Al-Azhar yalaani shambulizi la kigaidi lililolengea msikiti mmoja nchini Pakistan

  • | Sunday, 18 September, 2016
Al-Azhar yalaani shambulizi la kigaidi lililolengea msikiti mmoja nchini Pakistan

Al-Azhar Al-Sharif imelaani kikali lile shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na mgaidi wa kujitoa mhanga kwenye msikiti mmoja katika eneo la kikabila nchini Pakistan karibu na mipaka na Afghanistan kipindi cha Swala ya Ijumaa jambo lililopelekea kuauwa watu 25 na kujeruhiwa wengineo.
Al-Azhar Al-Shareif inasisitiza kuwa ina msimamo thabiti wa kukataa kabisa namna zote za vurugu na ugaidi zisizo na uhusiano wo wote na Uislamu, wala hazipambanui baina ya mtu na mwingine kwa mujibu wa dini yake, au uraia wake wala hazitofautishi baina ya mahali pa kufanya ibada au pengine, ikisisitiza kwamba ugaidi haufungamani kamwe na dini wala uraia, na kwamba Mwenyezi Mungu Ameandaa adhabu kali mno kwa yule anayehusika kutekeleza uvamizi kama huo dhidi ya mahali pa kufanya ibada.
Al-Azhar Al-Shareif wakati wa kukana shambulizi hilo la kigaidi, inatoa tena wito ya kutambua udharura wa kushikamana na kushirikiana kwa ajili ya kupambana na ugaidi, na kufanya juhudi zilizo kubwa zaidi ili kuzuia kuenea kwa vurugu na umwagaji damu za wasio na hatia, wakati huo huo inatoa rambi rambi kwa Pakistan serikali na raia, ikimwombea Mwenyezi Mungu (S.W.) awape familia za wahanga subira njema na awapona waliojeruhiwa kwa haraka.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.