika wameonya dhidi ya kuzitumia kwa njia isiyo ya kina, haswa katika nyanja maalum ambazo zinahitaji uelewa na utafiti kabla ya kuzama ndani yao, au kuzitumia katika  matini thabiti matakatifu ambayo hayakubaliki upotoshaji au taawili.

Baada ya kuenea maonyo mengi kuhusu madai ya upotoshaji unaofanywa na zana za akili bandia katika kuandika matini ya Qur'ani Tukufu na Sunna zilizotakasika za Mtume(S.A.W), kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali kiliamua kuwatahadharisha wasomaji na wafuasi wake juu ya mageuzi hayo ya hatari ambayo wengine hawaweza kutambue, haswa vijana, kulingana na tajriba iliyofanywa na kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali kwa zana za akili bandia zinazoitwa: "Meta AI" Basi tajriba ilikuwa kama yafuatayo:

ilipotakiwa kuandika aya ambazo ndani yake neno “riba” zilizotajwa katika Qur’ani Tukufu: ilitaja Aya 7, Aya mbili tu ambazo ni sahihi katika matini na marejeo, Aya mbili ambazo ni sahihi katika maandishi tu lakini zinatofautiana katika marejeo, Aya mbili zilizopotoshwa waziwazi, na Aya ambayo haikutajwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu(S.W) wala hata sehemu yake.

Labda asiye mhusika ambaye hahifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu hawezi kutambua upotoshaji huo, kisha anaweza kuitegemea katika utafiti wake au maswali yake kuhusu jambo fulani, jambo ambalo inaweza kusababisha kuchanganyikiwa katika imani yake, kupondoka mbali na dini ya kweli, au kumpeleka kwenye imani ya kuwa hakuna Mungu au msimamo mkali; Kwa sababu ya utata unaoweza kutokea kutokana na upotoshaji huo kamili au ya kisehemu.

kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali pia kilifanya jaribio jingine ambalo ndani yake kiliitakia “Meta AI” kutaja aya za Qur’ani tukufu zinazohusu hukumu za swala, basi ilitaja aya 13 miongoni mwake aya moja ambayo ni sahihi katika maandishi na kuhusiana na mada, lakini ni makosa katika marejeo, nayo ni:" Mkisha sali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala". aya hii imekuja katika sura ya Alnisaa aya (103) na siyo katika sura ya Almaidah aya (10). Na Aya nyingine ni sahihi katika maandishi na marejeo, lakini haihusiani na mada, ambayo ni:”Hamkuwauwa nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye wauwa. Na wewe hukutupa, walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye tupa” sura ya Alanfaal: aya (17), Ama Aya nyinginezo zimepotoshwa kikamili au kwa kisehemu, hivyo ilivyopotoshwa kikamili, kama vile:(kisha tawadhuni kwa ajili ya swala), (Na ikiwa mnapigana katika njia ya mwenyezi Mungu, basi jishughulishe na swala), (ikipatikana maji, osheni nyuso na miguu yenu), (Enyi mlio amini basi washirikina waumbaji wangu wakupeni kitu kutoka kwa Mwenyezi Mungu hali wanajaribu) na baadhi ya aya zilizopotoshwa kisehemu, kwa mfano:( Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka magoti mawili), (basi mkisalimika hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu).

Ama kuhusu Sunnah iliyotakasika ya Mtume(S.A.W), iliulizwa kuhusu hukumu ya mtu aliyelala na hakuswali Swalah ya Isha, na kama inavyodhihiri katika picha kiasi cha upotoshaji uliojitokeza katika Aya za Qur’ani tukufu na Hadithi za Mtume(S.A.W). Aya ya kwanza iliyoitaja imepotoshwa na haina uhusiano wowote na mada ya swali, na aya ya pili pia imepotoshwa, Ama Hadiyth tatu zote ni Hadithi za kutungwa na kuumbwa, na hazipo katika matini hizi.

Imebainishwa kutokana na tajriba zilizotangulia kwamba zana hii na zana nyinginezo na matumizi yanayotegemea akili bandia huonesha kwa msomaji kama kwamba ni mtu msomi anayetoa majibu sahihi na ya kina, Anagawanya jibu kwa vipengele kadhaa na chini ya kila kipengele huorodhesha maelezo ya kina, lakini kwa kweli yuko mbali na sahihi, kwani majibu yake ni ya kutungwa au ya uwongo, au sio sawa, au angalau yanazunguka jibu sahihi, na watu wachache tu wanaotambua hilo.

Matumizi ya zana hizi yameenea sana kati ya watumiaji katika muda mfupi sana; Kwa sababu ni bure watumiaji wote wanapatikana kwa urahisi, ambalo linazua wasiwasi kuhusu matumizi yake mabaya au kuegemea kwake katika masuala ya kidini, Iwe ni katika jaribio la mtu binafsi au utafiti wa kitaaluma, au kuitegemea na wataalamu kama vile: walinganiaji na watoaji hotuba ili kuwapa habari, au kurekebisha hotuba au utafiti wa kitaaluma kwa njia ya ufasaha na ubunifu zaidi, na wakati huo huo vibaya na kupotoshwa zaidi.

kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali kinatahadharisha dhidi ya kutumia zana hizo bila ya kutia maanane, pia kinasisitiza kuhakiki taarifa zilizomo ndani yake na kutozitegemea katika nyanja maalumu na ya kina hasa katika masuala yanayohusu dini na akida ya Kiislamu; Kwa sababu hii inaweza kusababisha kuwapotosha baadhi ya Waislamu, pia kupotosha matini ya kidini, na kueneza imani ya kuwa hakuna Mungu au za itikadi kali, pamoja na upotoshaji wa kimakusudi kwa matini madhubuti ambao baadhi ya maadui wa dini wanaweza kutumia kama kisingizio cha kuhoji dini ya Kiislamu, au kupinga imani za Waislamu na akida zao.

Pia kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali kinausi mtu lazima azishughulikie na zana hizo zenye akili bandia kwa tahadhari kali na kuzitumia tu katika kupata taarifa za kiujumla bila kuzitegemea katika taarifa maalumu na za kina, Inaweza pia kutumika kutengeneza programu za elimu ya kidini zinazojumuisha teknolojia na dini kulingana na michango iliyopitiwa na kwa uangalifu.

Pia kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali pia inapendekeza umuhimu wa kuwaelimisha vijana na wadogo kuhusu ulazima wa kuhifadhi utambulisho wa kidini katika zama za kidijitali na kutoongozwa na matokeo yanayotolewa na programu zinazopatikana bila utafiti na masomo, kwa kuandaa midahalo na mikutano ya kidini inayojumuisha pamoja wasomi wa kidini na wataalamu katika teknolojia ya akili  bandia.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.