Jiahd katika falsafa ya Uislamu haipitishwi kwa ajili ya kupanua eneo la dola la kiislamu, au kuzikalia ardhi, au kudhibiti rasimali ya watu wengineo, au kuwashinda watu na kuwadhalilisha, au mambo yo yote mengineyo kati ya malengo ya kimada yanayosababisha kuzuka vita katika staarabu kubwa zaidi duniani hapo zamani na katika enzi ya kisasa, bali Jihad imepitishwa kwa ajili ya kujitetea na kujibu uadui wo wote.