Hotuba ya Imamu Mkuu kwenye Mkutano wa "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa Ni nani ", Grozny, Chechan

  • | Sunday, 28 August, 2016
Hotuba ya Imamu Mkuu kwenye Mkutano wa  "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa Ni nani ",  Grozny, Chechan

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Shukrani zote ndizo za Mwenyezi Mungu, Mola wa Malimwengu kote, Swala, Salamu na Baraka zote zimfikie Bwana wetu Mtume Mohammad (S.A.W.) pamoja na jamaa na maswahaba wake wote  
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Chechan Bw; Ramadhani Ahmado Vitch Qadirouf
Enyi hadhira watukufu!
Assalamu Alykum Warahamtul lahi Wabarakatu
Imepokelewa kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kwamba alisema: "Ye yote asiyewashukuru watu – kwa mazuri wao waliyomfanyia – hatoi shukrani Anazozistahiki Mwenyezi Mungu", pia alisema: "….ye yote atakayekufanyia mazuri, basi mmlipizeni sawa sawa, mkikosa, basi mwombeni Mwenyezi Mungu ampe thawabu mpaka aridhike".
Kwa kweli wananchi wa Chechan walifanya jambo lililo zuri zaidi wakati wa kupokea ujumbe wa Al-Azhar Al-Shareif jana, ambapo wengi wao wakiongozwa na Rais wa Chechan Bw; Ramadhani Ahmado Vitch Qadirouf walitoka kupokea Al-Azhar Al-Shareif kwenye uwanja wa ndege mjini Grozny, jambo linalozingatiwa karamu kubwa mno inayoashiria shime na heshimu ya wachechan kwa Al-Azhar, maulamaa wake na masheikhi wake. Kwa hakika mapokezi mema kama hayo mliyoyatoa kwetu yanaashiria uzuri wa wananchi wa Chechan, ambao ndio mfano wa kuigwa katika kulazimika kwa mafunzo ya dini sahihi, na kushikamana pamoja kwa ajili ya kuilinda nchi na itikadi yao.
Basi, naelezea shukrani kubwa kwako Ewe Mheshimiwa Rais wa Chechan! Na wananchi watukufu na nchi iliyo nzuri zaidi….kwa hakika sisi hatuwezi kulipiza mazuri haya mliyoyafanya nasi isipokuwa kwa maombezi (Dua) kwa Mwenyezi Mungu (S.W.) Awape wachechan neema zote za kubainika na kisichobainika, na Aifanye nchi hiyo ndiyo nchi ya amani, maendeleo na mafanikio, kwa kweli wengi wa wananchi wenu hulazimika kwa haki na uadilifu.
Vile vile, mkutano huo ambao tunasikia furaha kwa kushiriki katika matukio yake, ndio jambo jingine linalostahiki kushukuriwa kwani Chechan inawafanyia waislamu wote duniani mema kwa kupanga mkutano kama huo, na huchangia vizuri sana kuzima moto ya vita visivyohusiana na ubinadamu, kwa hakika vita hivyo vimesababisha umwagaji damu za waarabu na waislamu kwa wingi, kwa msaada wa mifumo mipya ya kikoloni, ambayo inatoa mitazamo ya kishetani pamoja na kuchocheza vita hivyo, mitazamo hiyo ni kama vile; ulazima wa kuwepo mgongano baina ya staarabu, kumalizika kwa historia, ghasia ambayo haipelekei ila ghasia nyingine iliyo sawa au kubwa zaidi, na utandawazi ambayo humaanisha: "udhibiti wa nchi moja tu ndiyo hudhibiti ulimwengu kote kijeshi, kisiasa na kiuchumi".
  Isitoshe, bali mipango na mikakati mibaya hiyo haikuhusika kwa ukiukaji wa kijeshi na wa kiuchumi tu, bali imefika kuharibu ubinadamu wenyewe, walau mikakati hiyo ingalitosheleka kwa kujiingiza katika mambo ya kujeshi na ya kiuchumi tu, basi tungalivumilia na stahmali, kama alivyosema Torfah Bin Al-Abd:
أبا مُنْذِرٍ أفْنَيْتَ فاسْتَبْقِ بَعْضَنَا * حَنَانَيْكَ بَعْضُ الشَّرِّأهْوَنُ من بَعْضِ
Kwa hakika mikakati hiyo mibaya ikasababisha madhara kwa tamaduni za watu, itikadi zao na mapato yao ya kihistoria na kitamaduni, ambapo imewalazimisha kufuata vipimo mahsusui vya kitamaduni vya kimataifa..kwa ajili ya kufanya hivyo, utandawazi ulichukua hatua zinazotahadharisha kukaribia hatari ya kikweli, ambayo ni kusababisha kuenea umaskini katika maeneo ya mashariki, na kuweka vikwazo vinavyozuia kuendelea kwake, na kupitisha udhibiti juu ya mifumo ya utawala wake, kupitia kwa mashirika ya kimataifa, mabenki, mikopa dhalimu, mikutano yanayohusiana na Hali ya Hewa au Wakaazi au Mwanamke na Mtoto, na kubashiri kwa maradhi na majangwa mengi, na kueneza ghasia isiyo na sababu, kwa kutumia pesa nyingi sana ambazo hazitumiwi kuwalisha wenye nja nchini humo, au kuwasaidia wananchi wake kupata haki zao katika mafundisho, afya, chakula, kupambana na maradhi na ujinga na ujahili.
  Wengine wangeweza kuuliza uhusiano gani uliopo baina ya mkutano huu na hali ya kusikitisha ya ummah wetu hivi karibuni?
Ili kujibu swali hilo twakumbusha kwamba mkutano huo katika kuchunguza kuhusu: "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa ni nani hasa?" utajadili wakati huo huo kuainisha maradhi iliyoupata umma, ikaudhoofisha, na ikaufanya upatwe na mashaka mengi mno…kisha mkutano huo ni kwa kutafuta njia ya kupata staafu kwa maradhi zilizoupata ummah wetu, nataraji kwamba tafiti za maulamaa wanaoshiriki zitatoa ufumbuzi wa matatizo hayo.     
Mnaweza kuniunga mkono – Enyi Maulamaa waheshimiwa! – kwamba dhana ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ilikuwa katika enzi nzuri zaidi za kielimu na kistaarabu za Ummah huu ndiyo chanzo cha kuwaelekeza maulamaa na maimamu wake, katika kila wanayoyatolea kuhusu itikadi, Fatwa za Fiqhi na utungaji sheria, pia dhana hiyo iliweza kuulinda umma kutoka kutofautiana na kuhitalifiana, ikiwakumbusha wakati wote kwa kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): "Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka" Al-Imran: 103, na kauli yake (S.W.): "Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri" Al-Anfaal: 46.
La kusikitisha sana kuwa dhana hiyo ambayo ilikuwa ndiyo nguzo muhimu ya nguvu ya umma kwa karne kadhaa – ilichafushwa mwishoni kwa madai namatakwa, yaliyojionyesha kama ni kweli kimaumbile, yakapoteza misingi na vyanzo vyake na sifa zake halisi kimaumbile na kimaudhui, mpaka ikawa dhana hiyo – ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ndiyo dhana isiyo imara kwa waislamu wa kawaida, bali kwa walinginiaji pia, haibainiki baadhi ya maana zake za kikweli ila yakajitokeza maongezi mpaka ikawa mada ya kugombana baina ya makundi mbali mbali, yanayojidai kuwa wao ndio wafuasi wa madhehebu ya Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa, wakidai kwamba wao peke yao wenye haki ya kuwakilisha madhehebu hiyo…jambo lililopelekea kugawanywa kwa waislamu kwenye makundi tofauti kwa kugawanyika dhana hiyo bongoni mwa aghalabu ya  watu, wakiwemo wanaojihusisha na ulinginiaji na mafudisho, yakaja matokeo ya hali hii ambyo ni kuwa na misimamo mikali na mawazo makali, ugaidi, jinai za mauaji, umwagaji damu na ubakaji, hayo yote hufanywa kwa jina la Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa, kwa uongo juu ya watu na kutojali kwa waliyoyatolea maulamaa wetu kipindi cha karne kadhaa kati ya ishara bainifu, na dhana zinazolengea kutoa taarifa kubainisha Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa ni nani?
    Vile vile, la kusikitisha kwamba kubadilika badilika kwa dhana hiyo hata kwa wafuasi wa madhehebu wenyewe, jambo lililowapa wengine nafasi ya kuichafusha dhana hiyo, na kudai kwamba Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa ndio wanaohusika na jinai za kigaidi zinazofanywa na makundi ya kitakfiri yenye silaha….na wale wadai ndio wa kwanza kutambua kwamba makundi ya kitakfiri hayo kwa vitendo vyake vya kikatili hayana uhusiano wo wote kwa "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa"…inadhaniwa kwamba kundi hilo lilitumia dhana ya Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa ili kutekeleza miradi na mikakati ya kisiasa na mafanikio ya kimadhehebu na matumaini ya kueneza sababu ya kutofautiana baina ya waislamu, na kuchochesha fitina zilizozuiliwa tangu zamani, na kueneza fikira za chuki na uhasidi, na kukana mafunzo ya Uislamu kuhusu kuishi pamoja kwa amani na kutoruhusu kuingia katika masuala ya mataifa na nchi mbali mbali, na kuzingatia haki za jirani ambazo zilifikia katika sheria ya kiislamu kuwa sawa na haki za ndugu na kurithishana.
Enyi waheshimiwa! Na hali iliyotokea hapo zamani ni ile ile inayotokea siku hizi, ambapo ummah wa kiislamu unahitaji sana kutambua upya Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa ni nani hasa? Na nini misingi ya madhehebu yao? Na je, athari gani za kutokuwepo kwa madhehebu yao maishani mwa waislamu? Na nini sababu za kikweli za kutofautiana kwa waislamu? Na je, kuna njia ya kuhuisha madhehebu ili kuuokoa umma, kwa ajili ya kuleta mshikimano katika matatizo yake yanayofululiza, na kutowapa maadui nafasi ya kutekeleza mikakati yao mibaya kwa umma? Maswali hayo na mengine, nataraji kupata majibu yake mwishoni mwa mkutano huo.
Ama kuhusu jibu langu juu ya swali la: Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa ni nani? Basi nimelichukua kutoka mtalaa mmojawapo mitalaa ya Al-Azhar, ambayo nililelewa kwa mujibu wa mafunzo wake, nikauhifadhi tangu utotoni mwangu mpaka siku yetu hii…nikazisoma matini za mbinu hiyo na vitabu vya kuzisherehesha kwa muda wa miaka 25, nikiliwaza sana mbinu yake ya kutegemea mazungumzo baina ya matini na maelezo yake na maongezi, wakati wa kufundisha elimu za Usuul-Ddin, kwa muda wa miaka 20 takriban…ambapo nimejifunza kutoka kitabu cha "Sharhul-Kharida" cha Abul-Barakat Al-Dardiir katika marahala ya mafunzo ya kimsingi ambapo nimetambua kuwa "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ndio Wa-Asha'ariyya na Matridiyya, ili kuwaainisha mbali na makundi mengine ya kiislamu, kisha nikajifunza katika marahala ya kisekondari kwamba wakweli miongoni mwa makundi ya kiislamu ndio "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa", na kwamba istilahi hiyo huitwa kwa wale wafuasi wa Imamu wa "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ambaye ni Abul-Hasan Al-Asha'ariy, na wafuasi wa Imamu wa uongofu Abu Mansour Al-Matridiy.
 Kisha tukajifunza katika tafiti zetu za masomo ya juu kwamba "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ndio Wa-Asha'ariyya na Matridiyya, na watu wa Hadithi, na kwamba wanafiqhi wa madhehebu ya Hanafiy, Malik, Shaafi'iy na walioongoka kutoka wanafiqhi wa Hanbal, hawa wote hawakujiweka mbali na madhehebu hiyo ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa", kama alivyosema mwanachuoni bingwa zaidi Ezz Bin Abdul-Salam (aliyekufa mwaka 660 H.J.): hiyo ndiyo dhana inayojumlisha maulamaa wa waislamu na maimamu wao, miongoni mwa wenye elimu ya Mantiki, Fiqhi, Hadithi, Sufia na Uongofu, Sarufi na Lugha, iliyopitishwa na Wa-Asha'ariyya wa kale wenyewe mwanzoni kabisa wa kujitokeza kwa istilahi hiyo baada ya kufa kwa Imamu Al-Asha'ariy (aliyekufa mwaka 334 H.J.), hasa kwa Imamu mkubwa zaidi wa elimu ya Mantiki Abu Mansour Abdul-Qahir Al-Bughdadiy (aliyekufa mwaka 429 H.J.) katika vitabu vyake vya "Al-Farq baina ya Al-Firaq" Tofauti baina ya Makundi na Usuul-Ddin, kisha vikaja vitabu vingine vingi vya kubainisha "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" kama vile kitabu cha Abi Al-Mudhaffar Al-Isfraiiny (aliyekufa mwaka 471 H.J.) katika kitabu chake cha "At-Tabsiir Fi Ddin" na wengine wengi.
Lakini ni nani Al-Asha'ariy aliyeitwa lakabu ya Imamu wa "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa"? Na nini madhehebu yake? Na kwa nini umma unaikubali madhehebu hiyo? Ingawa majaribio ya kuichafusha na kuwafanya watu waichukia, na kuishutumu kuwa Bidaa na ufisadi, na kuwatuhumia Wa-Asha'ariyya kuwa wafisadi na pengine kuwashutumu kuwa wametoka nje ya dini?
Kwa kujibu maswali kama hayo nimeleta vitabu vinne pamoja nami kutoka Misri kwa Anuani: "Imamu Abul-Hasan Al-Asha'ariy..Imamu wa Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" vinavyojumuisha tafiti za kongamano la Al-Azhar la kimataifa kuhusu Imamu huyo mtukufu.
Kwa hakika madhehebu ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" haikutosha kuulinda umoja wa waislamu kwa muda wa zaidi ya miaka elfu moja, wala haikuwa sababu ya kuendeleza utamaduni wao wa kidini na kifikira tu, bali ilikuwa sababu ya kuendeleza ustaarabu wa waislamu kwa upande wa kielimu na kimada katika nyanja zote maishani, Abu Mansour Al-Baghdadiy alitambua uhusiano uliopo baina ya maendeleo ya kimajengo na utulivu wa kiakili na kiroho wa waislamu, na vipi madhehebu ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" iliweza kuwa sababu ya kuleta maendeleo kwa umma na kwamba machapisho ya Ahlu-Sunnah kuhusu dini na dunia – kwa mujibu wa anayoyasema Abdul-Qahir Al-Bughdadiy – ni chanzo cha fahari kwa umma, na athari zao za kimajengo kwenye nchi mashuhuri za kiiskamu zingalibaki mbele ya watafiti, athari hizo ni kama vile; misikiti, shule, kasri, viwanda, hospitali, na majengo mengine mengi yaliyoanzishwa nchini mwa Sunnah.
Enyi Hadhira watukufu!
 Nataka kumaliza hotuba yangu hii kwa kutaja baadhi ya sifa hasa za madhehebu ya Asha'ariy ambayo ndiyo madhehebu ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa", zile sifa zilizoifanya madhehebu hiyo ibaki daima:
1-    La kwanza madhehebu hiyo siyo madhehebu mpya, bali ni madhehebu inayohusiana na imani za Wahenga Wema (Al-Salaf) kwa mujibu wa mbinu mpya inayokwenda sambamba na hali halisi ya mambo na kutokana na mambo mwafaka baina ya akili na matini, jambo lisilofanywa na wanaojilazimisha kwa matini tu pasipo na kuliwaza akili, na Mui'tazilah na makundi mbali mbali mengineyo, Imamu Tagu-Ddin Al-Sobky anasema:


"Kwa hakika Al-Asha'ariy hakukubuni rai wala hakuianzisha madhehebu, bali alikwenda bega kwa began a madhehebu za  Al-Salaf, akitetea Sunnah za Mtume (S.A.W.) ama kuhusu kuinasabisha madhehebu kwake yaani; Al-Asa'ariy basi ni kwani ndiye aliyeshikamana kwa madhehebu kwa hoja thabiti, akawa Imamu wa madhehebu yenyewe na wafuasi wake wakaitwa Wa-asha'ariyya".
2-    La pili; kwani ndiyo madhehebu ya pekee ambayo haimkafirishi ye yote miongoni mwa waislamu, imepokelewa kutoka kwa Ibn Asaakir kwamba Al-Asha'ariy alipokaribia kufa mjini Baghdad alisema kwa mwanafunzi mmoja wake: "Uwe shahidi juu ya kwamba mimi simkafirishi ye yote miongoni mwa waislamu (Watu wa kuelekea Qibla hii), kwani wote wanamwabudu muabudiwa mmoja"
Na linalobainisha kukana kwa Al-Asha'ariy kwa mawazo ya ukafirishaji, na kutambua kwake matokeo ya kuenea mawazo hayo ambapo hupelekea kuhalalisha umwagaji damu, heshima, akatunga kitabu kinacozungumzia makundi ya kiislamu kwa anuani: "Maqalatul-Muslimiin na Ikhtilaaful-Muswallin" (Makala za waislamu na kutofautiana kwa wanaosali) akiashiria kwamba Uislamu unawajumuisha wote wanaoelekea Qibla katika Swala japokuwa kutofautiana kwao na kugawanyika katika makundi mbali mbali, kisha akataja ibara muhimu sana mwanzoni mwa kitabu kile, ile ibara ambayo waislamu wa siku hizi wanaihitaji sana kwa ajili ya kurejea kwa hali ya umoja na kuwa imara, alisema: "kwa hakika watu baada ya kufa kwa Mtume (S.A.W.) wametofautiana kuhusu mambo mengi, wengi wao wamewashawishi wengine, wakagawanyika katika makundi tofauti, lakini Uislamu hungaliwajumuisha wote"
  Jambo hilo alilolitaka Al-Asha'ariy kulihifadhi mwanzoni mwa kitabu chake ili afikishe ujumbe fulani kwa wanafunzi wake kutilia mkazo ukweli alioutaja mwanzoni mwa kitabu chake.    
   Enyi ndugu waheshimiwa! Kwa kweli ukafirishaji ndio sababu kubwa zaidi ya kumwaga damu za watu na kisingizio kikuu cha kuanza mapigano na wasio na hatia kwa kudai kupigana na makafiri, tukitazama ulimwengu wa kisasa tutagundua kwamba madhehebu ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ni madhehebu ya pekee kutowakafirisha watu sawa waislamu au wasio waislamu au kuwashutumu kuwa wahalifu wa sheria au wenye Bida'a hata wakiwa na mawazo tofauti na madhehebu yenyewe.
Kwa hakika "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ndio waislamu wote, na maimamu wao ni Malik, Al-Shafiiy, Abu Hanifa, Ibnu Hanbal, Al-asha'ariy, Al-Matridiy, wanafunzi wao na wasomi wao, na Al-Hasan Al-Basriy, Al-Jonied, Al-Muhaasibiy, Al-Sarraaj, Al-Ghazaliy, na wanavyuoni wa hadithi na wakuu wa madhehebu ya Hanabila wanaoshikamana na mbinu ya Imamu Ahmad na srea zake ambapo alikuwa hujiweka mbali na kuwashutumu waislamu kwa ufisadi au kuwatuhumu kuwa wametoka nje ya dini na kuzihalalisha damu zao.
 Na madhehebu ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ndiyo madhehebu aliyoiusia nayo Mtume (S.A.W.) kwa kuwaelekeza waisalmu washikamane nayo hasa jamii ya kiislamu ikipatwa na matatizo na mabadiliko na fitina, Mtume (S.A.W.) alisema: "Mshikamane Jamaa, Tahadharishe na kutofautiana, kwa kweli Shetani hushawishi anajiweka mbali na Jamaa, lakini wawili huwa mbali nao, anayetaka kuingia peponi basi ajishikamane na Jamaa".
Enyi hadhira waheshimiwa!
Najua kwamba nimechukua wakati mrefu nikitoa hotuba yangu hii, lakini nina sababu ya kufanya hivyo nalo ni hali mbaya ya umma wetu siku hizi, hali tusiyoitaka kuendelea, tukabidi kutosema maneno matupu ya kuzingatia hisia tu, ambapo hatulengei ila kuwajumisha waislamu katika safu moja, na kuzisafisha akili na nyoyo kutoka mawazo mabaya yanayokanwa kabisa na Uislamu na sheria yake, tunapaswa kutambua vyema kwamba hali ya umma wetu haitarekebishwa ila kwa kurudia misingi thabiti na kulazimika madhehebu ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ambapo ndiyo madhehebu iliyo nyepesi na yenye msamaha zaidi.
  Namaliza hotuba yangu kwa mwito kwa kila wanaojihusisha na madhehebu hiyo wakapotea njia yake iliyonyooka twawataka watubu na wafikkirie upya kuhusu jinai wanazozifanya kwa jina la madhehebu ilhali madhehebu yenyewe haihusiani kamwe na jinai zao hizo, wanapaswa kutafkuri yale maelezo makosa wanayoyatoa ambayo hayatawanufaisha mbele ya Mwenyezi Mungu (S.W.) Siku ya Kiyama, watambue kwamba wataulizwa kuhusu damu zinazomwagwa na ufisadi unaofanywa kutokana na maelezo yao hayo, wajue pia kuwa wana nafasi ya kutubu baada ya kusoma upya Qur-ani waifahamu ipasavyo kwa akili na moyo, na kuliwaza maana na mafuzo yaliyokuja ndani ya aya zake, wakiongoka kwa Sunnah za Mtume (S.A.W.) aliyetumwa ili awe rehema kwa walimwengu wote.
  Na wito yangu kwenu –Enyi wachechan – walio imara na kwa waislamu wote wa Russia kuendelea kushikamana madhehebu ya "Ahlu-Sunnah na Al-Jamaa" ambayo ni madhehbu ya Wa-Asha'ariya na Maturidiya na watu wa Hadithi na Sufia wenye matendo mema, mishikamane vizuri wafundisheni wana wenu madhehebu hiyo mkiifanya ni mojawapo mitalaa ya kufundishwa shuleni na vyuoni, mkitoa hoja na dalili thabiti za kubatilisha madai yo yote kuishutumu madhehebu yenyewe kwa kutumia Bida'a au kwa kutoa wito mbaya za kuichafusha madhehebu, zile wito zisizopelekea ila uharibifu, umwagaji damu na chuki kwa waislamu na Uislamu kwa pamoja.    
   
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Assalamu Alykum Warahamtul lahi Wabarakatu
Imeandikwa katika
Al-Azhar Al-Shreif
Mwezi wa Dul-Ke'da 1437 H.J.            Agosti 2016 B.K.
Ahmad Al-Tayib
Sheikhi mkuu wa Al-Azhar

 

Print
Tags:
Rate this article:
1.0

Please login or register to post comments.