Uislamu Wahimiza wafuasi wake kuishi pamoja na wafuasi wa dini nyinginezo kwa amani

  • || Thursday, December 15, 2016
Uislamu Wahimiza wafuasi wake kuishi pamoja na wafuasi wa dini nyinginezo kwa amani

Tangu Mwenyezi Mungu Alipomshusha Aadam katika ardhi basi Manabii, Mitume wamekuja kizazi baada ya kizazi kwa dini za mbinguni ili kuwageuza watu kutoka giza kwenye mwangaza, na ili watu wapate usalama, furaha, na uwongofu wao. Kwa hakika dini zote za mbinguni zimekubaliana kuwa ni dini zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu. Na malengo yake ni kuhakikisha utumwa wa kweli kwa Mwenyezi Mungu peke yake, na kuihuisha ardhi kwa mujibu wa mbinu ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo Uislamu unakubaliana na dini zilizoteremshwa kabla yake kama vile Ukristo kwa mfano kuhusu misingi hiyo na nyingine kama vile huruma, uadilifu, usawa, uhuru, ushirikiano na maadili mema, licha ya kuharimisha dhuluma, kuua, kuiba na tabia mbaya. Pia Uislamu umeashiria kwamba machimbuko ya ubinadamu ni moja hayatofautiani kabisa kwa rangi, ukabila, au lugha, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: (Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi) (AL-Nisaa:1). Pia Uislamu umebainisha kuwa kuna nafasi ya kutosh ya kuishiana na wengineo kwa uadilifu na ihsani, Mwenyezi Mungu Amesema (Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu). (Al-Mumtahanah:8). Na wakati alipohama Mtume (S.A.W) kutoka Makkah kuelekea Madinah na akaanza kuunda mfumo wa nchi ya kiislamu iliyotanda mpaka aghalabu ya maeneo ya peninsula ya kiarabu iliyokuwa inakusanya makundi mengi kama vile Al-Ansaar, Al-Muhajiriin, Mayahudi na wengineo, na kipindi hiki kimekusanya mikataba mingi, barua na vitabu vinavyoainisha uhusiano wa kisiasa na kijamii kati ya waislamu na wasiokuwa waislamu. Na katika zama ya makhalifa waongofu, wasiokuwa waislamu wamepata usalama na amani kama walivyozipata katika zama ya Mtume (S.A.W.), ambapo Makhalifa wamepitisha kwa wakristo wa Najran yale yale waliyoyapata katika zama ya Mtume (S.A.W)  wakati wa uhai kwake. Mayahudi na Wakristo katika zama ya utawala wa Umar Bin Al-Khattab (R.A.) walikuwa wakiishi katika hali ya amani, hata wakati Umar Alipoingia Palestina amewapa uhuru wa kunufaika kwa haki zote.
Na hivyo hivyo katika zama zilizofuatana, na katika enzi ya Banu Umayyad, kama alivyosema William James Durant katika kitabu chake (Kisa cha Ustaarabu)13/130:
"Hakika Wakristo, Wazaradishti, Mayahudi na Masabai katika zama ya ukhalifa wa Banu Umayyad walikuwa wakipata kiwango cha kusameheana kisicho na mfano ikilinganishwa na hali zao katika nchi za kikristo siku hizi. Hakika walikuwa wana uhuru katika kutekeleza ibada za dini zao, na wameendelea kumiliki Makanisa na Mahekalu yao.."
Kisha katika enzi ya Banu Abbas; enzi ya ustawi wa ustaarabu wa kiislamu, watu wasiokuwa waislamu wamepata nafasi ya kuwa mashuhuri zaidi kama vile Girgiis Ibn Bakhtishoo aliyekuwa daktari wa khalifa Abu Gaafar Al-Mansour, na Gibraiil Ibn Bakhtishoo daktari wa Haruun, ambaye Al-Rashiid alimsifu akisema: ye yote anayehitaji kitu kutoka kwa mimi, basi  amwulize Gibriil na kumfahamisha haja yake: kwani mimi natekeleza kila anayenitaka kulifanya, na pia Masweih ambaye Al-Rashiid alikuwa akimpa Derhamu elfu kila mwezi na anampa kila mwaka Derhamu elfi ishirini (Uislamu na Wakristo, kitabu cha mwalimu El-Kharbutli ukurusa wa 170).
Na wakati waislamu walipoingia nchini Uhispania hapo mwaka 711 anasema mtungaji wa kitabu cha “Kisa cha Ustaarabu” 13:282 (waislamu waliokuja wametendeana na raia wa Uhispania vizuri, na hawakuchukua cho chote kwa nguvu isipokuwa ardhi za waliowapigana nao, na hawakufaradhisha kwa raia wa nchi hiyo kodi ya ziada isipokuwa zile kodi zilizokuwa zimefaradhishwa na wafalme wa magharibi ya Al-Quut, wakawapa uhuru wa kidini usiokuwa na mfano nchini Uhispania isipokuwa katika wakati chache sana.
Na katika nchi za kiislamu za Al-Andalus mtungaji huyo amesema kuwa nchi za Al-Andalus katika historia yake ndefu hazikupata utawala wa kuzingatia huruma na uadilifu isipokuwa baada ya ujio wa waarabu.
Basi, Hayo yote ndiyo mifano ya kihistoria na ya kweli ambapo Uislamu inayobainisha kwamba Uislamu husisitiza kuishiana pamoja na wasio waislamu kwa kuzingatia matendeano mazuri, mpaka wengi wa wafuasi wa dini hizo wameshuhudia kwamba hawakupata neema ya usalama, utulivu, na amani isipokuwa pamoja na waislamu. Na kwamba kuwepo baadhi ya hitilafu kati ya wanadamu, hata hitilafu hizo zikiwa za kidini, basi hazizuie kusaidinan katika mambo mengi ya pamoja, bali ni lazima wanadamu wote wasaidiane pamoja ili baadhi yao wakamilishane pamoja kwa ajili ya kupata furaha kwa wote. Na Uislamu unapambanua baina ya wanaoupigana vita na wasioupigana, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: “Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu, na Mwenyezi Mungu ni Mweza, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 8. Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu. 9. Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu". (Surat Al-Mumtahanah:7-9).  
Na Mwenyezi Mungu Anajua Zaidi

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

Name:
Email:
Subject:
Message:
x