Kusambaratika kwa familia chanzo cha kuwashawishi vijana kujiunga na makuhndi ya kigaidi

  • | Monday, 14 April, 2025
Kusambaratika kwa familia chanzo cha kuwashawishi vijana kujiunga na makuhndi ya kigaidi

 

Jamii za kisasa zimeshuhudia mabadiliko makubwa katika muundo wa familia hivi majuzi, hali ya mgawanyiko wa familia imezidi kuwa mbaya zaidi, jambo lililosababisha athari mbaya kwa nyanja mbalimbali za maisha ya kijamii na kisaikolojia ya watu. Wakati huo huo, kuenea kwa fikra za itikadi kali miongoni mwa vijana kumekuwa suala la kimataifa lenye hatari kubwa.

Ufafanuzi wa mgawanyiko wa familia

Dhana ya mgawanyiko wa familia ni kutengana kwa familia kupitia kuvunjika au kuzorota kwa mahusiano ya familia, na kusababisha kupungua kwa utulivu wa kisaikolojia na kihisia wa wanafamilia. mgawanyiko wa familia kunatokea kwa sababu kadhaa, kama vile talaka, kufiwa wazazi au mojawapo ya wazazi, au mivutano inayoendelea ndani ya familia ambayo husababisha kukosekana kwa mawasiliano na maelewano kati ya wana wa familia wake.

Dhana ya fikra kali

 Fikra kali ni tabia ya kuchukua mawazo mkali, ambayo hayawezekani kubadilika au kujadiliana, fikra kali hii mara nyingi inatokana na hali ya kupinga au kukataa hali ya sasa.

Uhusiano kati ya mgawanyiko wa familia na kukubali kwa vijana fikra kali

Kuna njia nyingi za kuchukua fikra kali kwa sababu ya kuwepo mgawanyiko wa familia. Hapa kuna baadhi ya mambo muhimu yanayochangia jambo hilo:

A. Utupu wa kihisia na kisaikolojia: Vijana katika familia zilizotengana hukosa usaidizi wa kihisia na wa kimwili unaohitajika, jambo ambalo huongeza hisia zao za upweke na utupu wa ndani.

 

B. Ukosefu wa mwongozo wa familia: Familia ni chanzo cha kwanza ambacho kijana hujifunza maadili na kanuni zinazoongoza tabia na mwelekeo wake katika maisha. Lakini katika familia zilizotengana, vijana wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa mwongozo na ushauri, jambo ambalo hudhoofisha uwezo wao wa kuchukua maamuzi mazuri na yenye msingi.

C. Kuhisi kwa upweke na kutengwa: Vijana katika familia zilizotengana hupata hisia kuu za upweke na kutengwa, kukosa vifungo vya kihisia vinavyowaunganisha kwa wanafamilia wao.

D. Kukabiliana na ubaguzi wa rangi: Wakati mwingine, vijana hukabiliana na changamoto kubwa katika mazingira yao ya kijamii, kama vile ubaguzi wa rangi au kidini, jambo ambalo huzalisha hisia za hasira na ukosefu wa haki.

Athari za vyombo vya habari na teknolojia katika kukuza fikra kali

Katika zama zetu hizi, vyombo vya habari na teknolojia vimekuwa miongoni mwa mambo mashuhuri yanayochangia kuenea kwa mawazo yenye fikra kali miongoni mwa vijana. Mtandao, na hasa majukwaa ya mitandao ya kijamii, huyapa makundi yenye fikra kali fursa ya kuwasiliana moja kwa moja na vijana na kuwashawishi kupitia jumbe zinazotumwa kwa haraka na kwa njia zisizo za moja kwa moja.

Makundi yenye fikra kali pia hutumia teknolojia ya kisasa kudhibiti hisia za vijana kwa kuwasilisha maudhui ambayo yanaimarisha hisia zao hasi kuelekea jamii na kuchochea hisia zao za upweke na kutengwa.

Vipimo vya kisaikolojia na kijamii vilivyowajaalia vijana wanakubali fikra kali

Kukubali mawazo yenye fikra kali kuna athari kubwa kwa wasifu wa kisaikolojia wa vijana; kwani jambo hilo huongeza hisia za uchokozi na hasira, na kuwafanya wao wakubali zaidi mawazo yanayochochea vurugu, jambo ambalo hupanda mioyoni mwao hisia za uhasama dhidi ya wengine. Fikra kali pia inachangia kukuza hisia zao za kutengwa na jamii, na kuchukua mwelekeo wa kujiondoa kutoka kwa jamii pana na kugeukia makundi yaliyofungwa ambayo yanashiriki nao mawazo yenyewe yeneye fikra kali.

Suluhu na uzuiaji wa fikra kali kati ya vijana

Ili kukabiliana na athari za mgawanyiko wa familia kuhusu kukubali mawazo yenye fikra kali kati ya vijana, seti ya suluhu za kuzuia zinaweza kutekelezwa ambazo huchangia katika kuandaa mazingira salama na yenye afya kwao:

A. Kuimarisha jukumu la familia katika malezi ya kijamii: Wazazi lazima watambue kikamilifu umuhimu wa jukumu lao katika kujenga familia yenye nguvu na utulivu ambayo huwapa watoto wao mazingira ya kihisia na salama.

 B. Elimu na ufahamu: Ni muhimu kwamba taasisi za elimu zichukue jukumu la kuwaelimisha vijana kuhusu hatari za fikra kali kupitia programu za elimu zinazokuza maadili ya ubinadamu na uraia bora.

C. Kutumia teknolojia ili kueneza mawazo ya wastani: Mitandao ya kijamii na teknolojia ya kisasa inaweza kutumika ili kueneza maadili ya uvumilivu na kuishi pamoja kwa amani, na kuwatambulisha vijana kwa maadili nzuri za kibinadamu.

Mwishoni, inaweza kusemwa kwamba mgawanyiko wa familia ni moja ya sababu kuu zinazosukuma vijana kuchukua na kukubali mawazo ya fikra kali. Mgawanyiko huu unawafanya wao wanakubali mambo ya nje ambayo huahidi kwa kuleta suluhisho la haraka kwa shida zao za kisaikolojia na kijamii.

Kwa kukosekana kwa usaidizi wa kihisia na utulivu wa familia, vijana hupotea na wanatafuta chanzo chochote ambacho kitawapa hisia ya kukubalika.

Ili kuzuia jambo hili, jamii kwa ujumla inapaswa kufanya kazi ili kuimarisha utulivu wa familia na kutoa msaada muhimu wa kisaikolojia na kijamii kwa vijana katika familia zilizogawanyika, ili wasiingie kwenye fikra kali. Jukumu la taasisi za elimu na asasi za kiraia ni muhimu vile vile katika kuwaongoza vijana kuelekea maadili ya wastani, kupitia programu zinazowaongoza kuelekea njia nzuri za kufikiri zinazoimarisha mshikamano wao wa kijamii na kuwalinda dhidi ya kutumbukia kwenye fikra kali.

 

Makala imeandaliwa na kitengo cha lugha ya Kichina

Imefasiriwa na Bw., Eslam Ragab Mohammed

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.