Hotuba ya Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wakuu wa Waislamu na Baraza la Makanisa la Kimataifa

mjini Geneva, 27 Sept., 2016

  • | Sunday, 2 October, 2016
Hotuba ya Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wakuu wa Waislamu na Baraza la Makanisa la Kimataifa

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Enyi waliohudhuria!
Mwanzoni kabisa mnipe ruhusa kutoa shukrani zote kwenu kwa kuniita kuhudhuria mkutano huu unaokuja katika hali mbaya tunayoishuhudia ulimwenguni wote siku hizi, pamoja na matatizo ya ukosefu wa maadili kwa wanadamu wote, mpaka maana za kupendana na kuishi kwa amnai zikawa nadra, ilhali maana za chuki, kujipendeleza na kugongana zikastawi na kuenea.
Sidhani kwamba nimepita la kawaida nikisema kwamba hakuna nchi hata moja ila inakosea amani na usalama wa kudumu na kujikomboa kutoka kwa vurugu na ugaidi.
La kusikitisha mno kwamba dini zilipata kutuhumiwa kwa kuhusiana na ugaidi huo. Kwa hakika wanaodai hayo wameghafilika kweli mbili kuhusu jambo hilo nazo ni:
La kwanza: kwamba dini zimekuja kwa ajili ya kuimarisha na kueneza amani baina ya watu, kuondoa dhuluma, na kuharamisha damu za wanadamu, inatosha kuwa dini ya Uislamu ambayo ninajiunga nayo, jina lake linatokana na amani, ikawa Uislamu, na kwamba amani kwa mujibu wa dini hiyo ni jina mojawapo majina ya Mwenyezi Mungu (S.W.) na kwamba miongoni mwa majina yake (S.W.) "Ar-Rahman, Ar-Rahim, Ar-Raouf, Al-Wadoud na Al-Latif" maana Yeye ndiye Mwenye kurehemu, Mwingi wa rehema na Mwenye upole, vile vile Mtume wa Uislamu (S.A.W.) ametambulisha na kuainisha sifa za mwislamu kwa kusema: "Mwislamu wa kweli ni yule hawaudhi watu kimatamashi wala kimatendo".
La pili ni kwamba ugaidi ambayo dini zinatuhumiwa kusaidia kuueneza na kukuza, ndio ugaidi usiotofautisha kati ya mwenye kulazimika kwa mafunzo ya dini na yule asiyetambua Mungu wo wote, wala hautofautishi baina ya mwislamu na asiye mwislamu.    
Na tukitazama ni nani hasa walio wengi wa wahanga wa ugaidi itabainika kwamba wengi wao ndio Waislamu wanaopotezwa na maisha au hupatwa na majeraha mabaya, siyo tu katika nchi za mashariki, ambapo ugaidi unazipiga nchi hizo kama vile nchi za Iraq, Pakistan, Lebanon, Misri na Libya, na ambapo Syria ambayo ina zaidi ya misikiti elfu imebomolewa hadi sasa, na kuuawa zaidi ya watu laki nne, bali huko Ulaya ambapo damu za Waislamu imemwagwa, sambamba na damu ya Wazungu kufuatia matukio ya kigaidi, japokuwa hayo lakini hasara kubwa zaidi waliyo nayo Waislamu ni – katika maoni yangu – kufungamanisha baina ya ugaidi huo na dini yao, na kuushutumu Uislamu peke yake kwa tuhuma hiyo miongoni mwa dini zote zingine, na kuradidi tuhuma hiyo mara kwa mara, jambo lililopelekea kukuza hisia za chuki ambazo zilipitishwa na watu wenye mrengo wa kulia mwenye msimamo mkali, ambao wamezitukana dini na kuita kwa kuzitenga na kuwakimbiza watu wake toka makazi yao na kufanya madhara kwa mahala pa ibada zao, basi watu wasio na hatia wakawa kati ya nyundo ya ugaidi na fuawe ya Islamuphopia (kuchukia na kuogopa na Uislamu).
 
Mabwana waliohudhuria!
Sitaki kuendelea katika kutetea dini dhidi ya tuhuma hiyo ya udhalimu, kwani mnajua vyema kuwa tuhuma hiyo ni dhalimu na ya mwongo, lakini nataka kusisitiza kwamba jukumu la dini zote kuhusu uimarishaji wa amani na kuieneza ardhini kote ni jukumu la kwanza na la msingi kwa dini, bali ni lengo lake lililo muhimu zaidi, ambapo iliteremshwa kwa ajili yake, hakuna dini yo yote ila imeharamisha ukiukaji wa damu ya mwanadamu, mali yake, na heshima yake, mimi sijui dini yo yote ya mbinguni imeruhusu umwagaji damu, au kunyang'anya haki, au kuwatishia watu wasio na hatia.
Kwa mujibu wa maoni yangu amani haitaenea wala watu hawataifurahia, kama taasisi za kidini na viongozi wake hazitakufanya kazi mkono kwa mkono kwa ajili ya kueneza amani.
Na mimi narudia rudia kwa masikio yenu yale yaliyoitwa na Al-Azhar tangu zaidi ya miaka sabini, katika miji mikuu ya magharibi hapa, kuwa ni lazima kwanza kuieneza amani baina ya watu wa dini wenyewe kwa wenyewe, na kati yao na wasomi, na wanao haki ya kupituisha hatima ya umma, kabla ya kuieneza baina ya watu wa kawaida.
 
Mabibi na Mabwana!
Kwa kweli, kulaani kule na kauli zilizotolewa na wafuasi wa dini dhidi ili kukana vitendo vya vurugu na ugaidi na hotuba za chuki hazijatosha, kwa sababu ni kitendo hakiji ila kwa matokeo dhaifu tu hayana athari halisi, lakini ni lazima kupanga pamoja  kwa ajili ya kupambana na vurugu, na kupitia mradi wa kimataifa unaoafikiana na hali halisi, kwa uongozi wa viongozi wa dini kupitia mikutano mingi ya kuangalia sababu za hali hiyo na kutambua fumbuzi zilizo muhimu zaidi zilizopendekezwa ili kukabiliana nayo kiakili, kelimu, kijamii, kimalezi na kitekelezi.
La kumbukwa hapa kwamba Al-Azhar imeingiza somo jipya katika mitaala yake ya kielimu ili kuwafahamisha wanafunzi hatari za kuvuka mipaka na ugaidi, na kuwaepusha na kuvutwa na mawazo yo yote yanayoita kwa vurugu au kujiunga na makundi yenye kuinua bendera ya Uislamu, ilhali yanaichukua bendera hiyo ili kujificha nyuma yake na vitendo vyake vya kikatili na kutumia vurugu ya silaha.
Na kwa kwenda sambamba na hayo, dini hazina budi ila kulazimika kwa majukumu yake katika kuwaelimisha vijana wa ulimwengu kwa maadili kama vile; rehema na upole, kwa kuandaa makongamano makuu  ya kimataifa kwa vijana, yanayoshughulikia ufafanuzi wa dhana za kidini, hasa uimarishaji wa dhana ya uraia, inayomaanisha kutotofautisha baina ya mwananchi na mwingine kulingana na dini au ukabila, jambo ambalo ndilo ni msingi wa kuamini kwa uwingi (vitu vingi), uhuru, usawa, na kukubali mwengine na kuheshimu imani zake, na Mtume wa Uislamu - S.A.W – Ametekeleza dhana hizo akitangulia katiba za dunia alipoimarisha kanuni hizi katika mioyo ya wakazi wa Madina mara moja baada ya kuihamia ambapo akawaandikia kwamba "Waumini na Waislamu wa Quraish na watu wa Yathrib na Wayahudi, ni umma moja, na kwamba wayahudi wa Bani Awf ni umma pamoja na waumini, Wayahudi wana dini yao na Waislamu wana dini yao."
Hivyo Mtume – S.A.W – ameimarisha kanuni ya usawa baina ya raia Waislamu na wasio Waislamu, katika mfano wa nchi yake ya kwanza na akaitaja katika mkataba uliojulikana kwa «WATHIQA YA AL-MADINA».
Katika mnasaba huo, tunasisitiza kwamba kuamini kwa thamani ya kanuni hii kunaweza kuzikomboa nchi za Mashariki na za Magharibi kutoka matatizo mengi ya kidini na kijamii.
Sheria ya Kiislamu husisitiza daima kuwa Waislamu katika Mashariki ya Kiislamu wanapaswa kuwazingatia wenzao wanaofuata dini zingine ambao wanaishi pamoja nao ni wananchi wanaoshirikiana nao katika jukumu la kujenga nchi na kuitetea, na ilikuwa maarufu kwao kanuni ya kisheria "Wana haki sawa sawa nasi na wanapaswa wajibu sawa sawa nasi"
Vile vile, Al-Azhar Al-Sharief iliwaombea wananchi wa Kiislamu wanaoishi katika nchi za Magharibi kwa kujitambulisha kama ni sehemu ya jamii zao, wanaungana na kuingiliana na jamii, mwingiliano wa kufanikisha amani ya kijamii.
Hamna shaka kwamba viongozi wa dini wana roli muhimu haifai kuipuuza katika kuvunja vizuizi vya kisaikolojia vilivyojengwa na wenye kulingania vurugu, upweke, na chuki miongoni mwa wanaofuata imani tofauti, kupitia kusisitiza ukweli wa mambo mengi, la kuzingatia zaidi kati yake ni kwamba tofauti hiyo ni kwa hekima maalum ya Mwenyezi Mungu na matakwa yake, ambayo haiwezi kamwe kusababisha mapigano au upweke au vita, basi hii ni mkanganyiko kati ya uhuru wa uwingi (vitu vingi) na kunyang'anya haki hii.
Mwishoni mwa hotuba yangu natamani ilhali nimo hapa kati yenu kuongeza juhudi zetu kwa pamoja ili kukabiliana na hali mbaya zote na vitendo vyote vinavyozuia kueneza kwa amani, rehema na uadilifu baina ya watu katika Mashariki na Magharibi, na kuanzisha mradi timilifu wa kibinadamu utakaotusaidia kuwa na athari chanya katika mwendo wa matukio yanayojiri, huenda tukawa na matendo mema mbele ya Mwenyezi Mungu yanayoturahisishia hesabu na lawama yake (S.W.) hapo Akhera.

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.