Mazungumzo yanamaanisha mawasiliano ya moja kwa moja kwa lengo la kufikia dhamira maalumu, kwa hiyo mazungumzo yanaasisiwa vidhibiti maalumu na elementi mahususi kama vile washiriki wa mazungumzo, mada na mawazo ya mazungumzo, zana za mazungumzo, malengo ya mazungumzo n.k.
Aghalabu ya mazungumzo yanakusudia kubainisha kweli na kuthibitisha maelezo fulani au kurahisisha maambatano na kufahamiana baina ya washriki wa mazungumzo yenyewe. Kwa kuwa mwanadamu hayupo peke yake katika dunia bali anashirikiana na wanadamu wengine na hata viumbe vingine wanaoishi katika ulimwengu mmoja pamoja na mwanadamu, mazungumzo yakawa dharura na zoezi la kimaumbile hasa wakati amabpo maudhui na jambo la kushughulikiwa likuwepo.
Pia, mazungumzo yalianza kuanzia mwanzo wa kumwumba mwanadamu kwa ajili ya kuanzisha misingi ya mazungumzo na adabu zake, mazungumzo ya kwanza yalikuwa biana ya Mwenyezi Mungu na Malaika watukufu kuhusu kumwumba Adam, mazungumzo yaiyotajwa kwatika kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua * Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli * Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima} [2/29-31].
Kwa urefu zaidi, mazungumzo yanalengea kufikia mambo ya pamoja baina ya walio tofauti kwa ajili ya kudumuisha hali ya utulivu na kuishi pamoja kwa amani na usalama, kwani Uislamu haukuja ili uzikata kata husiano zilizopo baina ya watu, bali kuziimarisha na kuzikuza. Mwenyezi Mungu Anasema: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbenikutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutokanafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili haowanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na MwenyeziMungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni} [4/1], aidha Alisema (S.W.): {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana namwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa nimataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliyemchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu niMwenye kujua, Mwenye khabari} [49/13]
Hivyo, tunatambua kuwa aya hizo zimewakumbusha watu kwa asili yao moja na kuwahimiza kuchunga asili hiyo tu bila ya kujali tofauti yoyote nyingine. Na ikiwa hali ya kuwaumba watu na viumbe vyote katika sura mbalimbali na maumbili tofauti ni sunna na majaliwa yaliyopitishwa na Mungu basi kwa sababu gani baadhi ya watu wanachukua tofauti kama hizi sababu na misingi ya kugombana na kuzozana?! Mwenyezi Mungu Amepitisha ukweli huu katika kauli yake: {Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watuwote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana} [11/118].
Kinyume na wanayoyadai wapotofu wale, Mwenyezi Mungu Amewakataza waislamu kufanya uadui wowote kwa kisingizio chochote: {Enyi mlio amini! Msivunje hishima ya alama ya Diniya Mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu, wala wanyamawanao pelekwa Makka kuchinjwa, wala vigwe vyao, wala wanao elekea kwendea Nyumba Takatifu, wakitafutafadhila na radhi za Mola wao Mlezi. Na mkisha tokaHija yenu basi windeni. Wala kuwachukia watu kwa kuwa wali- kuzuilieni kufika Msikiti mtakatifukusikupelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katikawema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi nauadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Munguni Mkali wa kuadhibu} [5/2].
Historia ya kiislamu imetuarifu kuwa mazungumzo yalikuwa ndiyo njia thabiti ambayo waislamu waliifuata kwa lengo la kufikia uelewa wa pamoja baina yao na wenzio kartika masuala mbalimbali ya dini na dunia, wakitambua ukweli wa kwamba kutofautiana ndiko matakwa ya Mungu kwa lengo la kukamilishana na kushirikiana kuimarisha ardhi siyo kwa kupigana na kuuana. Mazungumzo haya ya waislamu na wenzio wakati wote huwa yanategemea kuheshimiana na kusaidiana kupata manufaa na faida kwa wote.
Suluhu ya Al-Hudaibiya lilikuwa mfano bora wa mazungumzo ya waislamu na wasio waislamu, amabpo Mtume (S.A.W.) alizungumza na wakuu na wawakilishi wa washirikina kama vile; Urwa bin Masoud Al-Thakafiy na Mkuu wa wahabashi, jamabo lililowasukuma washirikina wa Qureish wakae pia na kuanza mazungumzo na Mtume mpaka wakaafikiana na Mtume juu azimio hilo la Al-Hudaibiya la kupitisha amani na kuzuia mapigano baina ya waislamu na mashirikina, japokuwa baadhi ya masharti ya suluhu hilo yalikuwa dhidi ya waislamu, lakini Mwenyezi Mungu Ameliita Fath Akisema: {Hakika tumekufungulia Ushindi wa dhaahiri* Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, naakuongoe katika Njia Iliyo Nyooka,* Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu* Yeye ndiye aliye teremsha utulivu katika nyoyo zaWaumini ili wazidi Imani juu ya Imani yao. Na MwenyeziMungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi, Mwenye hikima} [48/1-4]
Haya yanathibitisha kuwa Uislamu ndio dini ya Amani na Usalama kwa kutegemea mazungumzo mema, isitohe, bali Mtume baada ya hili azimio hilo lipitishwe kwa muda usio mrefu akaanza mazungumzo na mayahudi wa Khaybar kutukana na vita vilivyouka kwa sababu ya khiyana waliyoifanya mayahudi hawa.
Pia, misafara iliyokuwa inatumwa na Mtume (S.A.W.) ilikuwa inakwenda huku na huku kwa lengo la kuanzisha mazungumzo baina ya waislamu na wasio waislamu mfano wa; Wahabashi walikouwa wanaongowa na Al-Nagashiy na kubadilishana zawadi baina yake na Mtume.
Kwa hiyo, tunasisitiza kwamba Uislamu huhimiza sana mazungumzo yoyote yanayotekelezwa kwa ajili ya kuhakikisha amani na utulivu kwa mataifa yote duniani. Kwa hiyo, ulimwengu ukawa kama kijiji kidogo kila linalotukia huku huathira hapa n.k., tumebidi kuzingatia mazungumzo kama njia ya msingi ya kuelewana na kufikia masuluhisho ya kutosha kwa mizozo yoyote dunaini, tukisisitia kuwa mazungumzo haya yanatakiwa yaasisiwa kuheshimiana, kushirikiana na kuelewana kwa upole na mema kama tulivyoamrishwa na kuelekewa katika Qurani Takatifu na Sunna ya Mtume.