Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif katika Sikuu kuu ya Amani duniani

  • | Thursday, 22 September, 2016
Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif  katika Sikuu kuu ya Amani duniani

Ulimwengu hushereheka kila mwaka tarehe ishirini na moja mwezi wa Septemba kwa sikuu kuu ya amani ili kuimarisha maadili ya amani na usalama miongoni mwa mataifa mbali mbali.
Kwa kweli siku hiyo imekuja mwaka huu ilhali mataifa kadhaa wamekosa kabisa maana ya amani na usalama kwa sababu ya vita vilivyozuka na mizozo iliyoenea, wakati huo huo mataifa wengine waliuawa kwa magonjwa, ujinga na umaskini, na kundi la tatu wakawa wanajaribu kujiepuka na hatima ya walioangamizwa na wanajikuta katika hali ya kusita sita baina ya kuwasidia wale wahanga wa vita na mizozo au kujiweka mbali ili kujiokoa kutoka hatima yao, kuna wachache wanaofaidika kwa hali hiyo ambapo wanajifurahisha kwa kuzinyonya damu za wasio na hatia na kusikia mayowe ya wanaopatwa na adhabu na waliohuzunika kwa kukosa jamaa zao.
   Al-Azhar Al-Shareif wakati wa kusisitiza utashi wake wa kuendelea juhudi zake za kueneza amani na usalama na kusameheana ulimwenguni wote, basi inataka kwa mnasaba hiyo kutoa wito kwa ulimwengu wote ukiongozwa na nchi kubwa zaidi, mashirika makubwa zaidi ya kijimbo na ya kimataifa, bodi ya kidini na yanayohusiana na masuala ya kibinadamu na ya kijamii, wito ya kufanya juhudi za kuimarisha amnai na usalama, na kushirikiana pamoja kwa ajili ya kupambana na mawazo makali na ugaidi, na kufanya juhudi zaidi ili kumaliza majanga ya umaskini, ujinga na  ugonjwa, vile vile Al-Azhar Al-Shareif inasisitiza kuwa iko tayari kushirikiana na wito wo wote kwa lengo la kuhakikisha kheri kwa wanadamu wote, ikitamani usalama na amani zistawi ulimwengu wote.

 

Print
Tags:
Rate this article:
3.0

Please login or register to post comments.