La kuzingatiwa kuwa mahusiano yote yanaasisiwa juu ya familiya ambayo inashikamana na kupendana, na kwamba tukiwa tunataraji jamii yetu iwe ni jamii ya upendo, huruma, upole, uadilifu na hisani basi hatuna budi kuangalia hali ilivyo familia kwani ni msingi wa jamii yote. Na tunaposema familiya tunakusudia wanachama wote wa familiya hiyo, ambapo kila mmoja ana wajibu wake na haki zake kwa lengo la kufanikiwa katika kutekeleza muradi wa kuundwa kwa familia hiyo.
Uislamu ulihimiza kujenga familia ya kiislamu kwa misingi ya kuwapa wanachama wote wa familia hiyo jukumu maalumu kila mmoja kutokana na kadri na nafasi yake, kwa mujibu wa kauli yake Mtume (S.A.W.): "Kila mmoja wenu ni mtawala na ana majukumu juu ya walio chini yake, ambapo kiongozi ni mtawala atakaeulizwa kuhusu watawaliwa wake, na mwanamume katika nyumba yake ni mtawala na ataulizwa kuhusu watawaliwa wake ambao ni jamaa zake, na mwanamke pia ni mtawala wa nyumba ya mumewe na watoto wake na ataulizwa kuhusu watawaliwa hawa, na hata mtumishi ni mtawala wa mali na kazi ya bwana wake na ataulizwa kuhusu watawaliwa wake, kwa kweli nyote ni watawala na mtaulizwa kuhusu raia wenu"
Kuhusu ulezi wa mwanamume na utunzo wake kwa jamaa zake huwa kwa mujibu wa amri aliyopewa na Mwenyezi Mungu kwa kuwafanyia wema na hisani mkewe na wanawe, na ulezi wa mke kwa nyumba wake huwa kwa kuwahudumia kwa wema na hasa na mumewe ambapo uhusiano mzito zaidi ni wa mume na mkewe kama ilivyoeleza Qurani Takatifu kuwa uhusiano huu hutegemea upendo, huruma, upole, wema, utulivu, kutambua fadhila ya kila mmoja na mwingine, kuzingatia haki na wajibu na kuunda familia inayoweza kuchangia kuanzisha jamii imara na yenye ustawi na utulivu.
Aidha, Uislamu uliamrisha kuzingatia rehma na huruma kama ni misingi inayotakiwa katika miamala na wanachama wote wa familia, kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na kaeni nao kwa wema} [4/19], naye Mtume (S.A.W.) alisema: "Kwa hakika mwislamu yeyote anaetoa sadaka au matumizi ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu hupata malipo mema ya kitendo hicho mpaka chakula anachokiletea kwa mkewe". Kwa upande mwingine, mke alikuwa anateseka sana kabla ya Uislamu haujakuja ambapo alikuwa anakatazwa kupata chakula na mumewe meza moja na alikuwa anadharauliwa sana, pengine dini hiyo ya rehma na huruma imemtaka mume amlishe mkewe, bali zaidi ya hayo Mtume mwenyewe alikuwa mfano bora wa mume akisema: "Aliye bora kati yenu ni aliye bora kwa jamaa zake na mimi ndiye bora kwa jamaa zangu" na alipokuwa akisifu upendo wake kwa Bi.; Asha alikuwa anatafuta mahali pa mdomo wake kwenye kikombe ili anywe kutoka katika mahali hapa hapa na kusema: "Kwa kweli nimeruzukiwa upendo wake"
Ama kuhusu watoto na kuwafanyia upole na mema, basi Uislamu ulinimiza sana kuwatunza watoto na kuwalea kwa msingi wa upendo, huuruma na upole. Si la kushangaza kuelewa msimamo wa Mtume (S.A.W.) kutoka yule swahaba anaeitwa Al-Aqraa Bin Haabis Al-Tamimiiy aliyekuwa na watoto kumi na alikuwa anasema Wallahi nina watoto kumi sikumbusu mmoja wao hata mara moja, kwa hiyo Mtume alimtazamia kwa ukali akamwambia: "Asiye na rehma na wengine hastahiki kuruhumiwa na Mwenyezi Mungu".
Kwa mujibu wa mafunzo ya Uislamu wazazi wanatakiwa kuwafanya wanao miamala mazuri kwa usawa na uadilifu. Na katika hadithi yake Mtume (S.A.W.) amesema: "Hapana malezi bora kuliko tabia njema". Aidha, Uislamu umewajibisha uadilifu baina ya watoto wote katika miamala na utunzi, kwa hiyo tunasimuiliwa kutoka kwa Al-Numaan bin Bashir kwamba babake alimpa mtumishi kama zawadi ili amsaidie shughuli zake, lakini mama yake alikataa akimtaka mwanawe aombe shauri la Mtume (S.A.W.) basi Bashir bin Saad alikwenda kwa Mtume (S.A.W.) akasema: "Je, umewapa wanako wote kama ulivyompa Al-Nuaman? akajibu: hapana, akasema Mtume: Mcheni Mungu na fanyeni uadilifu baina ya wana wenu". Kwa hiyo, familiya ya kiskamu inapaswa kuzingatia sana kuwalea watoto wake kwa mujibu wa mafunzo ya dini hiyo adhimu kwa ajili ya kuwafanya kizazi wema wanaoweza kuleta mafanikio, maendeleo na ustawi kwa ukoo wao, jamii yao, nchi yao na ubinadamu kwa jumla.
Uislamu imwajibisha malezi yaliyo bora kwa mujibu wa mafunzo ya Qurani Takatifu kama vile mafunzo yaliyotajwa katika sura ya Luqman ambapo sura hii imebainisha misingi ya malezi bora yanayotegemea tabia njema na sifa nzuri, hebu tuangalie baadhi ya Aliyoyasema Mwenyezi Mungu katika sura hiyo: { Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpamawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu.Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa* Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mamayake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu,na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwanguMimi ndiyo marudio* Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayohuna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwawema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Miminitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda* Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe yakhardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu aundani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo fichika,Mwenye khabari za yote* Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, nakataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo nikatika mambo ya kuazimiwa* Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchikwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna na kujifakhirisha* Na ushike mwendo wa katikati, na teremsha sautiyako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shakailiyo zidi ni sauti ya punda} [31/13-19]
Na kutoka kwa Ayubu Bin Mussa bin Amr bin Saidi bin Al-Aasi kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: "Hakuna kitu anachotoa baba kwa mwanawe bora kuliko tabia njema" kwa hiyo tunasema kuwa misingi hiyo ndiyo misingi inayojenga familiya inayoasisi jamii imara na yenye ustawi na maendeleo.