Sheikh wa Al-Azhar, Prof/ Dr. Ahmed Al-Tayyeb, na Mwenyekiti wa Baraza la Wakuu wa waislamu, alitoa hotuba katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Islamofobia, maadhimisho hayo ni matokeo ya juhudi, zilizobebwa na kundi la nchi za Kiislamu katika Umoja wa Mataifa, ili kukabiliana na hali hiyo isiyo ya kawaida, ambayo sasa imekuwa tishio la kweli kwa amani ya dunia.
Sheikh wa Al-Azhar, katika hotuba iliyotoa kwa niaba yake balozi Osama Abdel Khaleq, kwenye Umoja wa Mataifa, alieleza kuthamini sana misimamo ya haki na ya ujasiri ya Bw. António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na maneno yake ya haki kuhusu Uislamu, yanaonyesha uelewa wa kweli wa dini hii na mafundisho yake yenye huruma.
Imam Mkuu alibainisha kuwa neno "Uislamu" limetokana na neno "Amani" katika lugha ya Kiarabu, na linadhihirisha maadili yaliyoletwa na ujumbe wa dini hii tukufu, maadili: huruma, upendo, maelewano, uvumilivu, na udugu kati ya watu wote bila kujali rangi zao, imani zao, lugha zao, au asili zao. Hili limethibitishwa na maneno ya ALLAH katika Kitabu chake kitukufu: (hakika hatukumtuma ila rehema kwa walimwengu), [Al-Anbiya: 107], aya ambayo inadhihirisha kiini cha ujumbe wa Uislamu. Uislamu unahimiza maadili ya udugu, haki, na uvumilivu miongoni mwa wanadamu, kwa kuwa wote ni ndugu wanaotokana na baba mmoja na mama mmoja.
Aliendelea kusema kuwa inatosha kuthibitisha usamehevu wa wa dini hii tukufu kwamba Waislamu waliishi kwa karne nyingi bega kwa bega na wafuasi wa dini nyingine kwa amani kamili na ushirikiano wa kujenga, wakitokana na imani thabiti katika maneno ya ALLAH katika Qur'an Tukufu: (hakuna kulazimisha katika dini), [Al-Baqara: 256], kutoka hapa, historia imethibitisha kuwa "Uislamu" ni dini ya amani, na kwamba ujumbe wake unahimiza kufahamiana, kushirikiana, na kukataa migogoro na migawanyiko, ma kwamba usamehevu wa dini hii si madai yasiyo na ushahidi, bali ni ukweli ulioshuhudiwa na jamii nyingi mashariki na magharibi kwa karne nyingi, na imekuwa sehemu isiyoweza kutenganishwa na utambulisho wao na ujumbe wao kwa ulimwengu mzima.
Sheikh wa Al-Azhar alifafanua kuwa islamofobia, si ila matokeo ya kutojua ukweli wa dini hii tukufu na usamehevu wake, pamoja na juhudi za makusudi za kupotosha kanuni zake, ambazo msingi wake ni amani na kuishi pamoja kwa maelewano. Hali hii ni matokeo ya kawaida ya kampeni za vyombo vya habari na hotuba za mrengo wa kulia zenye misimamo mikali, ambazo kwa muda mrefu zimeuonyesha Uislamu kuwa ni dini ya vurugu na misimamo mikali—uwongo mkubwa zaidi katika historia ya kisasa.
Upotoshaji huu umetokana na tafsiri potofu na matumizi ya hila ya matukio ya kikatili ya kijeshi yaliyofanywa na makundi ambayo yako mbali kabisa na Uislamu. Je, itawezekanaje kwa dini hii, ambayo waumini wake hawawezi kukamilisha imani yao bila kuamini katika kanuni za kitabu chao kitakatifu.
Imam mkuu alisisitiza kuwa changamoto kubwa zinazozunguka dunia yetu leo, kama vile vita, migogoro, na ongezeko la haraka la hotuba za chuki, ubaguzi, na ukatili, zinatufanya tuungane na kuimarisha mshikamano ili kujenga madaraja ya kuelewana juu ya magofu ya ujinga, kiburi na chuki. Hii inatufanya kuwa na jukumu la kuwasha mishumaa ya hekima katika mapango ya picha za kijumla na giza lake nene. Mazungumzo kati ya dini na tamaduni leo sio anasa, bali ni hitaji la kimaisha ili kuokoa ubinadamu kutoka kwenye minyororo ya ujinga na kutokuelewana. Maneno yetu yanapaswa kuwa daraja linaloondoa hofu ya uislamofobia kupitia hotuba ya wastani na kushikilia msimamo wa kuwa wazi kwa wengine.
Pia, Imamu Mkuu aliiita jamii kukabiliana na hotuba za chuki zinazojitokeza kupitia hotuba na vitendo vya kila siku katika majukwaa ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, kama ilivyo kwa mamilioni ya Waislamu duniani kote; kama jibu kwa dhamiri ya kibinadamu inayotulazimisha kufanya hivyo, kwa kuinua hotuba za mazungumzo, uvumilivu na maisha ya pamoja, na kufanya kazi pamoja ili kutoa sheria zinazolazimisha, na kuanzisha kampeni za kuhamasisha zinazopanda mbegu za uvumilivu katika ardhi ya uelewa, na kuimarisha tamaduni ya heshima ya pande zote; ili tushirikiane katika kutengeneza hotuba inayoweza kurejesha uhusiano wa kuelewana, mshikamano, na undugu kati ya mataifa.
Vile vile, Imam Mkuu alieleza kwamba Dini ya Uislamu inawalazimu Waislamu kuwa na imani ya kidini inayosema: kwamba utofauti wa kidini na kitamaduni ni sheria iliyoamuliwa na hekima ya Muumba; kama ilivyo semwa na Mwenyezi Mungu:{Na Allaah Akitaka Angewafanya watu wote wafanane lakini wako tofauti tofauti na hiyo ni mojawapo hekima za uumbaji wao} [Hud: 118], na kwamba utofauti huu ni utajiri na si vita. Pia, kupambana na uislamofobia siyo kupigania kundi moja dhidi ya lingine, bali ni vita ya kila mtu mwenye dhamiri ambaye moyo wake unadunda kwa upendo wa haki.
Aidha, Imam Mkuu alieleza kwamba Al-Azhar Al-Sharif, ambayo ni rejea ya kihistoria ya Uislamu na nguzo ya wastani na usawa, pamoja na Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu - linaloongozwa na yeye - limeanzisha alama ya hatari tangu muda mrefu kuhusu kuenea kwa hali hii ya kigeni, baada ya juhudi zao kuungana na kuelekea kufungua milango ya mazungumzo kati ya Mashariki na Magharibi, ambayo ilikamilika kwa kutolewa kwa Hati ya Udugu wa Kibinadamu ya kihistoria, ambayo ilitiwa saini na yeye pamoja na ndugu yake Baba Francisko, Papa wa Kanisa Katoliki, huko Abu Dhabi mwaka 2019, pamoja na kuandaa mfululizo wa mikutano ya kimataifa ya kiakili, kutuma misafara ya kielimu duniani kote, na kuandaa vizazi vya wahubiri na wageni kama mabalozi katika misafara ya amani ya kimataifa ambayo ilizunguka Mashariki na Magharibi, ikileta ujumbe wa Uislamu wa upole, ukikataa kila aina ya hotuba za chuki na kutishiana, na ikihimiza kukuza maisha ya pamoja ya kibinadamu na ujumuishi chanya unaoegemea mazungumzo na ushirikiano, si mapigano na migogoro.
Imam Mkuu aliendelea kusema: "Kati ya juhudi za Al-Azhar katika kukabiliana na janga la uislamofobia ni kuanzishwa kwa Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Uzalendo wa Kiitikadi, ambacho kinajukumu la kufafanua dhana za dini sahihi kwa Waislamu na wasio Waislamu katika maeneo mbalimbali duniani. Aidha, kinapambana na fikra za kikatili, makundi ya kigaidi, na harakati za vurugu, na pia kinachunguza vitendo vya vurugu dhidi ya Waislamu vinavyosababishwa na dhana ya uislamofobia, kwa njia ya kufuatilia kila siku matukio ya vurugu duniani, na kuhamasisha ushirikiano chanya ili kupambana na hali hii hatari katika jamii zinazokubaliana nayo."
Sheikh wa Al-Azhar aliita na kusisitiza kuitaka dunia kuweka tafsiri ya kimataifa ya dhana ya uislamofobia, ambayo itajumuisha kuanzisha seti ya maneno na vitendo vilivyoelezewa kwa mara kwa mara, na kuonyesha hofu au kuchochea chuki au vurugu dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa sababu ya imani yao ya kidini. Alisisitiza pia kuanzishwa kwa hifadhidata kamili na za kisasa za kutambua uhalifu na vitendo vya ubaguzi wa rangi na kibaguzi dhidi ya Waislamu kwa sababu ya dini yao, na kufuatilia sheria na sera ambazo zinaongeza tatizo hili, au ambazo zinaweza kutoa suluhisho zinazosaidia kukabiliana nalo. Lengo la juhudi hizi ni kutunga sheria na kanuni zitakazozuia dhana hii, na kuhamasisha badala yake kukuza maadili ya: mazungumzo, uvumilivu na maisha ya pamoja ya kibinadamu.
Mwishoni mwa hotuba yake, Imam Mkuu alisisitiza kuwa vita dhidi ya uislamofobia ni juhudi endelevu za kiutendaji ambazo zinapaswa kutekelezwa katika maeneo ya: elimu, mazungumzo, vyombo vya habari, na sheria zinazolinda heshima ya mwanadamu, kwa ajili ya kila mwanadamu. Alisisitiza umuhimu wa kushirikiana mikono, serikali na mashirika, ili kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya ufanisi wa hatua na mipango inayolenga kupambana na uislamofobia, ikijumuisha viashiria muhimu vya utendaji, na kujenga dunia ambapo jua la haki na maisha ya pamoja linang'aa, huku bendera ya undugu kati ya wanadamu ikipepea angani.
Imefasiriwa na Bw., Said Moshtohry