Kuhusu Madai ya ISIS ya Kuwakufurisha Jamii.. Mtazamo wa Kichambuzi

Imefasiriwa na Bw., Eslam Ragab Mohammed

  • | Monday, 17 March, 2025
Kuhusu Madai ya ISIS ya Kuwakufurisha Jamii.. Mtazamo wa Kichambuzi

 

     Tangu lilipoibuka kundi la kigaidi la ISIS, takfir imekuwa ni njia ya kudumu katika itikadi yake, kwani imeelekeza juhudi zake za kuzitangaza nchi na jamii za Kiislamu kuwa ni makafiri, kwa kutumia tuhuma za uwongo za tafsiri ya matini ya kisheria ya Qur’ani, Sunnah na Qiyas ya kisheria. Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali kimekabiliana na fikra hii kwa kuikanusha kimantiki na kimaandishi, na kudhihirisha upinzani wake kwa misingi na malengo makuu ya Uislamu.

Katika makala ya toleo la Alhamisi iliyopita, 6 Machi, 2025, la gazeti la ISIS la Al-Naba, iliyopewa jina la: "Njia ya Utukufu," kundi hilo linageuka kutoka wazo la utukufu, kufurahi kwa imani na wazo la kuamini Mungu mmoja, kwenye wazo la kuwakafirisha jamii na kuzishutumu kwa unafiki, na mambo mengine. Nalo ni wazo ambalo kundi limevuka ndani yake mipaka ya Sheria na akili kwa ujumla na kwa undani, Anasema:

 “Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuwazia kwamba mtu anaweza kutafuta heshima mbali na uwepo wa Mwenyezi Mungu, akiacha jambo la utumwa kwake, na anasujudu kwenye vizingiti vya wadhalimu, akizurura mikusanyiko na majumba yao, kama vile vinavyofanywa leo na makundi na vyama vingi vilivyoacha Uislamu!"

Makala hii inalenga kutoa usomaji wa kiuchambuzi kwa mawazo yaliyotolewa katika gazeti lililotajwa hapo juu.

Kwanza: Misingi ya kimantiki ya kukanusha wazo la ISIS la kuzikafirisha jamii

Msingi wa kuwakafirisha watu unapingana na akili na mantiki

Hakika kuhukumu juu ya jamii kwa ujumla wake kuwa ni makafiri hupingana na maumbile na akili iliyonyooka,

kwani, itawezekanaje kwa taifa kuungana juu ya uwongo, hali Mwenyezi Mungu S.W ameahidi kuihifadhi dini hii? Bila shaka kuzikafirisha Jamii hupelekea kwenye machafuko ya kidini na kijamii, na hufungua mlango wa ufisadi na mapigano, jambo ambalo linapingana na madhumuni ya Sheria katika kuhifadhi maisha, akili na dini.

kukafirisha kwa pamoja kunapingana na msingi wa uhasibu wa mtu binafsi

kwa mujibu wa akili na mantiki, hairuhusiwi kujumlisha hukumu kwa watu binafsi kwa kuzingatia matendo ya mamlaka au serikali; Qur’ani Tukufu inasisitiza wajibu wa mtu binafsi, Mwenyezi Mungu S.W anasema: “Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?” (An-Najm: 38). Je, taifa zima linawezaje kutuhumiwa kwa kufuru kwa sababu ya sera fulani ambazo watawala wake wanaweza kuzipitisha? Hii ni dosari ya kimantiki inayopinzana na kanuni za msingi za kimantiki za haki na uadilifu.

Kupiga jamii za Kiislamu na kuwatumikia maadui wa Uislamu

Mfumo wa ISIS wa takfir umesababisha tu kugawanyika kwa jamii za Kiislamu na kumwaga damu ya Kiislamu, jambo ambalo hutumikia maslahi ya majeshi yenye uadui kwa Uislamu. Badala ya kuelekeza juhudi kwenye ujenzi na mageuzi, watu hawa wanashughulika na kuchochea mizozo na vita vya ndani, ambavyo vinasababisha kuanguka na kuporomoka kwa nchi za Kiislamu badala ya kuzisimamisha na kuzistawisha.

Pili: Dalili ya kimtaini juu ya ubatili wa takfir kwa jamii na nchi

Matini ya Qur’ani Tukufu zinazokataza takfir

Quran Tukufu inaonya dhidi ya kuwatuhumu wengine kwa ukafiri, na inathibitisha kwamba asili ya Mwislamu ni imani, si ukafiri. Mwenyezi Mungu S.W Anasema: "Enyi mlio amini! Mnapo safiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni, wala msimwambie anaye kutoleeni salamu: Wewe si Muumini" ( An-Nisa: 94). Je, ISIS inawezaje kutangaza jamii nzima na nchi kuwa ni makafiri bila ya uthibitisho, wakati Qur’an imekataza hata kumtangaza mtu Muislamu mmoja kuwa ni kafiri?

Sunnah inatahadharisha dhidi ya kumtangaza mtu kuwa ni mkafiri

Sunnah ya Mtume (S.A.W) ilitoa maonyo makali dhidi ya jambo la takfir bila haki, Mtume (S.A.W) amesema: "Mtu akimwambia ndugu yake: ‘Ewe kafiri, basi mmoja wao atakuwa na hatia katika hilo". kundi lenye fikra kali linawezaje kujinasibisha lenyewe uwezo wa kuzitangaza nchi na jamii kuwa ni makafiri, wakati Mtume mwenyewe hakufanya hivyo?

Makubaliano ya kifiqhi juu ya hatari ya takfir

Wanachuoni wa Umma wameafikiana kupitia karne zote kwamba takfir ni suala hatari ambalo halipaswi kuchukuliwa kirahisi, na kwamba kanuni ya msingi ya Muislamu ni Uislamu mpaka kudhihiri uthibitisho wa ukafiri wakeAl-Imaam Al-Nawawiy anasema: “Muislamu hazingatiwe kuwa ni kafiri isipokuwa akifanya jambo ambalo haliwezi kufasiriwa", Je, ISIS inawezaje kujenga mawazo yake juu ya tafsiri mbovu na kuyashutumu mataifa yote kwa ukafiri?  

Dhana ya dola katika Uislamu na kukataliwa kwa takfir

Uislamu ni dini ya utaratibu na uadilifu hautaki kuziharibu serikali na kuzipindulia nchi kwa kisingizio cha takfir, bali unahimiza utii kwa watawala katika mambo yote isipokuwa kumuasi Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu S.W Anasema: "Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi" {An-Nisa: 59}. Ama madai ya ISIS, yanasababisha machafuko na umwagaji damu, jambo ambalo linapingana na malengo ya Uislamu na ujumbe wake, ambao ulikuja kama mwongozo kwa walimwengu, kuendeleza ulimwengu, na kusimamisha amani na utulivu kati ya umma na jamii.

Tatu: Athari ya itikadi ya kitakfiri ya ISIS juu ya taifa la Kiislamu

kusambaratisha umoja wa Waislamu

Kuenea kwa itikadi ya ISIS kumesambaratisha safu za Kiislamu na kumebadilisha jihadi kutoka kukabiliana na maadui wa kweli kwenye kuwaua Waislamu na kumwaga damu zao, jambo lililodhoofisha taifa, likalitumbukiza katika kinamasi cha fitna, likasambaratisha umoja wake, na akaeneza mgawanyiko wa maoni na maamuzi kati ya watu wake.

Kupotosha sura ya Uislamu duniani kote

Sio siri kwamba hali na mawazo haya yamesababisha unyonyaji wa jinai za ISIS na vyombo vya habari vya Magharibi katika kueneza taswira potofu juu ya Uislamu na kuwajaalia Waislamu kama watu waovu, jambo ambalo limezidisha mawimbi ya chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa rangi na limesabibisha kuteswa kwa Waislamu katika sehemu mbali mbali za ulimwengu.

Kuziharibu akili za vijana

 kupitia propaganda zake potofu, kundi la ISIS liliweza kuwahadaa baadhi ya vijana na kuwavutia kwenye safu zao, wakitumia kutojua dhana sahihi za dini na ulaghai wao kwa kauli mbiu za uwongo na maneno yenye mvuto.

Hatimaye, tunathibitisha kwamba Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali kimejibeba jukumu la kupambana na jambo hili, kupitia kueneza ufahamu sahihi wa kidini na kukataa kabisa maoni ya kupotosha kutoka kwa dini, kwa kuzingatia dalili za kiakili na kimatini, na kufichua uwongo wa kile kinachodaiwa na fikra ya kitakfiri iliyofanywa na ISIS, kikionyesha kwamba inapingana kabisa na misingi ya Uislamu wenye uvumilivu, na haina msingi wowote wa kisheria, na kusisitiza kwamba ni wajibu wa Waislamu, hasa wanazuoni kupambana na fikra hii potofu kwa kueneza ufahamu, kurekebisha dhana, kuemaresha umoja wa Waisalmu wa elimu, na kutoa mwito wa elimu na kutumia akili.

 

Makala imeandaliwa na Kitengo cha lugha ya Kihispania

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.