Majibu ya Mawazo Makali

Kuuwa kwa sababu ya Madhehebu

2

  • | Wednesday, 11 January, 2017

Wamesema kuwa uhai katika njia ya Mwenyezi Mungu Ni nzuri zaidi kuliko kufa katika njia yake, Na kwamba uhai katika Uislamu una cheo cha juu, kwani Uislamu umekuja ili kusisitiza kustawisha ardhi, ukazingatia kushambulia mwili wa binadamu pasipo na haki ni sawa na kushambulia Ubinadamu wote, basi Mwislamu katika hali zake zote hupaswa kudhibiti matendo yake kutokana na kanuni kuu isemayo: "Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu” (Al-Baqara\208), kwa kweli yanayotukia hivi sasa miongoni mwa mauaji kwa sababu ya jinsia, ukoo, dini au madhehebu huashiria kuenea upya kwa ubaguzi uliokuwa umeenea katika zama za waarabu wa kale hapo katika enzi ya Jahiliya, ule ubaguzi uliokataliwa na Mtume (S.A.W.) ambaye ameulaani kwa kauli yake: "Basi muacheni kwani ni mbavu" akimaanisha ubaguzi, (imesimuliwa na As-Shaykhan na wengineo).

Kwa kweli Kuua kwa hoja ya mwelekeo ya kidini au nyingine… ni alama inayopandwa juu na makundi ya kikatili ili kuzidisha fitina ya kimadhehebu inayosababisha umwagaji damu pasipo na haki ila kwa sababu ya kujiunga na dini au madhehebu au ukoo tofauti.

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.