Kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W.): "Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia", aya hiyo inabainisha kuwa waislamu hawakuwashambulia makafiri kwanza, bali kinyume waislamu waliruhusiwa kupigania vita vya kujilinda kutoka uadui waliopatwa nao, kwa hiyo kitenzi kilikuja katika kauli ya kutendwa jambo linalomaanisha kuwa sababu ya kuteremshwa kwa aya hiyo ni kutokea mashambulizi juu ya waislamu na wsio waislamu.