Wanawake Mashuhuri wa Kiafrika .. Mifano angavu na Majukumu nyeti (6) "Zenzi M. Makeba, na Giselle Rapishella"

Imeandaliwa na Dkt., Hossam El-Din Mostafa

  • | Wednesday, 29 January, 2025
Wanawake Mashuhuri wa Kiafrika .. Mifano angavu na Majukumu nyeti (6)  "Zenzi M. Makeba, na Giselle Rapishella"

 

Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu kinaendelea kutoa sehemu ya sita ya mfululizo wa makala zinazohusu baadhi ya mifano angavu katika tarehe ya mafanikio ya bara la Afrika ya wanawake mashuhuri ambao wako hai au walioaga dunia, lakini kumbukumbu zao zimesalia katika kina cha historia. . Miongoni mwa mifano hii angavu:

Zenzi Miriam Makeba

“Zenzile Miriam Makeba” aliyefahamika kwa jina la utani "Mama wa Afrika" alikuwa Balozi wa Heshima wa Umoja wa Mataifa na mwanaharakati wa haki za kiraia. Alijulikana kama mmoja wa sauti muhimu zaidi zinazopinga mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Alishinda Tuzo ya Muziki ya “Grammy”, alipoteza uraia wake na kulazimika kukimbia Marekani kwa sababu ya nyimbo zake dhidi ya ubaguzi wa rangi. Alirejea Afrika Kusini baada ya “Nelson Mandela” kuwa rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo.

Giselle Rapishella

Mwanamke wa kwanza wa Kimadagaska kupata kiti katika baraza la manispaa na kushiriki katika siasa mwaka 1956, pia aliongoza chama cha kisiasa mwaka 1958, na kuteuliwa kuwa waziri mwaka 1977. Aidha, alianzisha gazeti lililoitwa “Imongo Vaovao” kwa ajili ya kutetea haki za binadamu, na alijitolea maisha yake kutetea uhuru wa Madagascar.

*****************

Hivyo, wanawake wengi wa Kiafrika wamechukua kazi muhimu na zenye ushawishi katika jamii zao, kama ilivyo kwa "Sahle Warq Zewde" ambaye aliteuliwa kuwa Rais wa Ethiopia, na "Catherine Samba Panzao" aliyekuwa Rais wa Mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya Raisi "Djotodia" kupitia baraza la mpito kati ya mwaka 2014 hadi 2016. Pia, "Dlamini Zuma" aliyeshika nafasi ya Urais wa Umoja wa Afrika, na "Fawzia Adan" aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa kwanza nchini Somalia.

Kuna pia wanawake waliotoa mifano mizuri ya uvumilivu na kujitolea. Huko Rwanda, kuna idadi kubwa zaidi ya wanawake wabunge duniani kote. Aidha, shujaa wa mauaji ya kimbari makubwa zaidi alitoka nchini humo, ambapo wanawake walifanya binduzi, wakiwemo "Norah Bagirinka," mmoja wa walionusurika na mauaji hayo, ambaye alianzisha shirika la "Wanawake wa Rwanda wenye harakati" akitangaza nia yake ya mabadiliko. Hii inatoa taswira kwamba mchango wa wanawake barani Afrika umeanza kuzaa matunda.

Hivyo ndivyo Afrika ilivyokuwa, na licha ya changamoto na matatizo yanayoendelea, bara hili lina rasilimali zinazoweza kufanikisha maendeleo ya kina. Msingi wa rasilimali hizi uko katika kumwezesha mwanamke. Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu kinathibitisha kwamba iwapo uwezo wa wanawake utaimarishwa ili wawe sehemu muhimu katika mchakato wa amani na mabadiliko ya kijamii, kumshiriki katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo, na kupatiwa fursa zote ipasavyo, basi wataweza kusaidia bara hili changa kwa njia bora zaidi kutoka kwenye matatizo yake na kuharakisha maendeleo barani Afrika. Hakika, kumwezesha mwanamke ni kumwezesha ubinadamu.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.