Al-Azhar yalaani mashambulizi mawili ya kigaidi mjini Kabul

  • | Tuesday, 6 September, 2016
Al-Azhar yalaani mashambulizi mawili ya kigaidi mjini Kabul

Al-Azhar Al-Sharif yalaani mashambulizi mawili ya kigaidi, ambayo yalitokea karibu na Wizara ya Ulinzi katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul, leo Jumatatu, yaliyosababisha kuwaua 24 na kujeruhi zaidi ya 90 wengineo
Al-Azhar Al-Sharif yasisitiza kuwa vitendo hivyo vya kigaidi ni kinyume na mafundisho mawazi ya Uislamu na kinyume na mila zote za Mungu na kanuni za binadamu ambazo zinakataa aina zote za vurugu na ugaidi, ikizingatia kwamba vitendo hivyo ni aina ya ufisadi katika ulimwengu, ambayo inaweza kusababisha hizaya duniani, na adhabu kali katika Akhera.
Wakati Al-Azhar Al-Sharif yalaani vitendo vibaya hivyo vya kigaidi, basi yarudia wito wake kwa udharura wa kupanga na kuunga mkono ili kupambana na ugaidi, na kufanya juhudi zaidi ili kupunguza vurugu na kumwaga damu kwa watu wasio na hatia.
Al-Azhar Al-Sharif yarambirambi Serikali na watu wa Afghanistan, ikiomba Mwenyezi Mungu azipe familia za wahanga uvumilivu na ujasiri, na kupona kwa haraka waliojuruhiwa.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.