Mazungumzo katika Uislamu ni msingi mmoja wapo misingi ya kuwaita watu kwa njia ya Mwenyezi Mungu, ambapo mtindo wa kuzungumza na watu wote wanaokubali na wanaokataa ni mbinu ya msingi katika Daawa, tena kuwaheshimu watu wote na kusikliza maoni yao yanayostahili kusikilizwa japokuwa tofauti yoyote kati ya pande mbili. Pia, inaeleweka kuwa njia bora ya kuthibitisha ukweli wa maoni fulani ni kuznugumza na kujadiliana na maoni tofauti na kukinaisha watu kwa ukweli huo mpaka upande wa pili.
Aidha, tunatambua kwamba matatizo mengi ya enzi ya kisasa yanatokana na tabia ya kutosikilizana na sifa ya kila upande kushikilia msimamo wake bila ya kusikiliza maoni ya upande wa pili, jambo linalopelekea kuzuka migongano na migogoro mpaka mapigano na uharibifu mkubwa.
Kwa hakika mazungumzo yanalenga kimsingi kubainisha kweli wakati wa kutukia hitilafu kwa ajili ya kutatua shida iliyojitokeza. Qurani Takatifu ilipanga zoezi hili kwa masharti yanayowalazimisha washiriki katika mazungumzo haya, amabpo wanatakiwa kulazimika hikima na mawaidha mema na kufuata mtindo wa upole, Mwenyezi Mungu Anasema: {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwahikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namnailiyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walio ongoka} [16/125].
Pia, Mwenyezi Mungu Anasema: {Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njiailiyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumumiongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwakwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu naMungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake} [29/46]
Kwa urefu zaidi, mazungumzo yanalengea kufikia mambo ya pamoja baina ya walio tofauti kwa ajili ya kudumuisha hali ya utulivu na kuishi pamoja kwa amani na usalama, kwani Uislamu haukuja ili uzikata kata husiano zilizopo baina ya watu, bali kuziimarisha na kuzikuza. Mwenyezi Mungu Anasema: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbenikutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutokanafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili haowanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na MwenyeziMungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni} [4/1], aidha Alisema (S.W.): {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana namwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa nimataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliyemchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu niMwenye kujua, Mwenye khabari} [49/13]
Hivyo, tunatambua kuwa aya hizo zimewakumbusha watu kwa asili yao moja na kuwahimiza kuchunga asili hiyo tu bila ya kujali tofauti yoyote nyingine. Na ikiwa hali ya kuwaumba watu na viumbe vyote katika sura mbalimbali na maumbili tofauti ni sunna na majaliwa yaliyopitishwa na Mungu basi kwa sababu gani baadhi ya watu wanachukua tofauti kama hizi sababu na misingi ya kugombana na kuzozana?! Mwenyezi Mungu Amepitisha ukweli huu katika kauli yake: {Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watuwote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana} [11/118].
Kinyume na wanayoyadai wapotofu wale, Mwenyezi Mungu Amewakataza waislamu kufanya uadui wowote kwa kisingizio chochote: {Enyi mlio amini! Msivunje hishima ya alama ya Diniya Mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu, wala wanyamawanao pelekwa Makka kuchinjwa, wala vigwe vyao, wala wanao elekea kwendea Nyumba Takatifu, wakitafutafadhila na radhi za Mola wao Mlezi. Na mkisha tokaHija yenu basi windeni. Wala kuwachukia watu kwa kuwa wali- kuzuilieni kufika Msikiti mtakatifukusikupelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katikawema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi nauadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Munguni Mkali wa kuadhibu} [5/2].
Historia ya kiislamu imetuarifu kuwa mazungumzo yalikuwa ndiyo njia thabiti ambayo waislamu waliifuata kwa lengo la kufikia uelewa wa pamoja baina yao na wenzio kartika masuala mbalimbali ya dini na dunia, wakitambua ukweli wa kwamba kutofautiana ndiko matakwa ya Mungu kwa lengo la kukamilishana na kushirikiana kuimarisha ardhi siyo kwa kupigana na kuuana. Mazungumzo haya ya waislamu na wenzio wakati wote huwa yanategemea kuheshimiana na kusaidiana kupata manufaa na faida kwa wote.
Suluhu ya Al-Hudaibiya lilikuwa mfano bora wa mazungumzo ya waislamu na wasio waislamu, amabpo Mtume (S.A.W.) alizungumza na wakuu na wawakilishi wa washirikina kama vile; Urwa bin Masoud Al-Thakafiy na Mkuu wa wahabashi, jamabo lililowasukuma washirikina wa Qureish wakae pia na kuanza mazungumzo na Mtume mpaka wakaafikiana na Mtume juu azimio hilo la Al-Hudaibiya la kupitisha amani na kuzuia mapigano baina ya waislamu na mashirikina, japokuwa baadhi ya masharti ya suluhu hilo yalikuwa dhidi ya waislamu, lakini Mwenyezi Mungu Ameliita Fath Akisema: {Hakika tumekufungulia Ushindi wa dhaahiri* Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, naakuongoe katika Njia Iliyo Nyooka,* Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu* Yeye ndiye aliye teremsha utulivu katika nyoyo zaWaumini ili wazidi Imani juu ya Imani yao. Na MwenyeziMungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi, Mwenye hikima} [48/1-4]
Haya yanathibitisha kuwa Uislamu ndio dini ya Amani na Usalama kwa kutegemea mazungumzo mema, isitohe, bali Mtume baada ya hili azimio hilo lipitishwe kwa muda usio mrefu akaanza mazungumzo na mayahudi wa Khaybar kutukana na vita vilivyouka kwa sababu ya khiyana waliyoifanya mayahudi hawa.
Pia, misafara iliyokuwa inatumwa na Mtume (S.A.W.) ilikuwa inakwenda huku na huku kwa lengo la kuanzisha mazungumzo baina ya waislamu na wasio waislamu mfano wa; Wahabashi walikouwa wanaongowa na Al-Nagashiy na kubadilishana zawadi baina yake na Mtume.
Kwa hiyo, tunasisitiza kwamba Uislamu huhimiza sana mazungumzo yoyote yanayotekelezwa kwa ajili ya kuhakikisha amani na utulivu kwa mataifa yote duniani. Kwa hiyo, ulimwengu ukawa kama kijiji kidogo kila linalotukia huku huathira hapa n.k., tumebidi kuzingatia mazungumzo kama njia ya msingi ya kuelewana na kufikia masuluhisho ya kutosha kwa mizozo yoyote dunaini, tukisisitia kuwa mazungumzo haya yanatakiwa yaasisiwa kuheshimiana, kushirikiana na kuelewana kwa upole na mema kama tulivyoamrishwa na kuelekewa katika Qurani Takatifu na Sunna ya Mtume.